Hili la Diwani mpya wa TLP Arusha laweza kuanzisha tena ghasia kubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili la Diwani mpya wa TLP Arusha laweza kuanzisha tena ghasia kubwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Feb 6, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  TLP wapinga NEC kuwateuliwa diwani

  Sakata la umeya wa Manispaa ya Arusha inazidi kuchukua sura mpya baada ya Chama cha Tanzania Labour (TLP) kupinga uamuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kupitisha uteuzi wa Mwaija Choga kuwa Diwani Viti Maalum kupitia chama hicho mkoani Arusha, kikidai kuwa si mwanachama wake halali.

  Hatua hiyo imefuatia baada ya uongozi wa chama hicho mkoani hapa ukiujulisha uteuzi huo na kuagiza kumuarifu diwani huyo taratibu za kuapishwa kabla ya kuanza kutekeleza majukumu.

  “Napenda kukutaarifu kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemteua Mwaija Choga kuwa Diwaninwa Viti Maalum katika Halmashauri ya manispaa ya Arusha, kwa barua ya Mkurugenzi wa Uchaguzi Kumb Na. EA.47/74/01/26 ya January 27, 2011” inaeleza sehemu ya barua ya kutoka kwa mkurugenzi wa Halamashauri ambayo Mwananchi Jumapili imeiona……..

  ………..Mwenyekiti wa TLP mkoani Arusha, Leonard makanzo, alisema jana kuwa TLP imepinga kwa nguvu zote uteuzi huo kwa maelezo Choga si mwanachama wa chama hicho, kuanzia Novemba 16, 2010.

  “Choga hawezi kutambuliwa kama Diwani wa Viti Maalum kupitia chama hicho cha na hastahili kutambuliwa kuwa diwani na asihudhurie vikao vyovyote vya baraza la madiwani vya halmashauri hiyo kwa tiketi ya TLP,” alisema Makanzo….

  Naye Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema uteuzi wa diwani huyo haukufuata taratibu na kwamba jina la Chogga halikuwa pendekezo la Kamati Kuu ya TLP Taifa. Mrema alisema maofisa watatu ndani ya chama hicho wakishirikiana na Chogga walifanya njama kuhujumu jina halali la mgombea lililopelekwa NEC…….


  Habari zaidi katika Mwananchi Jumapili.

  My Take: (kwenye red): Habari zilizozagaa Arusha zinasema kuna mkono wa CCM katika njama hizo…. kwamba endapo itaamuliwa uchaguzi wa Meya utarudiwa, basi CCM iwe imejijengea mazingira mazuri kushinda. Inavyoelekea CCM wakishirikiana na watu wao (NEC) wako tayari tena kuona ghasia zinaanza upya Arusha.
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kazi ipo!
   
 3. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  i am tired with these f...en business!!! tumechoka faulo zisizokuwa na kichwa wala mguu!! wao TLP walipeleka (ma)jina gani? watueleze!!! in short inatia kinyaa!!! hivi hadi leo,miezi kadhaa baada ya uchaguzi bado kuna biashara ya kuteuwana udiwani?
   
 4. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ccm wameishiwa,dalili za mfa maji
   
 5. Wakumwitu

  Wakumwitu JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  TLP wekeni wazi majina matatu mliyopeleka NEC ni yapi na kwa barua ipi ya kutoka TLP makao makuu/. Ili tujue ni nai mbaya wa maendeleo ya njii hii.
   
 6. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hasira ya Mungu sasa inahitajika ishuke juu ya huu ubabaishaji, tujue ni nani zaidi kati ya Mungu anayeishi milelel na huyu mungu tumbo ambaye watu wengine wameamua kumtumkia kwa nguvu zao zote. Kiu ya mioyo yetu ni kuona haki inatendeka kwani uinua taifa, sasa huu ubabaishaji unatoka wapi na kwa faida ya nani? Mungu pigana watu wakajue kuwa upo kwa ajili ya utukufu wako.
   
 7. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145


  Hivi baada ya Chadema kushindwa kufanikisha maandamano waliyoyaanzisha na kuamua kunyosha mikono juu bado kuna watu mna ndoto za kurudiwa kwa uchaguzi wa Meya wa Arusha?
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ninalo gazeti hilo na ninanukuu ibara nyingine ambazo mtoa mada hakuziweka:

  "(Mrema) Alifafanua kuwa kikao cha kamati kuu ya TLP taifa kilichokaa mwishoni mwa mwaka jana mkoani Kilimanjaro kilipendekeza jina la Mwamvua Wahanza.

  "Ni kweli Arusha kuna mgogoro kuhusu Choga, lakini jina lililopelekwa Tume si la Choga ni la Mwamvua Wahanza, lakini kuna maofisa watatu walishirikiana na Choga wakatengeneza na kuzipeleka tume kuhujumu uamuzi wa kamati kuu,' alisema Mrema."
   
