Hili la kupiga marufuku watoto kutumika "CCM kama chipukizi" Rais Magufuli kudos

sixgates

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
3,979
1,663
Jana Mh JPM baada ya kukabidhiwa kijiti na kuwa mwenyekiti mpya CCM alizugumza mengi.

Kwangu lipo moja ambalo nilidhani hata vyama vya upinzani wamekuwa wakilipigia kelele. Ni juu ya matumizi ya watoto kwenye siasa kwa kigezo cha kuwaita chipukizi.

JPM jana made cristal clear kwamba wale watoto waachwe wasome. Hatotaka kuona mtoto eti wa miaka nane anaingizwa kwenye hekaheka za siasa.

Kama kila chama kikianza utaratibu huo hao watoto watasoma kweli.

Vyama vya upinzani muungeni mkono Magufuli japo hili mliloliasisi nyie yeye katekeleza.
 
Vyama vya upinzani vinamuungaje mkono wakati yeye ndiyo kaviunga mkono? Au kwa kuwa yeye ni Rais? Kumbuka kuwa ni mwenyekiti kama wenyeviti wengine na yeye hakupaswa kusema amepiga marufuku. Alichopaswa ni kutamka hadharani kuwa anaunga mkono wapinzani juu ya suala la kutowatumia watoto kwenye siasa.
 
Ahsante, umeiweka clear kabisa
 
Sawasawa watoto walikuwa wanapindikizwa chuki za kisiasa mapema mno kwenye maisha yao( hasa Zanzibar). Big up JPM.
 
Vyama vya upinzani vinamuungaje mkono wakati yeye ndiyo kaviunga mkono? Au kwa kuwa yeye ni Rais? Kumbuka kuwa ni mwenyekiti kama wenyeviti wengine na yeye hakupaswa kusema amepiga marufuku. Alichopaswa ni kutamka hadharani kuwa anaunga mkono wapinzani juu ya suala la kutowatumia watoto kwenye siasa.
Mwenye kuungwa mkono ni yule mwenye mamlaka ya kufanikisha jambo likatekelezwa. Kuwaunga mkono wapinzani wa ki TZ inabidi uwe na tahadhali kubwa, hawaaminiki. Leo wataandamana kuaminisha umma EL ni fisadi kesho watasema bila yeye hakuna mabadiliko.
 
Vyama upinzani vinajitahidi sana big up maana taasisi za serikali zote macho Yao ni juu ya wapinzani Tu! Kama ccm Na miaka yake mingi Na ukubwa wao Na watu walio nao bado wanatumia Polisi kuwasaidia ni aibu! Acheni Polisi wafanye kazi yao! Nendeni uwanjani watu wapingane Kwa Hoja! Ccm ni chama kubwa acheni uoga
 
Miezi sita kuanzia sasa CCM haitakuwa hii tunayoijua bali kivuli chake!
 
Back
Top Bottom