Hili letu ni bora bunge na si bunge bora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili letu ni bora bunge na si bunge bora

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Jun 23, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,020
  Likes Received: 37,754
  Trophy Points: 280
  Watanzania sasa tunavuna kile tulichopanda baada ya kupeleka wawakilishi wengi wa chama kimoja ambao wao kwao kitu muhimu ni chama kwanza na mwananchi baadae.Inasikitisha kuona namna ambavyo wanatumia wingi wao bungeni kupitisha mambo ambayo hayana tija na mwisho wa siku anaeumia ni mwananchi wa kawaida.
  Katika mambo ambayo nilitarajia wangesimama kidete ni kuhakikisha mishahara ya watumishi inapunguziwa kodi kwani mishahara ni midogo sana na bado inatozwa kodi kubwa.Wao wenyewe wanaona posho ya sh 150,000 kwa siku haitoshi sasa mbona hawajiuliza huyu mtumishi ataishi vipi kwa mshahara wa sh 170,000 kwa mwezi.
  Jambo lingine miongoni mwa mengi ya kuudhi ni kuona wameruhusu kampuni ya Kiwira itengewe sh bilioni 40 licha ya hasara kubwa iliyosababishwa na mwekezaji wa mgodi huu.Kwanini hawakupinga jambo hili la kifisadi!Hivi hizo pesa zingeelekezwa kwa madaktari si zingeepusha mgomo.Hata kama si kwa madaktari zingeweza kusaidia ktk maeneo mengine.
  Hiyo ni mifano michache tu ya mapungufu ambayo ni ya wazi kabisa lakini watu hawa wameziba masikio na kutia pamba masikionoi wakiwaacha watanzania wanaangamia ktk dimbwi la umasikini.Na kinachouma ni kuona namna ambavyo wanashangilia na kupiga meza kanakwamba wamepata uungwaji mkono kutoka kwa wanaowawakilisha.Sijui labda huwa wanapigiwa simu za pongezi baada ya kupitisha.
  Mh.Tundu Lisu aliposema this is another silly season hakukosea kabisa na mimi naunga mkono kauli yake kwa asilimia mia moja kama wao wanavyounga mkono kwa asilimia mia moja hizo bajeti tata.
  Acheni siasa kwa mambo muhimu ya kitaifa na siasa mkafanyie majukwaani na sio humo bungeni.
  Binafsi huwa nashangaa kusikia spika anaanza kwa maombi( maarufu kama dua ya kuliombea bunge) alafu kinachofuata ni dhambi kwa watanzania, tena kwa kila kikao bila kujirekebisha.
   
 2. I

  Idofi JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 1,542
  Likes Received: 820
  Trophy Points: 280
  wakiambiwa dhaifu wanapiga kelele kweli rais, waziri mkuu wabunge wa ccm ni dhaifu, watz tuna safari ndefu sana ili tufike vinginevyo mateso ya jahanamu tunaanza kuyapata hapa hapa duniani
   
 3. mutabilwa

  mutabilwa JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi wanabord naomba nijaribu kujenga hoja yangu kwamba tumefika wakati ambapo tuanze kutembelea website ya BUNGE na tuanze kumuuliza Spika yale tuyaonayo ni mapungufu kwake, na tumuombe awe anajibu hoja zetu make ckutegemea mtu mkubwa kama yy kufumbia na kuizima wazwaz issue ya KIWIRA wakati tunaoitaji majibu ni wananchi hasa na si wabunge tu?
   
 4. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,589
  Likes Received: 16,542
  Trophy Points: 280
  Na pia kumwambia aache upendeleo wawazi.Pili awe kitaifa zaidi kuliko kichama.
   
 5. M

  MTK JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280

  Hayo yote mbwembwe na makeke na fikira zao za umimi vitaisha tu pale watanzania katika ujumla wao watakapozinduka na kujitambua na wakaamua kujiletea mabadiliko ya kweli kumaliza upuuzi wote huu. athe country need fundamental change.
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Tatizo bi kiroboto hana uwezo wa kuongoza nawaonea huruma wananchi wa jimbo analoliwakilisha na waTz kwa ujumla maana udhaifu wake unaathari kwa wote na hao hao wabunge wa ccm ndo waliosababisha yote hayo,
  kama jimbo lako lina mbunge wa ccm jua na wewe umechangia yote hayo!
   
 7. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,020
  Likes Received: 37,754
  Trophy Points: 280
  Jimbo langu kwakweli lina mbunge wa ccm ila ni bahati mbaya sana mimi ni mhamiaji wa hivi karibuni kutokana na sababu za kikazi.Jimbo lenyewe liko mjini kabisa ila ni katika ile mikoa ambayo ni choka mbaya isiyo na maendeleo lakini wao ccm ndio kama mungu wao kwani kuanzia mwenyekiti wa kijiji mpaka raisi walichagua ccm kwani ndio walioibuka washindi.
  Hata nilikotoka sikuchagua ccm na kamwe siwezi kuwachagua labda niwe nimelogwa.Na bahati nzuri mimi sio kipofu au kiziwi.
   
 8. B

  Bob G JF Bronze Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Watanzania hawatarudia makosa yaleyale wakati wa uchaguzi 2015, Gharama ya Mazoea Mabaya ndo hii ya kujaza wabunge wa ccm wanafiki na DHAIFU
   
Loading...