Hili la makamu wa rais kufundisha limekaaje

Nimemsikia rais jk akimwagiza dk bilal awe anaenda kutoa lekcha pale UDOM kwani habanwi na majukumu kivile. Hili lina athari gani kwa chuo na serikali kwa ujumla. Mojawapo ni wananchi kuamini kuwa umakamu rais ni kazi moja rahis rahis tu

Hebu acheni kupotosha umma ndugu zanguni, mie ndio maana nasema humu JF kule kujisifu kwetu ni GREAT THINKERS kunaondoka kabisa, na kuanza kushindwa hata Face book ambapo mtu akiweka mada watu wanachangia kwa umakini kabisa. Fanya utafiti halafu weka mada. Kilichotokea ni kuwa Makamu wa Rais yeye aliisha acha jukumu hilo la kufundisha na kukabidhi madaraka yote kwa uongozi wa chuo. Kilicho fanyika ni kuombwa na chuo aendelee kufundisha kwani ni mmoja wapo wa wataalamu wachache sana waliopo hapa Tanzania wa masomo ya Physics & Chemistry. Kilichofanyika , JK kuridhia juu ya hilo na hii haina maana kuwa atakuwepo pale full time kama walimu wengine, bali ni kwa vipindi vipindi maalum tu. Na hili sio la kwanza kwa kiongozi mkuu wa nchi kufundisha, kwani tunaona nchi za wenzetu viongozi wengi tu huenda vyuo vikuu kutoa Lectures.
 
Hiyo ni sifa kubwa aliyopewa Dr. Mohamed Gharib Bilal.

Kwanza ana wanafunzi wa Phd ana wasimamia, jee mlitaka awaache solemba? Kwa kushauriwa aendelee kuwahudumia ni wazo jema la kuwafikiria na hao wanafunzi pia.

Pili, kwa kuendelea kufundisha kwa Nuclear physics, kutamaanisha gap haipo pale UDOM na itamfanya asiache fani yake hiyo, amabayo ni waTanzania wachache sana walio nayo kwa kiwango cha Dr. Bilal.

Tatu, ni katika kuandika historia ya nchi yetu na kuwajulisha ma-professor wengine kuwa, msiache mbachao kwa msala upitao, yaani wasiiwache fani yao kwa kuwa tu wamepata kazi ya uongozi.

Hata huyo anayesimamiwa Phd yake na bilal hana akili kweli??yaani mimi na akili zangu nisimamiwe PhD na Dr..kwani maprofesa hawapo??
 
Kijana hiyo pia si afadhali jamaa ana Phd na ana experience ya miaka mingi na research publication nyingi. Lakini nenda MUHAS(muhimbili) nenda kaone huko jinsi mtu ana master tu na hana publication hata moja anasimamia wanafunzi wa masters.... Hatari kweli kweli

Tena maprofesa muhimbili karibu aslimia 98 ni master kwa kwenda mbele akiwemo Prof.Mwakyusa.Department ambazo zina watu wana PhD nI za Health Allied science.
 
Mfano Joe Biden-huko jimboni kwake kabla ya kuingia Ikulu alikuwa anafundisha sheria na bado kuna wikiendi moja moja anakwenda kutoa mhadhara.Huyo hatakuwa wa kwanza hapo nchini Prof.Sarungi mwanzoni mwa career yake ya kisiasa baada ya kuteuliwa na mwinyi waziri bado alikuwa anaenda mara kadhaa kutoa lectures na Kutwanga mzigo ktk kitengo za upasuaji mifua na majeruhi wa ajali,
 
Nimemsikia rais jk akimwagiza dk bilal awe anaenda kutoa lekcha pale UDOM kwani habanwi na majukumu kivile. Hili lina athari gani kwa chuo na serikali kwa ujumla. Mojawapo ni wananchi kuamini kuwa umakamu rais ni kazi moja rahis rahis tu

Ni wazo jema kama Dr. atapata muda wa kumwaga sera za Fizikia hapo UDOM , kumbuka itampa muda mzuri wa kufanya reserch na ku publish papers .
 
