Hili linakuwaje?

Princess21

JF-Expert Member
Oct 15, 2015
272
266
Wadau habari ya asubuhi, natumai kumekucha salama huko kwenu. Kuna kijitabia kibaya sana kimeibuka na watu wamekifumbia macho sjui wadau mnalionaje hili:

1. Mtu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na shemeji yake, na wakati huo wanaishi nyumba moja na mwenye mume/mke

2. Mtu kuwa kimapenzi na baba mkwe wake na inafikia mahali adi anabeba ujauzito

3. Mtoto wa kambo kuwa na husiano wa kimapenzi na baba wa kambo, na kila mmoja anaona ni sawa

Kiukweli swala la mahusiano ya kimapenzi yamekuwa ya kawaida sana, kiasi kwanba mtu anaweza kuwa na yeyote amtakaye hata kama ni ndugu wa damu. Wewe mdau nini mtazamo wako, je? Hii nayo imeigwa kwa wazungu au tumewazidi? Nini kifanyike kukikomboa kizazi chetu kinachokuwa?

Watoto wetu watarithi nini? Wanajifunza nini huko majumbani?
 
pole mkuu!!!Inaelekea janga limekukumba hadi hujalala!!!!! km ni baba / mam wa kambo kwanin ukae na mtot asie wake????? Hasa vibint!!! kwann muishi na wakwe??? akikutongoza utakuw na ubavu upi wa kumwelez mmeo / mkeo juu y tabia chafu za mama /baba yake????? Matatz mengne tunaysogez karbu cc wenyewe
 
Mambo hayo siku hizi watu wanayachukulia poa zamani baba mkwe kusalimiana na mkwe wake ilikuwa ni kwa kuviziana hawawez kukaa pamoja wakapiga stories lakn now days ni kawaida sana hata kutoana out baadaye shetan atawapitia maana ndo anayewapitia watu siku hizi na wao bila kukataaa wanajikuta wamezin tayari bila kuwa na aibu wanaendeleza, pili wanawake wengi siku hizi uvaaji wao umekuwa shida toka majumban mpaka barabarani na maeneo mbali mbali tunawaona, mwanamke akiwa nyumbani anaweza akashinda na kanga moja toka alipoamka na ndan ya kanga amevaa nguo ya ndani tu kama hapo kuna baba mkwe unategemea nini si tunawaona wengine wanatembea hivyo hivyo upepo ukipuliza mambo yote hadharani, tatu hofu ya Mungu imepungua sana tofauti na miaka ya nyuma siku hiz kwenye nyumba za ibada watu hawahudhurii kabisa bila kwenye shughuli za mtaani hawakosi hii imekuwa tatizo sana anyway niishie hapa
 
Hayo mambo yapo huko kwenu tu. Huku kwetu bado sijayashuhudia.
 
Watoto watajifunza kwamba mdogo wao ni baba yao mdogo pia . Walaumiwe wanaume since it is a man's world
 
Kwani ni watu gani ambao dini zimekataza, kuwa sio halali yako?
 
Kwani ni watu gani ambao dini zimekataza, kuwa sio halali yako?
Wewe unahisi una haki ya kuwa na kiumbe chochote chenye jinsia ya kike? Ok basi nikukumbushe mama yako, dada zako, bibi zako, watoto wa kike wote ambao ni ndugu zako wawe HALALI YAKO
 
Kwa wakati wa sasa hivi viumbe wengi nyuso zao hazina haya na wala hazijui vibaya.
 
Bad habits are like a comfortable bed, easy to get into, but hard to get out of.
 
Back
Top Bottom