Mnafiki! huwezi kumtenganisha JK na Lowassa hata kidogo, kukubali kuwa wewe ni CCM na kuwagawa hawa wasafi na hawa wachafu...hutafiki mbali
hakuna msafi CCM si wewe si bosi wako Membe na mjomba wako Kikwete!
Aibu!!!
Kwa kweli ninasikitika sana kwa watu kuitumia vibaya jamii forums kulisha maneno watu wengine
1.nchimbi hajapata kusema mahali popote wala kulalamikia kwa familia ya Mwalimu Nyerere kutohudhuria.
2.Shughuli ya kumuenzi Mwl Nyerere itaendelea kuwepo hata kama hakuna mjukuu wake butiama.nyerere si mali ya familia ni mali ya watz wote
3.Kwani miaka mia baadae wakati familia yake haitakuwepo watu hawatakuwa wanaenda tena Butiama ama itakuwaje
4.Nani kasema kuwa nchimbi hana analoweza,hata kuweza kukaa ktk siasa kwa muda mrefu pia ni kujua jambo.
End of the day mwanasiasa makini ni yule anaeweza kudumu ndani ya siasa.kumsaidia Membe kuwa rais wala sio kumsifu kwa kwenda butiama na kupokelewa huko....Wizara ya Nchimbi itakuwa tena tar 14 kuwasha mwenge ni wazi kuwa kama ni muhimu hao watu na atawaalika
Huyu nchimbi upeo wake wakufikiri ni mdogo saana.Amesoma kwa kuungaunga tu na mpake leo hajatuambia Phd yake kama ni halali au la.Tatizo langu na nchimbi nikuwa na uelewa mdogo katika mambo hata ya kawaida kabisa.Mnafiki! huwezi kumtenganisha JK na Lowassa hata kidogo, kukubali kuwa wewe ni CCM na kuwagawa hawa wasafi na hawa wachafu...hutafiki mbali
hakuna msafi CCM si wewe si bosi wako Membe na mjomba wako Kikwete!
Aibu!!!
Pamoja na kwamba kuendeshwa na ideologies za CCM si jambo la aibu kiasi cha mtu kulikwepa, mimi siyo mwanachama wa CCM na sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote. Lakini kwenye masuala ya kitaifa issues za chama zinakuja baadae. Huwezi kunitarajia kumuunga mkono Lowassa (hata kama angekuwa hagombei urais) wakati najua kwamba huyu bwana ni mchafu na ni mtu ambaye ni adui kwa ustawi wa mtanzania maskini. Na wala huwezi kumfananisha JK na Lowassa, kwa matendo na itikadi kwa sababu unapozungumzia maadili JK yuko kushoto na Lowassa yuko kulia. Labda unachosema wewe ni kwamba dhambi ya JK ni kuwateua hao wawili. lakini kuwateua ni kuwatuma wakatende mabaya waliyoayatenda? Mbona wengi wa wateule wake wengine ni waadilifu? Sijutii kusifia yale mema yanayofanywa na JK hata kama kufanya hivyo ni kuonekana mana CCM.
Unapozungumzia suala la 2015 na kunihusisha mimi na harakati hizo, unaingia kwenye mkubo wa watu wanaodhani kwamba kusifia jema ni kumfagilia mtu kwa 2015 na kukemea maovu ni kumvurugia mtu kwa 2015. Hilo hatuwezi kulikubali maana linatufanya tuwe wanafiki na waoga wa kutoa maoni ya wazi na ya kweli kwa hofu tu ya kuonekana tunampinga mtu kwa sababu ya ambition zake. Juu ya wewe kudai Nchimbi ni sawa na wengine, then hiyo ni self defeating kwa sababu mbona Waziri wa CCM aliyefuata hakufanya madudu kama hayo? Labda wewe mwenzangu umewekwa kwenye mtego wa kupenda chama chako kuliko nchi, au kupenda mtu kuliko nchi ndo maana mada zako zinaangalia mtu kuliko hoja.
Hizo blanket accusations zako dhidi ya JK bila kuwa na hoja ambazo mimi na watu wa aina yangu zitatubaidilisha msimamo au mtazamo wetu hazikupi heshima na kinyume chake unaonekana ni mtu ambaye anaendeshwa zaidi na chuki . Kila siku tumekuwa tuki-demand tuambiwe uchafu wa JK au hata huyo Membe lakini stori zinazokuja hapa ni kwamba wanajipanga kwa 2015. Wewe ambaye unasema Lowassa na Kikwete ni one and the same ndiye mwenye onus ya kuthibitisha hilo maana matendo ya Lowassa yanafahamika kwa ushahidi na hatujafika hatua ya kumuona hivyo kwa hisia au kwa kukurupuka.
Mimi nimekuambia kwamba sijawahi kuwa CCM wala chama chochote cha siasa and I am happy this way. Lakini siwezi kuingia kwenye fashion ya kudhani kuitukana CCM pasipostahili na kuisifia CDM pasipostahili ni uzalendo. Upumbavu uitwe hivyo unapostahili na hivyo hivyo ustaarabu. Kwa vile wewe unawiwa na allegiance ya chama chako, ndio maana kila wakati unajikuta ni mateka wa kushabikia kila linalofanywa na chama chako na hivyo hivyo kuponda kila linalofanywa na chama pinzani na chako. Grow up man!
Hivi na Membe alipoenda na mabalozi waliwasiliana na familia ya Nyerere? familia ilikuapo?