Hili jambo limenisikitisha sana

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
13,577
18,904
Hapa kwetu tuna jirani yetu anaitwa Victor ambaye ni mshikaji wangu sana. Victor ana mke anayempenda sana. Amemfungulia biashara lakini pia amemnunulia gari aina ya mark x.

Nikiwa nipo maeneo ya Sinza Kuna issue moja nashughulikia nikamuona mke wa Victor akiwa na jamaa fulani mimi binafsi simjui wanaingia gesti moja. Honestly sikuamini macho yangu nikajiuliza mbona huyu mwanamke anapewa kila kitu na Victor inakuaje anamfanyia huu upuuzi?

Lakini pia huyu dada amechangia percentage kubwa ya mafanikios ya Victor. Kipindi wapo kwenye uhusiano kabla ya ndoa kuna kipindi fulani Victor alikuwa hana kazi na mwanamke kwao kidogo kulikuwa na hela alikuwa anamuomba baba yake halafu akipewa hiyo hela anampa Victor na baadhi ya matumizi alikuwa anatoa yeye sababu pia alikuwa na kazi kabla hajasimamishwa.

So nikabidi nisimwambie mshikaji wangu Victor nionane na mke wake nijue tatizo ni nini? Kweli tukaonana na mkewe nikamwambia kuna mtu unatoka naye kimapenzi na niliwaona Sinza akakubali kweli amechepuka so nikamuuliza kwa nini unafanya upuuzi kama huu?

Kabla hajanijibu akaniuliza “umemwambia Victor?” Nikamjibu ukweli kuwa sijamwambia.

Akaanza kunieleza kuwa Victor hana uwezo wa kuzalisha mwanamke ingawa amemvumilia mpaka leo licha ya kumsingizia kwa familia yake kuwa ana tatizo la uzazi ndo maana anachelewa kubeba mtoto kutokana na pressure ya familia yake kutaka mtoto lakini mwenye tatizo ni Victor na yeye ikabidi amfichie aibu yake na asiwaambie ukweli familia yake.

Nikamuuliza “wewe ulijuaje Victor ana tatizo hilo la kutozalisha?” Akanijibu siku moja wakati yupo na Victor nyumbani baadaye Victor akatoka kwenda dukani na akaacha simu yake kwenye charger. Mara kidogo simu yake ikaita ikabidi aipokee.

Aliyepiga simu akaniuliza “wewe ni nani maana mimi nataka niongee na Victor” Akamjibu yeye ni mke wake na Victor ametoka kidogo atarudi muda si mrefu yule aliyepigia simu akauliza “ni kweli wewe ni mke wa Victor?”

Alipomjibu ndio akaomba no zake za simu akidai kuna jambo la muhimu anataka waongee kuhusu mume wake ikabidi ampe.


Walipofanikiwa kuonana na akaeleza yeye ni doctor binafsi wa Victor ndo akamwambia tatizo alilonalo Victor na pia akasema Victor hakumwambia kama ameoa.

So wakakubaliana awe anampa madawa ya kumponesha hata kama hayatamponesha amdanganye amepona ili hata akishika mimba ya mwanaume mwingine ionekane ya kwake.

Hayo ndo yakawa mwisho wa maelezo ya mke wa Victor kwangu. Mimi kiukweli nilichoka kuanzia kimwili hadi kiroho nikaona si budi hayo mambo yao niwaachie wenyewe wapambane na hali yao.

NB: Kupitia maisha ya Victor na mkewe nimejifunza kitu kwenye maisha yangu kiukwel duh! Kweli familia Zina Siri nzito.
 
Story ya kutunga! Hiyo coincidence ya kuona mke wa mtu anachepuka na njemba???? Huwa wanajificha. Alafu eti ujasiri wa kumuuliza mtu aliyechepuka alafu anakujibu kiulaini??? Alafu eti dakitari kapiga simu mke kapokea na kutoa siri za mgonjwa wake kwa mtu anayejiita mke?? Highest level of lie!
 
Story ya kutunga! Hiyo coincidence ya kuona mke wa mtu anachepuka na njemba???? Huwa wanajificha. Alafu eti ujasiri wa kumuuliza mtu aliyechepuka alafu anakujibu kiulaini??? Alafu eti dakitari kapiga simu mke kapokea na kutoa siri za mgonjwa wake kwa mtu anayejiita mke?? Highest level of lie!
Ahahahah.
Mzee naona umeshimdwa kuvunga baada ya kuona kama ambavyo wengi tumeona.
Anyway..tuwaachie wenyewe
 
Kwaiyo dr akamsnitch client wake au sio! Sasa alienda kumwelezea kimbea mbea kumuibia siri mke wa jamaa! Na wewe si ushamwambia victor maana victor naye yuko humu
 
Back
Top Bottom