Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,887
- 2,769
Nimemsikia rais jk akimwagiza dk bilal awe anaenda kutoa lekcha pale UDOM kwani habanwi na majukumu kivile. Hili lina athari gani kwa chuo na serikali kwa ujumla. Mojawapo ni wananchi kuamini kuwa umakamu rais ni kazi moja rahis rahis tu
JK kamuzalilisha mwenzake, kwani hayo hakupaswa kueleza hadharani bora angemwacha afundishe tu
Hiyo ni sifa kubwa aliyopewa Dr. Mohamed Gharib Bilal.
Kwanza ana wanafunzi wa Phd ana wasimamia, jee mlitaka awaache solemba? Kwa kushauriwa aendelee kuwahudumia ni wazo jema la kuwafikiria na hao wanafunzi pia.
Pili, kwa kuendelea kufundisha kwa Nuclear physics, kutamaanisha gap haipo pale UDOM na itamfanya asiache fani yake hiyo, amabayo ni waTanzania wachache sana walio nayo kwa kiwango cha Dr. Bilal.
Tatu, ni katika kuandika historia ya nchi yetu na kuwajulisha ma-professor wengine kuwa, msiache mbachao kwa msala upitao, yaani wasiiwache fani yao kwa kuwa tu wamepata kazi ya uongozi.
Dar Es salaam.
Bilal si Phd holder? Nifahamishe hapo kama Phd holder anweza kumsimamia mwanafunzi mwingine anayetafuta Phd, sbb nilichokuwa nafikiri mimi ili uweze kumsimamia mwanafunzi wa Phd lazima wewe uwe prof. Naomba kueleweshwa hapo.
Kijana hiyo pia si afadhali jamaa ana Phd na ana experience ya miaka mingi na research publication nyingi. Lakini nenda MUHAS(muhimbili) nenda kaone huko jinsi mtu ana master tu na hana publication hata moja anasimamia wanafunzi wa masters.... Hatari kweli kweliDar Es salaam.