 9. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,866
  Likes Received: 11,982
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo NEC inataka kutupeleka wapi tena inalazimisha watu uanachama.
   
 10. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,866
  Likes Received: 11,982
  Trophy Points: 280
  Kama huongelei upenzi nitakukumbusha post yako hii baadae.
   
 11. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #11
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  duuuu hapo napo ni maji marefu
  kama vipi jina la mwamvua lirudishwe na kuteuliwa kama mbunge wa viti maalumu,wasilazimishe mambo jamani.

  msema ukwelii hapendwiiii daimaaaaaa:clap2:
   
 12. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sikubaliani nawe....CCM wanaweza kulazimika kurudia uchaguzi huo. Lakini watakubali urudiwe tu pale ambapo wanajihakikikishia ushindi, si vinginevyo. Na hilli ni maandalizi.

  Kwanza jiulize tu: Katika mazingira ya halali na ya kawaida yaliyokuwapo kutokana na matokeo ua uchaguzi mkuu wa Oct 31, 2010, na kabla ya uchaguzi wa Meya, CCM haikuwa katika hali ya kushinda umeya moja kwa
  moja. Waliona kwanza lazima watunishe misuli -- na ndivyo walivyofanya na ushindi ukapatikana kwa njia zisizokuwa smooth -- zilikuwa za kiujanja ujanja tu na maguvu.
   
 13. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #13
  Feb 6, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Napendekeza kwa Mbowe ampe Mrema uwaziri kivuli mmoja katika Baraza lake la Mawaziri Kivuli.
   
 14. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #14
  Feb 6, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Butola acha ushamba cdm hawajashindwa na hawatashindwa,chadema hawajaanzisha vita ya umeya bali vita kati ya hakina dhuluma,ukweli dhidi ya uwongo,na chadema wamebadilisha mkakati kuhusu swala la arusha,na hawatalala hadi kieleweke,na wametoa mwongozo wao kwa madiwani,
  kwa kuwa lazima uchaguzi arusha urudiwe ccm kupitia nec wameanzisha vita na hujuma kwa tlp maana huyu Choga ni mamluki,na ni mmoja wa madiwani wanaopaswa kufungwa jela kwa ubadhirifu mkubwa wakati wa udiwani wake.
  Ni swala la muda
   
 15. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #15
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hizo ni wishful thinking!!

  Chadema imetoa tamko rasmi juu ya maandamano yale na serikali na CCM hawajatekeleza ata jambo moja, serikali imetangaza uchaguzi ule ni halali na haurudiwi, Kamati Kuu ya CCM imetangaza uchaguzi ule ni halali na haurudiwi.

  Pamoja na Chadema kusikia matamko ya serikali na CCM na kutotimizwa kwa masharti waliyoyatoa kwenye tamko lao wameishia kunywea tu na kuwaomba madiwani wake waudhurie vikao vya baraza la madiwani kama kawaida, sasa mnategemea serikali itaurudia uchaguzi bila shinikizo?

  May be chadema walikurupuka na kuanza kwa gia kubwa ya maandamano ambayo hawakujipanga wala kujiandaa namna ya kuyaendeleza hadi kufikia mafanikio, maana hauwezi ukaanza kwa maandamano alafu urudi mahakamani au kwenye baraza la madiwani ambako Meya mnayempinga ndie kiongozi, sikuzote ukianza maandamano endelea mpaka upate ulichokitaka vinginevyo umeshindwa.

  Nashukuru kuwa sina mapenzi na chama chochote maana ukiwa na mahaba unaweza ukajikuta unafikiri kutokea moyoni badala ya ubongo na matokeo yake kuishia kuwa na images nyiingi kichwani zisizo na uhalisia.
   
 16. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2011
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  swala la TLP mwachieni mrema, wala msiwafuatilie yule mtu wa system hivyo anajua kamchezo. cc tuchappe mwendo tu na CDM, mauza uza yote tuyaruke
   
 17. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #17
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Urudiwe kwa modality ipi mkuu??na kama kulikuwa na suluhisho kwa kutumia baraza la madiwani kwanini walitumia njia ya maandamano ambayo ilikuwa na risk ya kupoteza maisha ya watu?

  Kubali tu akilini mwako kuwa Chadema hawakujipanga na walikurupuka tu na maandamano wasiyoweza kuyaendeleza na kama kawaida ya siasa za kitanzania hawawezi kukiri hadharani kuwa wameshindwa na hivyo "kufunika kombe " kwa kinachoitwa mwongozo kwa madiwani usio na "timeframe" wala "mrejesho" kwa wananchi.
   
 18. Seto

  Seto JF-Expert Member

  #18
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 961
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hii too much sasa du! Huu utumbo mpaka lini?
   
 19. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #19
  Feb 6, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Unaumwa tafadhali muone daktari akupime akili
   
 20. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #20
  Feb 6, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Sick
   
Loading...