Hili la kifo cha Dkt. Faustine Ndugulile limeniumiza sana, shida ni nini?

Hili la kifo cha Dkt. Faustine Ndugulile limeniumiza sana, shida ni nini?

Mke wa Faustine ambae ni Program Manager pale NBTS, Magdalena Swai nilifanya nae kazi kwa karibu akiwa kama Program manager NBTS na dada yangu mkubwa huku mm nikiwa Junior pale Ocean Road Cancer Institute na kabla sijakimbilia Ottawa, Canada na kuachana na Utumishi wa Umma.

Faustine kuwa DG-WHO Africa, ni fursa na Watz wengi wangeingia huko , ila jamaa amelala kabla hata ya kukalia kiti cha enzi . kuna thin layer kati ya mafanikio ya ndoto yako na mstari wa kuzimu, a very thin layer. Carefully !

Cha kusikitisha kabisa ni haijulikani Faustine ameanza kuumwa lini na ameumwa nini. Ukiwa kiongozi na nyie viongozi tabia ya kufanya siri ugonjwa wenu hata mnapoumwa kikawaida muwe sana makini, wakati mwingine watu wanatembea humo humo, ukishakuwa kiongozi na public figure vitu kama magonjwa sio siri, ijulikane unaumwa nini.

Faustine ameenda India no one knows , tunakuja kupewa taarifa za Maiti, Mafuru kaenda India, tunakuja kupewa taarifa za maiti.

Moja ya sehemu ambazo sitamani kusikia kiongozi wenye maono ameenda kwa matibabu ni India na SA, these places ni very corrupt na system govt za nchi nyingi ikiwemo Tanzania. Kama kweli wewe ni mtu potential and public figure , those are not places to go . Bora uende hapo MNH.

Magufuli amepekekwa Hospitali , mkafanya siri, tunakuja kupewa info za maiti, yaani haijulikani mnauliwa au mnakufa. Mbona wenzetu nje kiongozi akiumwa inajulikana na inajulikana ameenda wapi, hata JK alipoumwa tupo tulioenda pale Hopkins kumcheki! This is how a leader should be , sio unafanya fanya siri then wanakuua huko unaletwa maiti na kuwekwa upande wa mizigo wa ndege.

wanajua wazi watz wamezoea tu kupewa taarifa za msiba. Hii ni mbaya sana you guys need to change. Kuna viongozi wengi sna ni wagonjwa na tumewapa nafasi kubwa za uongozi na mpo na watu wanatamani hizo nafasi au ni maadu but mnafanya siri hali zenu mnawasafirisha kwa siri then mnakuja kutupa taarifa za msiba !

Kama mnawakatishana uhai je?

Post ya Faustine ilikuwa na upinzani mkubwa sna, na fitna tulizozifanya kama taifa zinajulikana…….na kwa umoja wa taifa akashinda, lakini mapambano hayaishi hapo, kuna some people loses the battle but not war …… tulipaswa kuendelea kumlinda Faustine ….. worst enough na kwa usiri wa hovyo mkaja kumpeleka India, a very corrupt places kwenye system za govt nyingi.

Moja ya benefits alizokuwa anakwenda kupata ni salary not less than 130M on monthly , international health insurance, watoto wote wanasomeshwa majuu, wife analipwa 60% of the salary yake, anapewa nafasi 14 kila mwaka za kuajiri from his country, lots of benefits with the country recognition , it was not just a post for him , it was a post for the country.

Kuna kitu hakipo sawa kwenye hilo taifa!

Poleni watanzania, tumenyang’anywa tonge mdomoni.

PIA SOMA
- TANZIA - Dkt. Faustine Ndugulile aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni afariki Dunia
Mke wa Faustine haitwi Magdalena Swai na hayupo nbts
 
Kwa sababu viongozi wetu wanajua hospitali zetu ni za walala hoi na hazina huduma nzuri,Hivyo huenda India ambako viongozi wa huko India wanajua namna ya kutumia Kodi za wananchi wao kuboresha huduma za kijamii kama hospital za umma.
India haijawahi kuwa kwenye orodha ya nchi zenye public healthcare system ya maana duniani
 
Nioneshe huyo Tajiri.?

