Hili la Nape kupita kwenye migongo sio udhalilishaji kwa Mama zetu?

kiwatengu

Platinum Member
Apr 6, 2012
18,404
16,421
Wakuu! Nape kupita juu ya miili ya hawa kina mama imekaaje?
Bado kuna tamaduni kama hizi kandamizi namna hii?

Hivi endapo kama mke wako/mtoto wako ni mmoja waliokanyagwa na Nape utachukua hatua gani?
1ae1b913b6cbdb9a288b08e3d273c726.jpg
 
Mambo mengine kama hamfahamu ulizeni kwa nidhamu muelekezwe.

Ulichoandika hapa kinaashiria jinsi mitaala yetu isivyofundisha mambo yaliyopita kwenye jamii na mila zetu. Tunajisikia fahari kujifunza kufunga tai wakati hatujui tamaduni zetu!
Mkuu nimehoji kuhusu huo utamaduni au hizo mila nimeweka alama ya ulizo, jibu sasa kama unaufahamu wa mila hizo
 
Mkuu nimehoji kuhusu huo utamaduni au hizo mila nimeweka alama ya ulizo, jibu sasa kama unaufahamu wa mila hizo

Umeshaambiwa ni mila. Kila Makabila yana Mila zao.
Tanzania tuna makabila zaidi ya 120. Mtwara na Lindi kuna makabila mengi Wamakonde, Wamawiya(mawiha) ,Wamakuwa, Wamwera Wangindo,Wamatumbi.

Tamaduni na mila zao ni tofauti na Wabondei ,wakibosho,wamanyema, wandali, Wandamba.

Tambua pia kwamba katika makabila yetu haya heshima kutoka kwa jinsia ya kike kwenda jinsia ya kiume haijalishi umri ,ukoo , cheo nk.
Huyo ni mtoto wao, kaka yao, mjomba wao hawana budi kumpa heshima yake.

NB: Hicho kitendo ni fasihi kubwa sana. FASIHI ONESHI.
Mwenye macho na aone.
 
Back
Top Bottom