Hili hapa chimbuko la Mkataba 'tata' wa Bandari, hawa wanacho cha kutueleza!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Nimeamua kuwadokeza watanzania jambo hili. Kujua chimbuko ni mwanzo wa kujua suluhisho la tatizo, kama lipo. Kwa ubobevu wangu kiutumishi serikalini na chamani, nimefuatilia na kujua chimbuko la mkataba huu 'tata' wa bandari kati ya Serikali yetu na ile ya UAE ikiwakilishwa na kampuni ya DP World.

Sakata la ukodishwaji wa Bandari lilianza mwaka 2016. Ni pale ambapo Serikali ya Hayati Magufuli ilipoona kuwa kuna haja ya kufanya mapitio ya mkataba wa uendeshaji wa Bandari yetu kati ya Serikali na Kampuni ya TICTS. Kampuni ya TICTS ilikuwa na mkataba mrefu wa kuendesha Bandari (hasa upande wa makontena).

Kamati Maalum ya kufanya mapitio hayo ya mkataba wa TICTS iliundwa. Kiongozi wake alikuwa Wakili Hamza Johari, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TCAA). Kazi ilianza mwaka 2016 na kukamilika mwaka 2017. Kati ya matokeo ya mapitio hayo, mkataba wa TICTS ulifanywa kuwa wa miaka mitano (2017-2022). Pia, TICTS waliwekewa malengo ya kuyafikia ili kuweza kupewa mkataba mwingine.

Mwaka 2022 ulipofika, TICTS ilionekana kutotimiza/kutoyafikia malengo ya kimkataba na hivyo ikaondolewa Bandarini. Mamlaka ya Bandari (TPA) ikachukua majukumu yote ya TICTS na kuiendesha Bandari rasmi kuanzia Januari mwaka huu. Lakini, katika kipindi chote cha TICTS na hata cha TPA, Serikali haikuwa ikiridhishwa na utendaji, manufaa na ustawi wa Bandari yetu.

Serikali ikajipanga kupata ufumbuzi. Ukatokea mwaliko wa kuhudhuria Maonesho ya Bidhaa na Huduma mbalimbali huko Dubai, Falme za Kiarabu mwaka 2022. Timu kubwa ya Serikali ikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ilihudhuria. Walikuwapo pia Mawaziri, Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali za kiserikali (zikiwamo TPA na TCAA). Huduma na Bidhaa zikaonwa.

Kutokana na Maonesho hayo ya Dubai, DP World akaonekana. Alionesha, zaidi, masuala ya huduma za kibandari kwenye nchi mbalimbali duniani. Serikali ikatamani kufanya kazi naye. Ikatamani (na si jambo baya) kuwa na huduma kama zilizooneshwa kwenye Maonesho hayo. Ikakata shauri kukaa mezani na DP World, kwa msaada wa Serikali yao, kuona nini cha kufanywa.

Timu ya Majadiliano ya Serikali iliundwa. Ikaongozwa tena na Wakili Msomi Hamza Johari. Timu hii iliundwa na Wajumbe ambao, kwa aslimia zaidi ya 90, walikuwa ni Wanasheria wabobevu katika nyanja ya majadiliano; biashara; uwekezaji na masuala ya Bandari. Majadiliano yakafanyika na Makubaliano pamoja na Mkataba baina ya Serikali zetu ni watoto wa majadiliano hayo.

Kiukweli, hakukuwahi kuwepo na kushindanisha makampuni ili kumpata DP World. Hakukuwahi kuwepo mchakato wa 'kimanunuzi' uliozoeleka wa kushindanisha. Ilitumika 'single source procurement'. Hadi hapo, iko wazi kuwa Maonesho ya Dubai ndiyo chimbuko la Makubaliano na Mkataba uliozua mjadala kila mahala. Na vyote vina baraka ya kiserikali.

Pamoja na nia njema ya kuboresha utendaji na ufanisi wa Bandari yetu, Makubaliano na Mkataba wa Bandari vimeleta sintofahamu kubwa. Vimekataliwa na wanachi kwa kusema na hata kwa kuguna. Bado wananchi wanatoa maoni yao. Waachwe wakosoe. Waachwe wakohoe. Waachwe waboreshe. Waachwe walie na kucheka hadi mabo yawe yanaeleweka.

