Hili Bunge letu hili la Tanzania ....

Ukitaka kuiona vyema, hebu ibovye picha yenyewe, nice weekend

Mkumbuke IBADA kesho jamani after that ni kwenye kitimoto, by the way someni gazeti la mwananchi la leo 25 june 2010 Dk. Makufuli anasema idadi ya wala kitu chetu wameongezeka...wat a good news?
 
Ila kwa kweli wanatia fora kwa kusinzia hii inadhihirisha kuwa kinachojadiliwa hakina maana wala faida kwao maana wanachojali wao ni masilah yao. Au hii ndio sababu akitokea mpinzani kwenye jimbo lake unasikia ka ugonvi kaanza. Yaani kama Bunge la Mwaka huu unaona kabisa Wabunge wengi wapo bungeni kama wajibu wa kufika, na posho lakini mawazo yao yako kwenye uchaguzi, naona kama miaka mingine haikuwa hivyo au kwa sababu sikua mfuatiliaji sana.

Tuendele tu kuwa wadanganyika, wakati wenzetu wanajitahidi kupunguza matumizi ya serikali kama magari ya kifahari n.k sisi ndo tunazaidi kuyanunua tena kwa bajeti ya mkpo
 
Umenema vyema PJ kwa mie imefikia hatua huwa naangalia bunge letu kwa bahati mbaya au nimekosa cha kuangalia kwenye TV
ni kama vile danganya toto ili tuone Tanzania bado kuna Bunge Aibu tupu

Kwa kifupi ni Bunge la mafisadi. Lipo pale kutetea na kulinda maslahi ya mafisadi ndiyo maana kwa mpenda maendeleo ya Tanzania yetu anayefuatilia Bunge letu ataona limejaa usanii wa hali ya juu. Kumbuka jinsi mijadala mizito ya Richmond, EPA, Vitambulisho vya Taifa, Wizi wa Kiwira ilivyozimwa kisanii ili kutetea maslahi ya mafisadi. Kinachouma zaidi ni kwamba hawa waheshimiwa wanalipwa mishahara mikubwa mno pamoja na marurupuru lakini wanachokifanya kule bungeni ni USANII MTUPU!
 
moz-screenshot-1.png
 
Very good observations, ni kweli bunge la Tz linatia watu hasira sana,.the very serious matter ambayo watu wanahisi na kufikiri kuwa itajadiliwa kwa kina na mapana, unakuta inajadiliwa kijuu juu tu, kweli hata mimi hili bunge letu huwa silikubali hata kidogo, wapo kwa ajili ya kuangalia maslahi yao tu kwa kifupi ni kwamba more than 75% wanajiwakilisha wenyewe.
 
Back
Top Bottom