Hili gari BMW 7 limerogwa?

Hili gari BMW 7 limerogwa?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,579
Reaction score
161,432
Ndugu yangu ana gari aina ya BMW 7 series ambalo huwa analitumia kama chaguo lake la pili, chaguo lake la kwanza ni Mercedes Benz G Guard.

Juzi kati Noah yangu ilipata hitilafu hivyo nikawa naswampa na madaladala.

Ndugu yangu huyu kwa kunihurumia akasema niwe natumia BMW yake.

Aisee hii gari ina engine ya zaidi ya CC 2000 lakini ulaji wake wa mafuta ni mdogo kama wa Vitz yaani km 17 kwa litre.

Hili gari nimetokea kulipenda sana na sasa nadhani ni wakati muafaka kwa Watanzania kuachana na magari ya Kijapani yanayokula mafuta mengi bila sababu na kujiunga na magari ya Ulaya na India yasiyotumia mafuta mengi.
 
Ha haaaa, nyie mnalia na vigari vya CC 2500? Je sisi wenye ma Range Rover ya cc 4600 alafu engine ya Petrol tusemeje?
 
Inaweza kuwa inatumia mafuta kama Vits ila ikipeleka service unaacha 500,000/- au ukipasua taa 1.5m..si ushawahi kusikia BI-XENON head lamps?! Ukinunua gari inabidi uzingatie vigezo vingi sio kimoja tu kama mafuta.

Kuna gari fuel consumption ni nzuri lakini inapokuja swala la service na body parts ndio tabu inaanza.
 
Ndo maana watu wanakuwa wakali wanapoguswa au kukwangliwa? Binafsi kama gari inanipa utility na kuifurahia basi nitaihudumia kwa mapenzi ya dhati as long as hyo hela ya service inakuwa compasatef kwenye mafuta. Naoma picha yake mkuu.
 
Picha ya nini?
 
Kuna gari fuel consumption ni nzuri lakini inapokuja swala la service na body parts ndio tabu inaanza.

Discovery 3, Audi q7,vw touareg zote zipo za 3.0TDi, zinatumia wese vizuri sana! Ila maintance ndio balaa.
 
Back
Top Bottom