Hadi hapa, wapo wa kutueleza juu ya hili. Nimewataja. Watuambie, wanayaonaje Makubaliano yaliyozalishwa na Majadiliano? Watuambie wanauonaje Mkataba uliotokana na majadiliano yao? Watuambie, itakuwaje mikataba ya utekelezaji itakayofuata baada ya msingi huu uliojengwa uliozua gumzo na mzozo?

Kosa lolote kwenye Bandari ni hatari!

Mzee Tupatupa wa Lumumba ( kwasasa Chato, Geita)
 
Hakuna mwananchi mwenye shida na uwekezaji , na hawa jamaa wamewekeza sehemu nyingi tuu duniani , tatizo kwetu ni mkataba tulioingia nao, ndo unaleta ukakasi , ndo mana watu wanataka marekebisho yafanyike. Hata Barrick ni wawekezaji wazur tuu tatizo ni mkataba tulioingia nao unalalia Kwa mwekezaji , na mwekezaji akiona kuna upenyo wa kukulipua lazima akunyooshe tu.
 
Kama hayo makubaliano ya Uwekezaji na Kimkataba yaliongozwa na Wanasheria wetu wabobezi kama ulivyosema basi Kuna haja hao Wanasheria Wachunguzwe Uraia wao.

Au wakati wanajadiliana kuhusu Muda wa Mkataba wenzetu walikuwa wanashikwa shikwa na wale mabinti wa Kiarabu hivyo kujikuta wanajibu Ndiyo Ndiyo..?

Maana hata Samason alipokuwa anaulizwa na Delila (Akiwa amemkalia kwa Juu) kuhusu zilipo nguvu zake akajikuta anasema tu kuwa zipo kwenye nywele zangu za kichwani

All in all hatupo tayari kuona huu mkataba unatekelezwa iwapo hakuna limitations ya Muda pamoja na kuruhusu TRA kukusanya kodi hapo
 
Nimeamua kuwadokeza watanzania jambo hili. Kujua chimbuko ni mwanzo wa kujua suluhisho la tatizo, kama lipo. Kwa ubobevu wangu kiutumishi serikalini na chamani, nimefuatilia na kujua chimbuko la mkataba huu 'tata' wa bandari kati ya Serikali yetu na ile ya UAE ikiwakilishwa na kampuni ya DP World.

Sakata la ukodishwaji wa Bandari lilianza mwaka 2016. Ni pale ambapo Serikali ya Hayati Magufuli ilipoona kuwa kuna haja ya kufanya mapitio ya mkataba wa uendeshaji wa Bandari yetu kati ya Serikali na Kampuni ya TICTS. Kampuni ya TICTS ilikuwa na mkataba mrefu wa kuendesha Bandari (hasa upande wa makontena).

Kamati Maalum ya kufanya mapitio hayo ya mkataba wa TICTS iliundwa. Kiongozi wake alikuwa Wakili Hamza Johari, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TCAA). Kazi ilianza mwaka 2016 na kukamilika mwaka 2017. Kati ya matokeo ya mapitio hayo, mkataba wa TICTS ulifanywa kuwa wa miaka mitano (2017-2022). Pia, TICTS waliwekewa malengo ya kuyafikia ili kuweza kupewa mkataba mwingine.

Mwaka 2022 ulipofika, TICTS ilionekana kutotimiza/kutoyafikia malengo ya kimkataba na hivyo ikaondolewa Bandarini. Mamlaka ya Bandari (TPA) ikachukua majukumu yote ya TICTS na kuiendesha Bandari rasmi kuanzia Januari mwaka huu. Lakini, katika kipindi chote cha TICTS na hata cha TPA, Serikali haikuwa ikiridhishwa na utendaji, manufaa na ustawi wa Bandari yetu.

Serikali ikajipanga kupata ufumbuzi. Ukatokea mwaliko wa kuhudhuria Maonesho ya Bidhaa na Huduma mbalimbali huko Dubai, Falme za Kiarabu mwaka 2022. Timu kubwa ya Serikali ikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ilihudhuria. Walikuwapo pia Mawaziri, Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali za kiserikali (zikiwamo TPA na TCAA). Huduma na Bidhaa zikaonwa.