All in all hujaelewa mada.utabibu sio madaktari, utabibu ni vifaa. Hata dawa unazoandikiwa hazitoki kwenye vichwa vyetu, zinatoka kwenye guideline na miongozo ambayo imeshaweka…. Akiumwa malaria mpe hiki, akiwa na infection mpe hicho….. ndio mana hata wasiosomea udaktari akipewa train anaweza ku practice. Unaponiambia madaktari wanatoka india na kwenda USA na wanafanya vema…….. unakuwa na notion kuwa udaktari ni watu

Now days tunatumia robotucs and automation with machine learning and artificial intelligence kutibu. Tunahitaji limited number of human resources.

Hata ukimchukua Dr wa Tanzania, akienda USA akafanya registration, atafanya vema kwa sababu hatotibu from his head bali from miongozo na resources zinazokuwepo ambazo ni advanced

Je umenielewa ? Au unahitaji kueleweshwa zaid ?
Hakuna unachofahamu, naona unaunga unga maneno tu, bora ukae kimya.
 
Kuna kitu hakipo sawa kwenye hilo taifa!
There's no doubt about this,...But; pamoja na kukubaliana nawe katika mambo mengi uliyo andika, kuna mengi pia ambayo umejisemea tu, bila ya kuyapa tafakari ya kutosha.

Kwa mfano: umejiuliza na waTanzania wangapi walio kwenda India; wakatibiwa vizuri tu na kurudi nyumbani Tanzania?
Ni kama nakumbuka kuwa hata Mwandosya ni mmoja wa hao.
Tanzania bado hatuna uwezo wa kuwapeleka wagonjwa wetu huko John Hopkin; kama ilivyo kuwa kwa Kikwete. Maswala ya 'corruption' kama unavyo yazungumzia, nadhani umefanya 'generalization' tu; na wala huna ushahidi wa kutosha kuwa hizi hospitali maalum zilizopo India kwa kutibu wagonjwa toka nje, ni 'corrupt', na ndiyo iwe sababu ya viongozi hawa kuto pata huduma nzuri iliyo pelekea kupoteza maisha yao.
Kwanza umeeleza mwenyewe, kwamba hata magonjwa yaliyo sababisha vifo hivi huyajui. Siyo kila ugonjwa unatibika, hata huko Johns Hopkins, watu wana kufa..

Hata hivyo, inanipa shida kuelewa hasa andiko lako lilitaka kutoa ujumbe gani hasa maalum, maanake limechanganya mambo mengi bila ya mwelekeo maalum.

Hongera zako za kuwa 'mwana-diaspora'. Usikose kuwa unafika mara kwa mara kututembelea sisi tulioko huku tukipambana sasa na haya maswala ya CCM na utekaji wanao tufanyia. Nadhani wanataka tuwe waoga zaidi na zaidi, ili siri zao, pamoja na hizo za magonjwa tuogope kuzi zungumzia kati yetu.
 
What's so special na Hospital za India??????.
Kila anayekwenda huko anakata moto!!!
UK, USA, NA Europe hakuna hospital za kisasa???
'Medical Tourism', hata watu wa mataifa hayo uliyo yataja wapo wanao kwenda kutibiwa India na Thailand na kwingineko.

Kuna maswala mengi katika jambo la matibabu; yaliyo muhimu zaidi ni huduma inayo patikana na unafuu wa huduma hiyo.

Hizi hospitali wanako kwenda hawa watu, huduma zake hazina tofauti na hizo za huko uliko kutaja; tofauti yake ipo kwenye gharama za huduma hizo.
 
Viongozi hawa nao. Wanaiba. Wanalipana mahela mengi na marupurupu kibao. Wanakula vinono. Ni kutoka kiyoyozi home mpaka kiyoyozi cha kwenye vi eite. Mazoezi hata yale ya kutembea tu hakuna. Wengi wana BP, high cholesterol na ni pre-diabetic. Insulin resistance imeshaanza. Lakini wao wanatanua tu kwa nyama choma na vinywaji vya kila aina.

