Hili kwenye mahusiano linakupa picha gani?

Ndechumia

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
1,103
418
Heshima zenu wana MMU,
Mi kuna jambo huwa linanipa shida sana, Hivi inapotokea unampigia simu mpenzi/mchumba/mume/mke au mtu yeyote ambae unamuheshimu ghafla katikati ya mazungumzo yenu unashangaa anakuwa anaongea na watu wengine wakati bado upo online, alaf anarud kuendelea na mazungumzo yenu.

Hii inatokea wakati mpo kwenye mazungumzo Mara ghafla unasikia anatoa maelezo au anamwagiza kitu fulan mtu mwingine alaf baadae ndo anarudi kwako kuendelea na mazungumzo.

Unashangaa tena baada ya dakika chache anakuacha tena na kuendelea na mazungumzo mengine kisha anarud, we utasikia tu eeh tuendelee.

Hii hali inapotokea mara kwa mara kwenye mazungumzo yenu inamaanisha nini?
mimi huwa natafsiri kuwa huyo mtu ananidharau ama ninachoongea nae kwake ni pumba.

wana jamvi hii mnaichukuliaje?
 
Hapo inategemea mnaongea mda gani, kwa sababu kama ndo mnaongea kwa masaa 10 its only logical akifanya hivyo kwa sababu hayupo outa space yuko duniani...Kama ni mazungumzo ya less than 2mins then una haki ya kudemand exclusivity ya mazungumzo yenu...
 
Inategemeana na mtu unaempigia kazungukwa na shughuli gani...!? na vilevile wewe unaepiga una mazungumzo ya aina gani? kama mazungumzo ambayo kila siku iendayo kwa mungu ni hayo hayo tuuu! (na hili lipo kwa watanzania wengi). wewe unategemea nini? labda akikukatia cm utaanza kulalamika kama ni mpenzi wako.
 
hapa umenipa jibu kamanda,tx
 
sasa mkuu hivi wakati anakuacha online akaanza mazungumzo mengine hajui kama unapoteza credit bure na kuwafaidisha Tigo? Ila hapa nimejifunza kitu,
 
Heshima zenu wana MMU,
Mi kuna jambo huwa linanipa shida sana, Hivi inapotokea unampigia simu mpenzi/mchumba/mume/mke au mtu yeyote ambae unamuheshimu ghafla katikati ya mazungumzo yenu unashangaa anakuwa anaongea na watu wengine wakati bado upo online, alaf anarud kuendelea na mazungumzo yenu.

Hii inatokea wakati mpo kwenye mazungumzo Mara ghafla unasikia anatoa maelezo au anamwagiza kitu fulan mtu mwingine alaf baadae ndo anarudi kwako kuendelea na mazungumzo.

Unashangaa tena baada ya dakika chache anakuacha tena na kuendelea na mazungumzo mengine kisha anarud, we utasikia tu eeh tuendelee.

Hii hali inapotokea mara kwa mara kwenye mazungumzo yenu inamaanisha nini?
mimi huwa natafsiri kuwa huyo mtu ananidharau ama ninachoongea nae kwake ni pumba.

wana jamvi hii mnaichukuliaje?

Kama unaongea na mtu kitu cha dharura hawezi kufanya hivyo. But kama ni stori za kawaida, hii huwa inatokea sana, hata mi huwa nafanya hivyo, na nafanyiwa hivyo. Simaindi wala sichukulii kudharauliwa...
 
Inategemea na maongezi yenu
Kama maongezi ni serious hawezi kufanya kitu kama hicho
Ila kama ni yale yale ya kila siku na ambayo hakuna jipya au ubunifu au ni muendelezo wa yale yale ya kila siku hapo hana ujanja
Ni lazima atakukatisha amuagize dada ampikie chai au afanye usafi au apike chakula
 
sasa mkuu hivi wakati anakuacha online akaanza mazungumzo mengine hajui kama unapoteza credit bure na kuwafaidisha Tigo? Ila hapa nimejifunza kitu,
Hapana mkuu.
Kwanza kama ushaongea nae kwa muda wa dakika kadhaa, maanake una credit za kutosha haswa! hauwezi kulalamikia dk moja alokuacha online ili aongee na mtu,
pili mara nyingi ili usimfikirie vibaya ni vizuri ukisikia anachokiongea upande wa pili.
Nadhani mpaka hapo utamwelewa mwenzio hana anachokificha upande wa pili zaidi ya kutaka kuwa free zaidi kwako....!
She loves you!

sasa mkuu hivi wakati anakuacha online akaanza mazungumzo mengine hajui kama unapoteza credit bure na kuwafaidisha Tigo? Ila hapa nimejifunza kitu,

Sawa pengine huyo yuko ofisini ama shghulizake ni Gerezani,au Kidongo Chekundu..

Sasa kuna ile umemtembelea mtu kwake ama kwao,mnapiga stori,anakatishakatisha mara amuite huyu,mara yule.. Mara amtume hiki,mara anyanyuke aweke kitu kingine sawa.. Yaani atafanya hivyo hata mara tano hadi sita!

Na kila wakati anaporudi,ni "enhe..","ikawaje sasa",na saa nyingine unataka umweleze ili kama analimudu hilo swala akupe jibu fasta,uondoke..lakini anakuharibia pozi hadi unatamani uage uende...

Nadhani ni tabia zao tu!
 
Yaani kama dkk tano zilizopita nilikuwa naongea na mtu ,..mara nasikia hao kuku pakia pitisha kwa mzee shoo mmh!
...
 
Inategemea na maongezi yenu
Kama maongezi ni serious hawezi kufanya kitu kama hicho
Ila kama ni yale yale ya kila siku na ambayo hakuna jipya au ubunifu au ni muendelezo wa yale yale ya kila siku hapo hana ujanja
Ni lazima atakukatisha amuagize dada ampikie chai au afanye usafi au apike chakula
Mkuu tena asikwambie mtu maongezi ya mtu na hawara yake katika cm hayana maana sana, hayako serious, alafu yanachukua zaidi ya saa nzima eti jirushe! sasa hapo unategemea nini kama hajakukatiza kila dakika.
Mara wewe ebu niletee ndoo maji yanamwagika!
au kama ndio yuko dukani "eeh hiyo pedi na hiyo krimu ya kokoa....!"
au kama anauza naniliu " eeh nikupimie na nini unataka mara hela haitoshi"
Tusiwalaumu tulaumu mazungumzo tunayoyafanya kwenye cm ni mengi na hayana maana sana.
 
mkuu nimependa comment zako sana, unaonekana una busara sana na subira. bigup
 
Mkuu tena asikwambie mtu maongezi ya mtu na hawara yake katika cm hayana maana sana, hayako serious, alafu yanachukua zaidi ya saa nzima eti jirushe! sasa hapo unategemea nini kama hajakukatiza kila dakika.
Mara wewe ebu niletee ndoo maji yanamwagika!
au kama ndio yuko dukani "eeh hiyo pedi na hiyo krimu ya kokoa....!"
au kama anauza naniliu " eeh nikupimie na nini unataka mara hela haitoshi"
Tusiwalaumu tulaumu mazungumzo tunayoyafanya kwenye cm ni mengi na hayana maana sana.

Yeah kabisa mkuu
Ukiwa na maongezi serious na mtu then akakupuuza akaanza kuongea na watu wengine pembeni kwenye simu hapo kweli unaweza kulaumu
Ila kama ni yale yale ya kawaida ambayo eti unamuuliza eeehh niambie sasa hivi unafafanya nini au jioni hii utakuwa wapi au sijui leo mchana ulikula nini aahhh hapo lalzima akuache unaongea au akugandishe kwenye simu aongee na mtu pembeni
Ila wewe kuwa serious na maongezi yenu utoaona atakavyokupa attention kukusikiliza
Siku unamwambia habari za kuongeza mtaji wake wa salon au genge lake au kumpangishia nyumba uone atakavyokuwa serious hata akiwa ana wateja pembeni hatawasikiliza
 
Mkuu umenchekesha sana hapa! ni kweli kabisa tena atakuwa yuko serious na hataki bughuza.

Back
Top Bottom