Kuna padri mmoja enzi zile alikuwa anahubiri kigoma akasema kama wewe hivi " hakuna uchawi hapa wala mtoto wa uchawi, shijeni imani yenu nanyi mtakuwa salama" akarudi kukaa kule juu altareni,
alipotaka kunyanyuka tena, kiti kikawa kimenasa makalio, ilibidi asemee pale pale " nimeamini uchawi upo," kiti kikamuachia.
Lakini pia waulize wafuatao habari za uchawi wa kigoma.
Mwl Nyerere ( Ni kigoma pekee wakifanikiwa kumuibia fimbo yake pamoja na kuwa baba wa taifa)
Yusuph Makamba ( huyu alilazimisha wananchi kulima pamba katika kijiji cha ruhita, aliporudi kukagua, wakamuonesha pamba imestawi na kuchanua vizuri, akapiga picha akiwa katika mashamba makubwa ya pamba akarudi mkoani. Picha zilipotoka, akajikuta kumbe alipiga picha zote akiwa katika pori kubwa la kibhambila, mpaka leo kigoma hailimi pamba na makamba alihana ukuu wa mkoa akakimbilia dsm.
Mzindakaya. (Huyu alikuja kwenye vikao vya Tanu kule akwatukana wazee, wakaamua kutundika makoti hewani, kikao kiliishia hapo na mpaka leo usimuulize habar za ujiji.)
List ni ndefu, muulize
mshana jr