Kutokana na Maonesho hayo ya Dubai, DP World akaonekana. Alionesha, zaidi, masuala ya huduma za kibandari kwenye nchi mbalimbali duniani. Serikali ikatamani kufanya kazi naye. Ikatamani (na si jambo baya) kuwa na huduma kama zilizooneshwa kwenye Maonesho hayo. Ikakata shauri kukaa mezani na DP World, kwa msaada wa Serikali yao, kuona nini cha kufanywa.

Timu ya Majadiliano ya Serikali iliundwa. Ikaongozwa tena na Wakili Msomi Hamza Johari. Timu hii iliundwa na Wajumbe ambao, kwa aslimia zaidi ya 90, walikuwa ni Wanasheria wabobevu katika nyanja ya majadiliano; biashara; uwekezaji na masuala ya Bandari. Majadiliano yakafanyika na Makubaliano pamoja na Mkataba baina ya Serikali zetu ni watoto wa majadiliano hayo.

Kiukweli, hakukuwahi kuwepo na kushindanisha makampuni ili kumpata DP World. Hakukuwahi kuwepo mchakato wa 'kimanunuzi' uliozoeleka wa kushindanisha. Ilitumika 'single source procurement'. Hadi hapo, iko wazi kuwa Maonesho ya Dubai ndiyo chimbuko la Makubaliano na Mkataba uliozua mjadala kila mahala. Na vyote vina baraka ya kiserikali.

Pamoja na nia njema ya kuboresha utendaji na ufanisi wa Bandari yetu, Makubaliano na Mkataba wa Bandari vimeleta sintofahamu kubwa. Vimekataliwa na wanachi kwa kusema na hata kwa kuguna. Bado wananchi wanatoa maoni yao. Waachwe wakosoe. Waachwe wakohoe. Waachwe waboreshe. Waachwe walie na kucheka hadi mabo yawe yanaeleweka.

Hadi hapa, wapo wa kutueleza juu ya hili. Nimewataja. Watuambie, wanayaonaje Makubaliano yaliyozalishwa na Majadiliano? Watuambie wanauonaje Mkataba uliotokana na majadiliano yao? Watuambie, itakuwaje mikataba ya utekelezaji itakayofuata baada ya msingi huu uliojengwa uliozua gumzo na mzozo?

Kosa lolote kwenye Bandari ni hatari!

Mzee Tupatupa wa Lumumba ( kwasasa Chato, Geita)
Vizuri sana!
 
Kama hayo makubaliano ya Uwekezaji na Kimkataba yaliongozwa na Wanasheria wetu wabobezi kama ulivyosema basi Kuna haja hao Wanasheria Wachunguzwe Uraia wao.

Au wakati wanajadiliana kuhusu Muda wa Mkataba wenzetu walikuwa wanashikwa shikwa na wale mabinti wa Kiarabu hivyo kujikuta wanajibu Ndiyo Ndiyo..?

Maana hata Samason alipokuwa anaulizwa na Delila (Akiwa amemkalia kwa Juu) kuhusu zilipo nguvu zake akajikuta anasema tu kuwa zipo kwenye nywele zangu za kichwani

All in all hatupo tayari kuona huu mkataba unatekelezwa iwapo hakuna limitations ya Muda pamoja na kuruhusu TRA kukusanya kodi hapo
Kuna uwezekano pia vipande vya fedha vilitumika kupunguza maarifa ya mawakili wetu wasomi..
 
DP wanapewa kuendesha Ports za kwenye Sea and Lakes yaani Bandari za kwenye bahari na maziwa yetu yote. Yaani kampuni moja!

Huu mkataba umekaa vibaya
Hiyo ni shida kubwa sana. Kampuni moja kupewa bandari zote bila ukomo ni hatari kwa hali na mali. Atachagua vipaumbele vyake kwa kuangalia biashara inavyoenda. Tutalia na kulia. Hakuna mkataba unaokaa hivyo duniani.
 
Back
Top Bottom