Kuna ubaya kwa JK kuwa mkweli kuwa makamu wa Rais hana kazi yoyote, bora akafundishe. Hii katiba mbovu ndio inatupa viongozi wengi na wasio na kazi. Mfumo wa umakamu wa Rais unatokea na katiba ya Amerika ambapo makamu wa Rais anakua kiongozi wa bunge la seneti. Kwa Amerika hakuna waziri mkuu, kiongozi wa chama chenye wajumbe wengi wa seneti anakuwa senate majority leader. Tanzania imeiga mfumo wa Amerika na wa Uingereza kwa wakati mmoja. mfumo wa uwaziri mkuu ni wa kiingereza na India, iSRAEL NA KWENGINE. WAZIRI MKUU ANAKUA KIONGOZI WA SERIKALI BUNGENI. Tatizo la kuchanganya mifumo ndo tunapata pumba tupu. Tujue moja tunaenda na Amerika au Uingereza. Kwa kuwa tumempa waziri mkuu dhamana ya kuwa kiongozi wa serikali bungeni, ivyo makamu wa Rais hana kazi yoyote zaidi ya kusubiri rais afe. JK nakukubali, Bilal hana kazi aende akawafundishe wajinga wa UDOM

nimeupenda uchambuzi wako hasa unaposema kazi ya bilal ni kusubiri jk afe! Nadhani wakati umefika wa kuainisha upya kazi za VP kuliko rais kumuamulia cha kufanya. Hili lifanyike kwenye mchakato wa kutengeneza katiba mpya
 
Nadhani alikuwa anatania, kama alikuwa serious basi kamdhalilisha mwenzie kwani kaonyesha uma kwamba makamu wa rais hana kazi! Dah! OMG! huyu mtu mimi huwa sielewi kama tatizo ni speech zake au ni ulimi wake!

ni huyu huyu aliyesema hataki kura za wafanyakazi. Akasema wanaoathirika ni kiherehere chao. Akasema hajui umasikini wa watanzania unatokana na nini. Akasema urais wake hauna ubia na mtu! Akasema akili za kupewa changanya na zako n.k n.k. I believe jk is more of ceremonial leader than Dr. Bilal
 
MKUU NIKUREKEBISHE KIDOGO, KWANZA HAKUMWAGIZA, MIMI NILIKUWEPO UKUMBINI WAKATI J.K ANAYATAMKA HAYO, ALISEMA ANAFURAHI KUONA UTAYARI WAKE KUENDELEA KUFUNDISHA UDOM, NA HILO JUKUMU SIO LA KILA SIKU KWANI ATAWASIMAMIA WANAFUNZI WA Ph.D , HIVYO HILO HALINA SHIDA KABISA COZ HAFUNDISHI UNDERGRADUATE WALA MASTERS AMBAO INGEMLAZIMU KUWA NA LECTURE KADHAA KILA WIKI.

nimekuelewa mkuu, lakini uelewe kuwa wakati fulani Makamba alisema mtu mzima akikosea hasemi samahani. Kikwete si lazima aseme nakuagiza, bali anadhamiria nini kwa anachoongea. Kuhusu kusimamia kazi za phd bado yataka moyo. Katika awamu ya kwanza ya jk kuwa madarakani kafika udom mara kibao. Mbona hakuwahi kumwambia Dr. shein maneno kama hayo?
 
Wote hamjui mawazo yaJK mwenzenu kasoma alama za nyakati, kajua baada ya hapa hakuna future kwa wana CCM kwahiyo wale wenye fani zao wasije wakazipoteza ndio maana kamshauri swahiba maadam hayuko bize aendelee kukamua asije LIA baadaye.
 
Gurtu na Nik wana hoja za msingi. Suala si kufundisha bali mazingira ya kufundisha. Ukifanya analysis za hao ndugu wawili niliowataja utaona kuwa kwa makamu wa rais kufundisha ni suala gumu. VP ana hadhi yake na ndio maana kuna itifaki kadhaa hufuatwa akiwa katika shughuli fulani. Tukubaliane pale jk alipitiliza

kwahiyo kufundisha kutamshushia hadhi au?
 
Technolojia inakua. Anaweza akafundisha hata akiwa nyumbani kwake. Au wadau hamlijui hilo. Sio lazima ashike chaki.
 
Kwanza huyu Dr Mohamed Gharib Bilal, huenda ni Kilaza fulani ndo maana amekimbilia kwenye siasa. Kwanini hakuwahi kuwa Prof Miaka yote alofundisha chuo kikuu, nimegoogle sijaona hata chapisho lake moja la kisayansi. Kwenye Mtandao sijaona hata article aloandika isije kuwa baada ya PhD yake aliamua kuwa mwanasiasa.

http://dkbilal2010.blogspot.com/
 
Back
Top Bottom