Hili la makamu wa rais kufundisha limekaaje

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,769
2,544
Nimemsikia rais jk akimwagiza dk bilal awe anaenda kutoa lekcha pale UDOM kwani habanwi na majukumu kivile. Hili lina athari gani kwa chuo na serikali kwa ujumla. Mojawapo ni wananchi kuamini kuwa umakamu rais ni kazi moja rahis rahis tu
 
Mkuu mimi kwa mtazamo wangu sioni kazi ya makamu wa rais, na nimapendekezo yangu nafasi hiyo ingefutwa, nadhani umeona hapo kuwa hana kazi so anaambiwa aendelee tu kufundisha, yaani hata bila yeye mambo yanaenda.
 
Ni kawaida kwa JK kuropoka.... Sijui kwanini hua azingatii hotuba anazoandaliwa....
 
Kwani hamkumbuki why alipewa hicho cheo??? ilikua kumpoza kutokana na kumuengua kule ZNZ koz hakuwa part n parcel ya Cabinet yao this time...so thus y anamwambia awe anaenda kukamua mapindi UDOM
 
Majukumu aliyompa ni mepesi: kuharakisha uwepo wa mahakama ya kadhi, tz kujiunga na oic.
 
Kauli za jk huwa zinabeba maana anayoijua yeye. Mbona Shein ni Dr lakini haikuwahi kutokea kuambiwa akashike chaki?
 
JK kamuzalilisha mwenzake, kwani hayo hakupaswa kueleza hadharani bora angemwacha afundishe tu

Hii itakuwa ni zaidi ya udhalilishaji na ni tatizo la JK kutokuzingatia hotuba ndio maana anajikuta kila siku yuko off-point, huyu mkuu sijui ni kiongozi wa aina gani asiyepima kauli zake.

Eti VP awe anafundisha, kwa hiyo hapo nje ya darasa ni lazima kuwe na askari wa kutosha kumlinda, wanafunzi wote wafanyiwe screening kabla ya kuingia kwenye kipindi au kama walikuwepo watote wawe screened then waingie, kipindi si kitakuwa kimeisha kabla ya kuanza??. Na hizo kelele za ving'ora kila siku si itakuwa kero??... Poor gaffes from the president, hivi huyu president hana washauri mbona haishi kuongea kauli za masihara na zenye utata?

Ila tuna mshukuru kwa kutufahamisha kuwa VP hana kazi ndo maana hata kama atakaa dodoma mambo pale magogoni yataendelea tu.
 
Nadhani JK yupo sahihi, Makamu wa Rais wa Muungano hana majukumu ya kumfanya haache kuwakatia nondo vijana wetu pale UDOM, hiki cheo kipo kwa ajili tu ya kujenga sura ya Muungano katika uongozi lakini kimsingi hakina sababu nyingine ya kuwepo.
 
Akapige nondo awape vijana ujuzi wake mkubwa.....maana alikuwa anafundisha hadi last june
 
Hiyo ni sifa kubwa aliyopewa Dr. Mohamed Gharib Bilal.

Kwanza ana wanafunzi wa Phd ana wasimamia, jee mlitaka awaache solemba? Kwa kushauriwa aendelee kuwahudumia ni wazo jema la kuwafikiria na hao wanafunzi pia.

Pili, kwa kuendelea kufundisha kwa Nuclear physics, kutamaanisha gap haipo pale UDOM na itamfanya asiache fani yake hiyo, amabayo ni waTanzania wachache sana walio nayo kwa kiwango cha Dr. Bilal.

Tatu, ni katika kuandika historia ya nchi yetu na kuwajulisha ma-professor wengine kuwa, msiache mbachao kwa msala upitao, yaani wasiiwache fani yao kwa kuwa tu wamepata kazi ya uongozi.
 
Dar Es salaam.
Bilal si Phd holder? Nifahamishe hapo kama Phd holder anweza kumsimamia mwanafunzi mwingine anayetafuta Phd, sbb nilichokuwa nafikiri mimi ili uweze kumsimamia mwanafunzi wa Phd lazima wewe uwe prof. Naomba kueleweshwa hapo.
 
