Hili la Diwani mpya wa TLP Arusha laweza kuanzisha tena ghasia kubwa

Nashukuru kuwa sina mapenzi na chama chochote maana ukiwa na mahaba unaweza ukajikuta unafikiri kutokea moyoni badala ya ubongo na matokeo yake kuishia kuwa na images nyiingi kichwani zisizo na uhalisia.

Tumia kichwa chako vizuri sio upenzi (mOYO) wa ccm mifano matumizi ya maneno "Nashukuru kuwa sina mapenzi na chama chochote maana ukiwa na mahaba unaweza ukajikuta unafikiri kutokea moyoni badala ya ubongo na matokeo yake kuishia kuwa na images nyiingi kichwani zisizo na uhalisia" MBONA NDIVYO UNAVYOFANYA? Halafu ni uchochezi washauri ccm siyo chadema
 
My Take: (kwenye red): Habari zilizozagaa Arusha zinasema kuna mkono wa CCM katika njama hizo…. kwamba endapo itaamuliwa uchaguzi wa Meya utarudiwa, basi CCM iwe imejijengea mazingira mazuri kushinda. Inavyoelekea CCM wakishirikiana na watu wao (NEC) wako tayari tena kuona ghasia zinaanza upya Arusha.


Hayo majina ya viti maalum yanapelekwa NEC kabla ya siku ya uchaguzi. Sasa hapa CCM wanahusika vipi?

Kama amehama mwezi wa 11 ina maana hiyo ni wakati jina lake tayari limeshapelekwa huko NEC.

Wao waijulishe NEC kwamba huyo mama sio mwanachama wao tena na NEC wanatakiwa kuteua mtu mwingine.

Pia majina ya madiwani hayapelekwi na chama ngazi ya taifa bali ngazi ya wilaya na mkoa na hivyo TLP wawalaumu viongozi wao kwenye ngazi ya mkoa.

Lakini kama huyo mama sio wao tena mbona kuna taratibu za kurekebisha hilo? mambo mengine tunayakuza wakati taratibu zake zipo.
 
Hizi mbinu mbofu mbofu za huyu nyoka mzee(ccm) asiejibambua, za kuchakachua kila kitu zitaipeleka nchi kwenye machafuko.
.
 
Hivi baada ya Chadema kushindwa kufanikisha maandamano waliyoyaanzisha na kuamua kunyosha mikono juu bado kuna watu mna ndoto za kurudiwa kwa uchaguzi wa Meya wa Arusha?

HAKUNA ALIYE SURRENDER ni kwamba wananchi wansubiri tu kupewa GO AHEAD WAANZE MAANDAMANO WE USIFIKIRI VIBOMU VYA FFU VINAMTISHA YEYOTE. KAMA UNABISHA BASI HUDHURIA MAHAKMANI SIKU ZA KESI ZA AKINA MBOWE UONE
 
Butola sielewi kwa nini unashindwa kusoma alama za nyakati,swala la uchaguzi kurudiwa si la ccm au serikali kukubali ni swala la kufa na kupona,na chadema wamelifanya kuwa ajenda ya kitaifa,subiri bunge liishe uone maandamano nchi nzima,na ikifika hapo ujue si tu meya atakimbia bali hata Jk anaweza kimbia,kimsingi hali si shwari na cdm wanajipanga kimkakati
time will determine my words
 
Butola sielewi kwa nini unashindwa kusoma alama za nyakati,swala la uchaguzi kurudiwa si la ccm au serikali kukubali ni swala la kufa na kupona,na chadema wamelifanya kuwa ajenda ya kitaifa,subiri bunge liishe uone maandamano nchi nzima,na ikifika hapo ujue si tu meya atakimbia bali hata Jk anaweza kimbia,kimsingi hali si shwari na cdm wanajipanga kimkakati
time will determine my words

Ebu soma tamko la kamati kuu ya chadema ..................................................................................

2. Mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi Jijini Arusha

Kamati Kuu imepokea kwa masikitiko taarifa ya vifo vya wananchi watatu wasio na hatia kwa kupigwa Risasi na askari wa Jeshi la Polisi kufuatia vurugu zilizosababishwa na Jeshi hilo katika harakati zao za kuzuia maandamano halali na yenye Baraka zote za Kamanda wa Jeshi la Polisi Wilayani Arusha. Aidha, Kamati Kuu imesikitishwa na uvurugwaji wa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha kulikofanywa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa maelekezo ya Chama cha Mapinduzi na Serikali yake. Katika maazimio yake:

  1. Kamati Kuu imewapa pole ndugu wa wafiwa wa vurugu za Arusha pamoja na wananchi wa Arusha na watanzania kwa ujumla
  2. Kamati Kuu imewapongeza Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Mhe Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Willibrod Peter Slaa, Mbunge wa Arusha Mjini Mhe Godbless Lema na viongozi wengine wa CHADEMA kwa juhudi zao kubwa za kuepusha shari na kutoa uongozi wa kisiasa pale ambapo wananchi wa Arusha walitelekezwa na viongozi wa Serikali ya CCM katika kipindi chote cha matatizo ya Arusha
  3. Kamati Kuu imeiagiza sekretariati ya CHADEMA kuendelea na harakati za kudai haki za wananchi wa Jiji la Arusha kwa njia za kisiasa.
  4. Kamati Kuu imewaagiza madiwani wa CHADEMA katika Halmashauri ya Jiji la Arusha kuendelea kuingia katika vikao vya Baraza la Halmahauri hiyo na kuwawakilisha wananchi waliowachagua kikamilifu na wahakikishe kuwa wanatumia nafasi yao kufanikisha uchaguzi wa Meya.
Ukiangalia vizuri taarifa hii ya Kamati kuu utaona jinsi isivyo na continuity na tamko la Chadema lililotolewa kwenye mazishi ya walikufa kwenye maandamano...................................................

Tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Juu ya Mauaji ya Wananchi
wakati wa Maandamano ya Amani yaliyofanyika Arusha tarehe 5 Jan, 2011




