Hiki kitendo kinanitatiza

Hiki kitendo kinanitatiza

unachohisi ndo exactly ukweli wenyewe

sasa chagua kusuka au kunyoa...

na mlishaelezwa humu na lara 1 mambo ya kwenda kupika na kusafisha nyumba subirini muoelewe

haraka ya nini?

halafu kumbe hata uhuru wa kuongea kinachokukwaza tu mbele yake huna?

utachakazwa reception kwa kumkosoa kaka?

je siku akija mama mkwe kukutukana,utaweza hata kulisema hilo?

naona umeanza taratiibu kuingia 'utumwani'..

ndo maana sometimes namuona lara 1 kawazidi dada zake akili...

Leo kwa mara ya kwanza umenigusa na like nimekupa so unajua me na wewe!

Back to topic madam charming navyokupenda nakwambia maneno 3 tu. leave the guy
 
Last edited by a moderator:
Khaa!
Pilipili usoila yakuwashia nini?
...
Unataka kucontrol nyumba kabla ya wakati?
...
Kwanini usiwe na imani na boyfrnd wako kwa matendo ayafanyayo kaka yake?
Ivi hujawai kuona mama mcharuko but mtoto katulia?
For sure boyfrnd wako hawezi kufanya kama utakavyo wewe!
Amgombeze mbele yako!
...
Na akimgombeza tu ataambiwa hivi "unajifanya mjuaji coz nipo kwako?"
...
Embu tulia utuwe kuna baadhi ya vitu ke mnachokoroa wenyewe!

Hapo hapo kwenye bold, nakataa. Wanasema an apple does not fall far away from the tree...na vibaya ni kwamba mwanafunzi huwa mzuri zaidi kumliko mwalimu aliyemfundisha...mcharuko+++
 
Haya mambo bwana ya wasichana kutaka kuolewa yanachanganya sana,kuna wengine wapo radhi kuingiliwa kinyume na maumbile eti kuonyesha tu anampenda boyfriend wake ni mwisho wa siku wanaishia kumwagwa tu.Wasichana bwana wananishangaza sana, hivi kweli hawajui kuwa unapokuwa na mchumba inatakiwa umubanie ili awe na hamu na wewe, unapomubania anakuwa na hamu na wewe HAKUNA KUPIKA, KUFUA WALA KUVUA PICHU YAKO nakuambia hata kama alikuwa ameahidi kuoa baada ya miaka 3 atajitaidi kuweka mazingira fasta ili angalau ndani ya miaka miwili akamilishe mambo.Sasa kama kila huduma ipo 24/7 kwa nini asikupige kalenda na mwisho akumwage maana ameshaonja kila kitu chako kwa hiyo huna jipya.NATAMANI SANA WASICHANA WOTE WAWE NA MISIMAMO KAMA HII NA NAAMINI NDOA ZINGEFUNGWA KILA SIKU MAANA HAKUNA VYA BURE TENA

Umesomeka mkuu...... Shukrani!
 
Binafsi! Nisingeweza kumshauri braza ktk isue kama hiyo, manake ni mtu mzima na ana maamuzi yake! Especially akiwa anaishi kwangu inakuwa ngumu zaidi manake braza lazima atakuwa na inferiority kwangu so nikianza kumsahihisha itaongeza uadui ndani yetu!

So achana na maisha ya shemeji yako, angalia maisha yako na mchumba wako! Ongeza safari ambazo hazitabiriki kwa mchumba wako ili kupata hali halisi ya maisha yake kabla hujaamua kuanza kuishi naye jumla jumla!

Kikubwa zaidi ni upendo ulionao kwake! kama unampenda then, hayo matatizo mengine yanasolvika tu bila shida!
 
Habari zenyu binafsi,

Mimi na mchumba wangu tumedumu katika mahusiano kwa takribani miaka miwili sasa, ndani ya huo muda kumekuwa na mitafaruku ya hapa na pale ila tumesolve na tunasonga. Nafahamika kwao naye nanafahamika kwetu kwa malengo ya kwamba mwakani panapo majaaliwa tufunge ndoa.

Sasa kitu kinachonitatiza ni hiki, boyfriend wangu anaishi na kaka yake, yaan kaka yake ndiye nayeishi kwa boyfriend wangu. Juzi kati nimeshuhudia kitendo ambacho sijakifurahia hata kidogo na kinanitatiza sana.

Iko hivi, ilikuwa jioni moja alinipigia simu kuwa anahitaji nikamsaidie kupika chakula fulani ambacho anakipenda, mie huyooooo nikaenda. Kufika nikakuta mazingira ya uwepo wa msichana ndani, na kweli nilipogonga akaja kufungua. Roho ilipasuka nikahisi mke mwenza, alinikaribisha as if yeye ndiyo mwenyeji, nikaingia moja kwa moja mpaka chumbani kwa boyfriend wangu. Nikabadili nguo na kwenda jikoni kufanya nilichoelekezwa. Kufika nikamkuta bidada kajaa tele jikoni anapika, nikamuuliza unaitwa nani na umetokea wapi na ni mgeni wa nani? Akanijibu ni mgeni wa "Jay" ambaye ndiyo shemeji yangu. Basi nikamtaarifu Boyfriend wangu uwepo wa mgeni huyo. Naye kaonekana kushangaa make yule shemeji yangu naye ana mchumba tofauti ya yule bidada aliyeko jikoni. Na kwa wakati huo mchumba wa shemeji yangu alikuwa kasafiri.

Basi baada ya muda Shemeji karudi na pia boyfriend wangu akarudi ila sikuona kama boyfriend wangu kachukizwa na kile kitendo cha kaka yake kuleta msichana mwingine pale kwake tofauti na anayefahamika. Mbali na hilo kuna siku tulikuwa tumetoka out ile kurudi shemeji akatoka chumbani kwake akiwa ameongozana na msichana mwingine tofauti na mchumba wake na pia tofauti na yuleeee bidada niliye mkuta jikoni.

Kiukweli nilichukizwa kile kitendo cha shemeji kubadilia wasichana watatu ndani ya mwezi mmoja, nilimhoji mchumba wangu, kwanini kaka yake nafanya vitendo vile mbele yake na yeye mdogo mtu hachukui hatua hata ya kumkanya? Pale sio ghetto bali ni nyumba ya familia, heshima inatakiwa kuwepo, yaan nilionekana mwiba make kidogo nichakazwe reception.

Kitendo kile ninanitatiza sana, kama kaka mtu anaweza kufanya vile mbele ya mchumba wangu na mchumba wangu haonekani kuchukua hatua wala kuchukia si hata mchumba wangu pia anafanya hayo????? Yaan nimekosa imani naye tena nahisi hata mimi nisipokuwepo naye huwa ananifanyia hayo hayo!! As "Birds of the same feather flock together."

Naomba ushauri wenu....

Ndimi Dada Hawa C/O charminglady

Utasubiri sana mdada, hakuna cha ndoa wala nn hapo isije ikawa kwa kisingizio anakuchunguza. Akuchunguze ye TAKUKURU ??? Kuwa makini hisia zisikupeleke bondeni, TUMIA AKILI WEWE, jitahidi umjue kiundani zaidi kuna mengi yamejificha hapo. Somethings dnt click in mind at all. Kumkosoa tu ni janga sembuse kumwambia matatzo / shida zako. Unapelekwa machinjioni alafu na we umetulia mwenyewe kama unangojea mkate wa komunio. KALAGHABAHO !!! Usije ukasubiri na huo mpete wako wa bati hadi ugeuke rangi ya ugoro ila kaa ukijua Uchumba hauna Graduation Ceremony. Usije ukaishia kupika, kufua boxer na nguo zake mpaka vidole vinukie gololi nyama. Huna chako hapo utakuja niambia.
 
why should he leave the guy...........[/QUOTE

Reasons has been advanced by the boss. kwani mumy unafikiri hao ndugu tabia zitakuwa tofauti?
Tatizo kina dada mwanamme akishapromise hata ukufanyie nini unakomaa tu thinking that h will change after marriage kwenye tabia hamna miujizza unless otherwise.

Angekuwa si mwenye tabia hizo asingerespond kwa kutaka kushusha kipigo bali angesympathize his brother misbehaviour.
To me mwanaume anayenipenda sitegemei anitishe when am asking genuine question
 
Back
Top Bottom