Hili tusi la Siku hii ya Valentine limenitafakarisha

sabuwanka

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
690
751
Wana MMU hongereni kwa kuona siku ya valentine ya 2020! Nikiwa natoka kwenye mihangaiko ndani ya Costa...Kuna mama jirani alikuwa na mtoto wa kiume mwenye mwaka Kama 1 na nusu hivi maana alikuwa ananyonya...na alikuwa akilia kwa muda mrefu huku akiwa anafurukuta Kama vile anashindana na mama yake...

Tukiwa tunaendelea na Safari na kelele za dogo mithili ya mtoto aliyechomwa sindano na nesi mage, konda wa Costa akamtazama mtoto Kisha akaropoka kwa nguvu" muone jinsi unavyomsumbua mama yako...halafu ukikua uende kuanza kujenga ukweni" watu wote tukaanza kucheka Hadi mama mtoto nae akacheka...

Konda akaongeza sie wanaume shida Sana unahangaika na mama yako ukifanikiwa kupata pesa unaanzisha ujenzi ukweni kabla ya kwenu...

Halafu Kila siku unampiga tarehe mama yako kuwa kuwa nitakujengea Mambo yakiwa mazuri" mwisho wa nukuu,

Nimetafakari Sana Jambo hili siku hii ya Valentine's day of 2020
 
Lakini haya mambo ya kukaa kizembe unasubiri eti watoto waje wakujengee haijakaa vizuri! Umetangulia kuliona jua alafu unasubiri dogo aje akujengee? Utasuburi sana! Huu ni ubwege uliopitwa na wakati. Mzazi umridhisha mtoto na sio mtoto kumridhisha mzazi!
 
Kujenga ukwen au kwenu ni tatizo


Jenga nyumba yako zinazo patikana wekeza zikusaidie izeeni sio kujifanya unajua kuwajengea wazazi



Kwani wao walikuwa wapi kujijali mpaka wewe uwajali

Tumia muda na nguvu zako vizuri nawe usije subiri wakwe na watoto wako waje wakujengee
Hapana ndg..kama ana nafasi fanya tu kwa wazazi hata kama ni pande zote..la muhimu ujali pia familia yako kwanza..kiukweli wazazi walihangaika kutulea mpaka tulipo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoto wa kiumeni mara nyingi tunazikosa baraka za Mungu kupitia wazazi wetu kwa mambo mengi yanayofanana na hayo.

1. Wazazi wana nyumba mboovu lakini ukweni umewajengea.

2. Wazazi hawana kitanda kizuri ila mtoto mjini anaitwa Pedezsee la mjini.
Kitanda cha toka unazaliwa!
Godoro la tokea alizaliwa bibi, hadi mjukuu analitumia!

3. Chakula ndiyo usiseme kabisa!
Wazazi wanakula mlenda na mchicha kila siku ila mtoto wao mjini hadi chakula kinamwagwa!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio tu watoto wa kiume, mimi nilijipendekeza kufanya finishing ukweni utafikiri kwetu shida zimeisha....wakati huo mahaba yamenitia upofu. Nilipoona true colours za walimwengu na matukio niliyopigwa nilifyata mkia kama mbwa mgonjwa nikarudisha kihere here changu kwetu.
Sasa wamekosa mwana na maji ya moto wanaishia kuntangaza kwa ubaya.Mwenzao nimepiga hatua mtoto wao karudisha mpira kwa kipa kaoa mke wanaishi hapo hapo ukweni.
Nimeamini baraka ya mtoto iko kwa wazazi wake na sio ukweni!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabongo bhana, watu simple, maisha yetu simple tu, kila kitu kina jibu simple tu, sasa mtoto analia unasema anamsumbua mama yake, kama anaumwa je? Kulia ndo njia pekee mtoto anaweza kuitumia kuelezea hisia zake kwani hawezi kuongea kama wewe na mimi.
Ahahahahahah.Mkuu umeongea ukwel sana na umenikumbusha quotation hii moja ilinifilirisha na kunichekesha at same time.Inasema

" KUWA MTOTO NAPO NI KAZI KWELI KWELI, UNAWEZA UKAWA UNALIA KWASABABU MATAKO YANAKUUMA,HALAFU SISI AS A RESULT TUKAKUPIKIA UJI KWA KUDHANI UNALIA NJAA"

nimemaliza
 
Back
Top Bottom