Ili tutimize majukumu yote haya, tunahitaji kuhakikisha kwamba mambo yafuatayo yanafanyika:
  1. Serikali hii iwajibike kwa wananchi kama ilivyotamkwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Waziri wa Mambo ya Nchi Shamsa Vuai Nahodha na Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema wajiuzulu mara moja ili kuwawajibisha kama viongozi na wasimamizi wa juu kabisa wa Jeshi la Polisi la Tanzania. Aidha, kujiuzulu kwao kutapisha uchunguzi huru na wa kina wa matukio yote yaliyosababisha wananchi wetu kuuawa, mamia kujeruhiwa na mamia mengine kukamatwa bila sababu yoyote na kuwekwa rumande na baadaye kufunguliwa mashtaka ya uongo ya jinai;
  2. Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Andengenye na wale wote walioamuru au kutekeleza amri ya kuvunja maandamano na mkutano halali wafunguliwe mashtaka ya jinai kwa matumizi mabaya ya madaraka na kwa kusababisha mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia;
  3. Fidia stahili ilipwe kwa mujibu wa sheria husika za nchi kwa ndugu na/au jamaa wa wale wote waliouawa kutokana na vitendo vya Jeshi la Polisi la Tanzania na kwa wale wote walioumizwa kwa namna yoyote ile na/au kuharibiwa mali zao kutokana na vitendo hivyo;
  4. Mashtaka ya uongo ya jinai yaliyofunguliwa dhidi ya viongozi wa ngazi zote wa CHADEMA, wanachama, wafuasi na wananchi wengine wote waliokumbwa na kumba kumba ya Jeshi la Polisi la Tanzania yafutwe bila masharti yoyote kwa sababu maandamano na mkutano wa hadhara uliozuiliwa yalikuwa halali kwa mujibu wa sheria husika za nchi yetu. Tunasisitiza katika jambo hili kwamba viongozi, wanachama na wafuasi wetu wote waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka haya hawatahudhuria mahakamani tena kuhusiana kesi iliyofunguliwa dhidi yao hata kama kwa kufanya hivyo kutafanya wakamatwe na kurudishwa tena gerezani;
  5. Kwa vile uchaguzi wa viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ndio chanzo cha mauaji ya wananchi na kwa kufahamu utaratibu haramu uliotumika kumpata Meya wa Jiji hilo, matokeo ya uchaguzi huo yafutiliwe mbali na uchaguzi mpya uitishwe haraka iwezekanavyo kwa kufuata sheria husika za nchi yetu;
  6. Haki ya vyama vya siasa na wananchi kufanya maandamano ya amani kama inavyotambuliwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iheshimiwe na kutiliwa nguvu zaidi kwa kufuta vifungu vya Sheria ya Jeshi la Polisi nay a Vyama vya Siasa vinavyoruhusu Jeshi la Polisi la Tanzania kuzuia na/au kusitisha maandamano ya amani. Badala yake, sheria ziweke wazi wajibu wa Jeshi la Polisi la Tanzania kulinda maandamano ya amani na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na/au ya wananchi;
  7. Tume huru ya uchunguzi ya kimahakama (Judicial Commission of Inquiry) itakayoundwa na majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania iundwe ili kufanya uchunguzi huru, wa kina na wa wazi wa matukio yote yaliyopelekea Inspekta Jenerali wa Polisi na/au Jeshi la Polisi la Tanzania kupiga marufuku maandamano ya amani na mkutano wa hadhara na baadaye Jeshi la Polisi la Tanzania kufanya vurugu zilizosababisha mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia. Tunapenda kusisitiza kuundwa kwa tume huru ya kimahakama kwa sababu historia ya tume nyingine ambazo zimeundwa kwa utaratibu wa Rais kuteua watu anaowataka inaonyesha kwamba zimefanya kazi zao za uchunguzi mafichoni bila kushirikisha wadau wengine na bila wananchi kufahamu kitu kinachoendelea. Matokeo ya tume nyingi za namna hiyo ni kwamba ripoti zake mara nyingi zimepuuzwa na/au kufichwa na watawala. Tume ya uchunguzi ya kimahakama hufanya kazi zake kwa uwazi na huruhusu wananchi kuhudhuria na/au kushiriki moja kwa moja katika kazi za tume kama mashahidi na/au kwa kuhoji mashahidi wengine wanaotoa taarifa kwenye tume hiyo;
Hii inaonyesha Chadema wamenyosha mikono juu na na kuachana na misimamo yao ya awali, na hii inaturudisha kwenye jambo moja la msingi "Walikurupuka bila ya kuwa na strategy ya kufanikisha lengo lao".




Na sasa wame-divert attention ya maandamano kwenye jambo lingine kabisa ili kuwasahaulisha Wadanganyika...............

3. Matatizo ya Nishati ya Umeme na Gesi na Malipo kwa Kampuni Hewa ya Dowans

Kamati Kuu imeiagiza Secretariat yake kuanza maandalizi ya maandamano ya nchi nzima ya kupinga ongezeko la bei ya umeme, gesi na kuilipa Dowans. Na tarehe 24/02/2011 itakuwa siku ya kuanza maandamano kwenye Jiji la Mwanza na miji mingine kadiri ratiba itakavyotolewa.


.....Na nyie bado mnasubiri maandamano ya kurudiwa kwa uchaguzi wa Meya wa Arusha?
 
Hivi baada ya Chadema kushindwa kufanikisha maandamano waliyoyaanzisha na kuamua kunyosha mikono juu bado kuna watu mna ndoto za kurudiwa kwa uchaguzi wa Meya wa Arusha?

...Kwa akili za kawaida, Arusha ina Meya au kuna mtu anaitwa Meya wa Arusha?
 
Hizi mbinu mbofu mbofu za huyu nyoka mzee(ccm) asiejibambua, za kuchakachua kila kitu zitaipeleka nchi kwenye machafuko.
.

Mi naona kuna shida kubwa sana kwenye upinzani. Wapinzani wa kweli ni wachache sana wengi ni mapandikizi. We need to be careful here
 
Back
Top Bottom