Hili la Mawaziri Kutaja Jina la Mbunge Mmoja Mmoja Waliochangia Hoja Lina Mantiki Yoyote?

Kingcobra

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,000
309
Wakuu,

Kama kuna jambo linalonikera mjengoni wakati wa kikao cha bajeti ni pale mawaziri wanapoamua kutaja majina ya wabunge mmoja mmoja waliochangia hoja yake. Mawaziri takribani nusu ya muda aliopewa kutaja majina ya wabunge na muda mfupi unaobaki eti ndiyo anajibu hoja zao. Tafadhali wajuzi watuelimishe hapa, hivi kweli tabia hiyo ina maana yoyote? Mimi naona kama ni kupoteza muda tu.
 
watafanya nini hali hawana hoja?
Hawajui kwa nini ni mawaziri?
Hawaajui job responsibility zao?
 
kuna huyu wa michezo na habari hata majina hayajui anatamka utafikiri sio mtz
 
Ndugu yangu hilo ni suala la kanuni zinamtaka mtoa hoja kuwatambua kwa kuwataja majina wachangiaji. Ni muendelezo wa kanuni tulizoachiwa na mzee 6. Kanuni nyingi mnazozipigia kelele kuwa ni mbovu ndio matunda ya mzee 6 hayo. Na mama makinda mnamfahamu ni mtu wa kanuni sana. Ushauri wangu hakuna haja ya kutaja majina!
 
....Udhaifu! Leo Mukangara ametumia zaidi ya 10 KUSHUKURU! Hivi wanashindwa kutoa shukrani zao mpaka wawe Bungeni?
 
Yaani kuleta hii kitu umenikera na kuniharibia siku yangu kabisa.Mijitu inataja majina miambili hamsini yote halafu inachangia kidogo tu,na muda unaisha.Haya ni matumizi mabaya kabisa ya muda.Hili likanuni silipendi kabisa,bora lifutiliwe mbali kabisa, tupa kule kabisa aaaaaaghhhhhhh!!!!!!
 
huo ni ujinga na upumbavu wa wabunge wote wanaotajataja majina bila sababu yeyote mi nadhani ni utotezaji muda mwishowe watainda kuwashika kwa mikono sehemu walio kaa
 
....Udhaifu! Leo Mukangara ametumia zaidi ya 10 KUSHUKURU! Hivi wanashindwa kutoa shukrani zao mpaka wawe Bungeni?

Dr Mgimwa alitumia si chini ya dakika 29 kushukuru, Naibu wake akatumia another 10 kufanya hivyo hivyo. Kwa ujumla Tanzania hatuna bunge la wananchi kuna Bunge la wabunge na familia zao.

Bila haya wala huruma badala ya kujadili matatizo ya wananchi wanatumia muda huo kutambulisha wanafamilia wao na wageni wao! Hata kwenye speech - wabunge wa vyama vyote, wanashukuru watoto, waume, wake zao! Na wakati wa mjadala badala ya kujadili sheria na utekelezaji wa kazi za serikali wanapongezana na kutukanana! Hatuna bunge.
 
Hivi kweli huyo waziri ni mtanzania kweli au hajui kusoma vizuri?nimeona jina lake limeanza na Dr.
 
watafanya nini hali hawana hoja?
Hawajui kwa nini ni mawaziri?
Hawaajui job responsibility zao?
mawaziri,
wabunge wa tanzania huwa wapo ili wapate posho tu, lakini hawana hoja wala mtazamo ndio maana wanapoteza muda, maoni yangu muda wanaopewa upunguzwe labda utalingana na akili zao fupi
 
Ni lazima awataje ili kuonyesha kwamba wamo bungeni na wanachangia. Mimi nilishasahau kama tuna mbunge anayeitwa Juma Kapuya. Kwa hiyo wanatajana kwa majina ili wajulikane majimbo kwamba wamechangia kwa maandishi. Kuna wabunge waliowahi kuwa mawaziri zamani hawa hawasimami kabisa kuchangia. Kwa hiyo kwa kuwataja watajulikana wamechangia. Ni namna ya kuwalinda kwa wapiga kura wao hasa hawa wanaochangia kwa maandishi.
 
Kutajana majina yote ya wabunge waliopo kwenye kikao ni uhuni na ujambazi. Hici katika hali ya kawaida inaleta mantiki waziri kutumia nusu ya muda kushukuru wabunge wote mmoja mmoja pamoja na mke/mume na watoto wake na ndugu na jamaa wengine then anatumia nusu nyingine kujibu hoja. Nchi hii aijui ni nani aliyeturoga?
 
Fennela Mkangara jana kaumbuka kutaja majina ya wabunge, halafu kwa UDHAIFU wake akawa anajicheka mwenyewe. majina hayana maana ni kupoteza muda tu.
 
Wakuu,

Kama kuna jambo linalonikera mjengoni wakati wa kikao cha bajeti ni pale mawaziri wanapoamua kutaja majina ya wabunge mmoja mmoja waliochangia hoja yake. Mawaziri takribani nusu ya muda aliopewa kutaja majina ya wabunge na muda mfupi unaobaki eti ndiyo anajibu hoja zao. Tafadhali wajuzi watuelimishe hapa, hivi kweli tabia hiyo ina maana yoyote? Mimi naona kama ni kupoteza muda tu.

Ndio njia pekee ya kutumia muda waliopewa kujibu hoja; kutokana na kutokuwa na majibu ya michango ya wabunge wanawapotezea kwa hivyo
 
ni muhimu sana,ili wananch wajue kama hoja imepata wachangiaji wengi au la,alafu n kutambua mchango a mp husika kwny hoj
 
Back
Top Bottom