Unachoongea ni nadharia isiyokubalika kabisa. ukiendelea kufikiri kwa mtindo huo basi ukapimwe akili yako. Ni nadharia isiyokubalika siyo kwa sababu hana uwezo bali cheo alichonacho hakiwezi kumruhusu kufanya majukumu hayo. sababu za msingi za nadharia hiyo kutokubalika ni kama hizi:
1. Kufundisha chuo kikuu ni lazima taratibu zitumike, kwa mfano lazima awe mwajiriwa iwe full time au part time na lazima atasimamiwa kwamba kweli anafanya kazi hiyo na hatimaye atalipwa kwa kazi hiyo. Unadhani kama makamu wa rais ataweza kukidhi matakwa ya kazi hiyo? maana yake ni kuwa siyo kwenda kufundisha tu kwa kujifurahisha bali anatakiwa amudu kweli majukumu ya kufundisha.
2. Dr. Bilal kama makamu wa rais anapewa ulinzi na ndiyo maana anaandama na walinzi muda wote katika majukumu yake. Je, atakuwa anaingia nao kwenye vyumba vya kufundishia?
3. Ina maana kwamba majukumu yake kama makamu wa rais hayapo au hayatoshi kiasi cha kufanya hayo mengine. Sidhani kama hana majukumu ya kutosha ila nadhani watu wanakejili tena kejili za kufedhehesha na kudhalilisha kabisa.
4. Mfano wa makamu wa rais kufanya kazi ya ziada kama kufundisha unapatikana katika nchi gani? au ni vitu vya kufikirika tu? Tangu nizaliwe sijawahi kusikia hili la namna hii. nadhani badala ya kujenga historia ya maana itakuwa vichekesho mbele ya uso wa dunia.
 
Dar Es salaam.
Bilal si Phd holder? Nifahamishe hapo kama Phd holder anweza kumsimamia mwanafunzi mwingine anayetafuta Phd, sbb nilichokuwa nafikiri mimi ili uweze kumsimamia mwanafunzi wa Phd lazima wewe uwe prof. Naomba kueleweshwa hapo.

Nani alikwambia au imeandikwa wapi kumsimamia mwanafunzi wa PhD lazima uwe professor? umeipata wapi hii tumegee mkuu.
 
Mmm nafikiri JK alikuwa anatania haiwezekani makamu wa Rais akenda kushika chaki ingawa ujuzi hauzeki
 
Dar Es salaam.
Bilal si Phd holder? Nifahamishe hapo kama Phd holder anweza kumsimamia mwanafunzi mwingine anayetafuta Phd, sbb nilichokuwa nafikiri mimi ili uweze kumsimamia mwanafunzi wa Phd lazima wewe uwe prof. Naomba kueleweshwa hapo.
Kijana hiyo pia si afadhali jamaa ana Phd na ana experience ya miaka mingi na research publication nyingi. Lakini nenda MUHAS(muhimbili) nenda kaone huko jinsi mtu ana master tu na hana publication hata moja anasimamia wanafunzi wa masters.... Hatari kweli kweli
 
Gurtu na Nik wana hoja za msingi. Suala si kufundisha bali mazingira ya kufundisha. Ukifanya analysis za hao ndugu wawili niliowataja utaona kuwa kwa makamu wa rais kufundisha ni suala gumu. VP ana hadhi yake na ndio maana kuna itifaki kadhaa hufuatwa akiwa katika shughuli fulani. Tukubaliane pale jk alipitiliza
 
Nimemsikia rais jk akimwagiza dk bilal awe anaenda kutoa lekcha pale UDOM kwani habanwi na majukumu kivile. Hili lina athari gani kwa chuo na serikali kwa ujumla. Mojawapo ni wananchi kuamini kuwa umakamu rais ni kazi moja rahis rahis tu

Inawezekana, mwache atimize wajibu wake
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom