Hili janga litapita, lakini tuchukue hatua madhubuti

Dogo Lao

Member
Nov 2, 2011
94
38
Kwa sasa tunajua kuwa Dunia nzima tunapita katika mtihani mkubwa wa ugonjwa wa COVID_19. Kila nchi inahangaika kutafuta majibu ya changamoto hii.

Mashirika ya kiserikali na asasi za kiraia zinajitahidi katika kutoa maelekezo na kupendekeza mbinu mbali mbali za kujikinga. Nchini kwetu kama zilivyo nchi nyingine duniani tunajitahidi nasi kutafuta solutions, kufuata maelekezo na kutengeneza mikakati tunayodhani itatusaidia.

Kwa uhalisia, nionavyo mimi tunajitahidi kupambana LAKINI mikakati yetu inanipa mashaka. Mheshimiwa Rais anatupa mbinu hii "IMANI" tuitumie kama mkakati stahiki wa kudhibiti COVID_19. Ndiyo, ni IMANI.

Amesisitiza siyo mara moja, na ametuhakikishia kuwa "Kwa jina la Yesu tutaishinda Corona". Tusidharau, wala tusimpuuzie, inawezekana kweli imani yetu ikatuokoa. Swali langu ni hili: Mbinu ya kiimani ikiprove failure dunia itamwelewa kweli?

Mbinu hii ipo kikatiba au ni maono binafsi? Najaribu kujiuliza, watu wakizembea kuchukua tahadhali za kujikinga kwa sababu tu ya kuamini kuwa Mungu atawaponya, Watendaji wake wakazembea kutoa elimu na hamasa madhubuti katika kukabiliana na janga hili, idadi ya vifo na maambukizi ikawa kubwa na ya kutisha East Africa,

Je! Mheshimiwa Rais atauambia nini ulimwengu? Hao watakaosalia ambao watakuwa wamewapoteza ndugu na jamaa zao watamwelewa?

Mimi nafikiri, hata kama tunaishi kwa "IMANI", lakini mipango na mikakati madhubuti tena ya makusudi ichukuliwe kwa nguvu zote. Tunamfahamu Rais wetu ana kipawa kikubwa cha kusimamia jambo na likawa, hivyo ningetamani kuona hatua madhubuti za kitaalamu zinasimamiwa ili janga hili lisitumalize.

Tumeaminishwa kwa muda mrefu sasa kuwa tunazo fedha za kutosha. Tumeambiwa mara kadhaa kuwa sisi ni matajiri na uchumi unapanda ndio maana tunauwezo wa kununua ndege kwa fedha cash.

Haya ni mafanikio makubwa sana katika nchi, na kama tunauwezo wa kununua ndege kwa fesha cash it means tunayo akiba ya kutosha. Pia nafahamu ktk serikali yoyote kuna mfuko wa majanga, sasa kwanini tuhofie tutakufa njaa wakati fedha tunazo?

Siyaongei haya kukebehi juhudi za mheshimiwa Rais, lakini naongea haya nikiwa kama mnyonge ninayeamini juu ya utajiri tulionao. Imani itumike, maarifa yatumike na fedha itumike ikiwezekana serikali ije na mikakati ya kulinda raia wake wasife kwa njaa ktk kipindi hiki cha kupambana na covid_19.

"Imani pasipo matendo imekufa". Yakobo 2:26


#Epuka misongamano, epuka kushikana, nawa mikono kwa maji na sabuni mara kwa mara, mwombe Mungu.
 
Hayo mambo ya kusema Mungu atatusaidia ni ya kufikirika hayana uhalisia wowote,nakubaliana na wewe hapa zinatakiwa mbinu na mikakati ya kusayansi ili kushinda hii vita...

Tukiendelea kudanganya mungu atatusaidia tutapukutika kama kuku wa kideli wallah!
 
Back
Top Bottom