babe hizi zambarau zinanikumbusha mengi na huzuni.. zamani sana tulikuwa tunaenda kurasini na kuvuka kwenda upande wa kibada.. Siku yangu ya mwisho kwenda kuangua zambarau ni pale rafiki yangu wa utoto (wenyewe tulikuwa tunamuita Juma bondia) alipoanguka toka juu ya mzambarau.. urefu wa kama mita 20 hivi.. Sintoisahau hiyo siku.. nakumbuka alipofika chini akili zetu za kitoto zilitutuma kukimbia na kila mtoto alirudi kwao kimya.. Nakumbuka ilipokuja kugundulika nilikula kibano cha haja toka dingi.. Mshkaji wangu alifia hospital baada ya kufikishwa na wavuvi waliokuwa maeneo ya karibu..
RIP Juma Bondia..