Na wengi wao ukiwaona sura zao hazina nuru. Likely wamo kwenye gridi ya taifa na wanaishi kwa kula njugu mawe. Na ubaya wa njugu mawe ni kwamba siku likibumburuka linabumburuka kweli maana inafika mahali viungo vinachoka. Na culprit mkubwa ni figo, ini na hata moyo.

Mbali na sarakasi za hata kuondoana wao wenyewe kwa wenyewe kimya kimya lakini wengi wao wanaishi maisha ya hatari sana maana kwa mwanaume ukivuka 50 inabidi uwaangalie sana maadui hawa watatu - cholesterol, Hypertension na diabetes. Na ikibidi ubadilishe kabisa mtindo wa maisha...

Anyway. Safari yetu wanadamu hapa duniani ni fupi; na kila mtu ni kwa zamu yake. Apumzike salama daktari huyu msomi. Kama taifa tumepoteza mtu wa muhimu sana kabla hata hajashika nafasi yake ambayo ingemtambulisha yeye na nchi yetu. Na jana Yanga walipigwa magoli mawili. Na leo Simba wanacheza. Ndiyo mjadala wa kitaifa. Mengine yote hayana maana. Hili nalo litapita. Na maisha yataendelea tu.

Maisha!

Hata sijui yana maana gani!

Fumbo tata ajabu!
Maisha hayana maana cc kezilahabi
 
India iko overrated sana na Watanzania
Inategemea una zungumzia jambo gani.
Ni muhimu kutofautisha huduma zinazo tolewa katika "hospitali hizo maalum", na huduma zinazo patikana nje ya hizo hospitali maalum.

Kwa mfano: Huwezi kutoa tofauti kati ya "bomu la nuclear", lililo undwa India na mabomu ya 'nuclear' yaliyopo katika nchi zingine. Inawezekana hata mfano huu ukakuwia vigumu kutambua kinacho husika hapa.
 
Inategemea una zungumzia jambo gani.
Ni muhimu kutofautisha huduma zinazo tolewa katika "hospitali hizo maalum", na huduma zinazo patikana nje ya hizo hospitali maalum.

Kwa mfano: Huwezi kutoa tofauti kati ya "bomu la nuclear", lililo undwa India na mabomu ya 'nuclear' yaliyopo katika nchi zingine. Inawezekana hata mfano huu ukakuwia vigumu kutambua kinacho husika hapa.
India ni takataka
 
Maisha hayana maana cc kezilahabi
Ni kitabu gani cha Kezilahabi unakipenda kuliko vyote; na kwa nini?

Ndiyo. Kezilahabi alikuwa mfuasi mahiri wa tapo la falsafa la Existentialism. Katika tapo hili maisha hutazamwa kwa hatihati sana, nafasi ya binadamu katika mtazamo mpana wa kimalimwengu hudogoshwa na dini huonwa kama bandeji tu isiyo na faida katika donda ndugu lisilotibika. Maisha, katika upana wake, hudarubinishwa sana na kuonekana kama mchezo fulani wa watoto usio na maana pengine tu kuleta burudani hafifu isiyo na ridhiko na ya muda mfupi tu.

Kuanzia kwenye kazi zake akiwa angali kijana (Rosa Mistika), kwenye diwani zake kadhaa (Kichomi na Karibu Ndani) na hata kazi zake komavu za kifalsafa (Nagona na Mzingile) maisha yanaonwa kama mchezo fulani hivi mfupi sana, usio na kanuni wala mshindi.

Ila kwa vile, kama asemavyo Dk. Dyaboli, mbegu za baba zetu zilikuwa na kiherehere cha kulishinda lile shindano kubwa kuliko yote kule kwenye fallopian tubes za mama zetu tukajikuta tunazaliwa tena bila ridhaa zetu, basi inabidi tu tuyaishi haya maisha na kupambana nayo - hata kama ni magumu na yasiyokuwa na maana kiasi gani 💪💪

Maisha na kifo!

Kifo na maisha!

Rosa Mistika - Ua waridi lenye fumbo! 🙏🏿
 
Back
Top Bottom