Mababu zenu walikuwa na hekima. Si busara hata kidogo kumsimulia mtoto mambo yanayotisha maana utaharibu ubongo wake.
Ujue tu uchawi upo maana hata katika biblia ( Rejea kitabu cha kutoka) wakati musa anawaondoa wana wa israeli kutoka utumwani Misri, kulikuwa na maonesho makubwa ya nguvu za giza wachawi wakishindana na Mungu kugeuza fimbo kuwa nyoka.
Ni busara kujielimisha walau kwa kupitia jf au tembelea maeneo husika.
Mimi siyo mchawi ila nimeishi na wachawi cocords kabisa. Ukifika sehemu, ujikalie kimya tu maana ukiongea kama hayo, utageuzwa Field farm, kila mchawi atataka kujaribu uchawi wake kwako kama utashika. Kama utakutana na wabembe, watajaribu kukugeuza fisi, mbwa ama kunguru ilimradi tu wakuone uwezo wako.
Enzi hizo walimu waliofika pwani ya ziwa Tanganyika, waliomba kubadilishiwa vituo mara moja maana walikuwa wanajikuta wamelala utupu bara barani asubuhi, ikawa mwisho wa viboko mashuleni kwa wageni na Mwanzo wa walimu au wafanya kazi kuukwepa mkoa wa Kigoma.
Kuna miti (mibuyu) mingi ilikiwa ikimeza watu na barabara nyingi zsizokuwa na mwisho zilikuwepo hapo kale ambazo habari zake zastaajabisha. Huwa nikiona mshana Jr akiandika naona kama anaufunua mkoa wa kigoma. Ikumbukwe tu na narudia tena, Mimi si mchawi.