CharmingLady
JF-Expert Member
- Apr 16, 2012
- 18,304
- 12,999
habari zenyu binafsi,
mimi na mchumba wangu tumedumu katika mahusiano kwa takribani miaka miwili sasa, ndani ya huo muda kumekuwa na mitafaruku ya hapa na pale ila tumesolve na tunasonga. Nafahamika kwao naye nanafahamika kwetu kwa malengo ya kwamba mwakani panapo majaaliwa tufunge ndoa.
Sasa kitu kinachonitatiza ni hiki, boyfriend wangu anaishi na kaka yake, yaan kaka yake ndiye nayeishi kwa boyfriend wangu. Juzi kati nimeshuhudia kitendo ambacho sijakifurahia hata kidogo na kinanitatiza sana.
Iko hivi, ilikuwa jioni moja alinipigia simu kuwa anahitaji nikamsaidie kupika chakula fulani ambacho anakipenda, mie huyooooo nikaenda. Kufika nikakuta mazingira ya uwepo wa msichana ndani, na kweli nilipogonga akaja kufungua. Roho ilipasuka nikahisi mke mwenza, alinikaribisha as if yeye ndiyo mwenyeji, nikaingia moja kwa moja mpaka chumbani kwa boyfriend wangu. Nikabadili nguo na kwenda jikoni kufanya nilichoelekezwa. Kufika nikamkuta bidada kajaa tele jikoni anapika, nikamuuliza unaitwa nani na umetokea wapi na ni mgeni wa nani? Akanijibu ni mgeni wa "jay" ambaye ndiyo shemeji yangu. Basi nikamtaarifu boyfriend wangu uwepo wa mgeni huyo. Naye kaonekana kushangaa make yule shemeji yangu naye ana mchumba tofauti ya yule bidada aliyeko jikoni. Na kwa wakati huo mchumba wa shemeji yangu alikuwa kasafiri.
Basi baada ya muda shemeji karudi na pia boyfriend wangu akarudi ila sikuona kama boyfriend wangu kachukizwa na kile kitendo cha kaka yake kuleta msichana mwingine pale kwake tofauti na anayefahamika. Mbali na hilo kuna siku tulikuwa tumetoka out ile kurudi shemeji akatoka chumbani kwake akiwa ameongozana na msichana mwingine tofauti na mchumba wake na pia tofauti na yuleeee bidada niliye mkuta jikoni.
Kiukweli nilichukizwa kile kitendo cha shemeji kubadilia wasichana watatu ndani ya mwezi mmoja, nilimhoji mchumba wangu, kwanini kaka yake nafanya vitendo vile mbele yake na yeye mdogo mtu hachukui hatua hata ya kumkanya? Pale sio ghetto bali ni nyumba ya familia, heshima inatakiwa kuwepo, yaan nilionekana mwiba make kidogo nichakazwe reception.
Kitendo kile ninanitatiza sana, kama kaka mtu anaweza kufanya vile mbele ya mchumba wangu na mchumba wangu haonekani kuchukua hatua wala kuchukia si hata mchumba wangu pia anafanya hayo????? Yaan nimekosa imani naye tena nahisi hata mimi nisipokuwepo naye huwa ananifanyia hayo hayo!! As birds of the same feather flock together.
naomba ushauri wenu....
Ndimi dada hawa c/o charminglady
unachohisi ndo exactly ukweli wenyewe
sasa chagua kusuka au kunyoa...
na mlishaelezwa humu na lara 1 mambo ya kwenda kupika na kusafisha nyumba subirini muoelewe
haraka ya nini?
halafu kumbe hata uhuru wa kuongea kinachokukwaza tu mbele yake huna?
utachakazwa reception kwa kumkosoa kaka?
je siku akija mama mkwe kukutukana,utaweza hata kulisema hilo?
naona umeanza taratiibu kuingia 'utumwani'..
ndo maana sometimes namuona lara 1 kawazidi dada zake akili...
Habari zenyu binafsi,
Mimi na mchumba wangu tumedumu katika mahusiano kwa takribani miaka miwili sasa, ndani ya huo muda kumekuwa na mitafaruku ya hapa na pale ila tumesolve na tunasonga. Nafahamika kwao naye nanafahamika kwetu kwa malengo ya kwamba mwakani panapo majaaliwa tufunge ndoa.
Sasa kitu kinachonitatiza ni hiki, boyfriend wangu anaishi na kaka yake, yaan kaka yake ndiye nayeishi kwa boyfriend wangu. Juzi kati nimeshuhudia kitendo ambacho sijakifurahia hata kidogo na kinanitatiza sana.
Iko hivi, ilikuwa jioni moja alinipigia simu kuwa anahitaji nikamsaidie kupika chakula fulani ambacho anakipenda, mie huyooooo nikaenda. Kufika nikakuta mazingira ya uwepo wa msichana ndani, na kweli nilipogonga akaja kufungua. Roho ilipasuka nikahisi mke mwenza, alinikaribisha as if yeye ndiyo mwenyeji, nikaingia moja kwa moja mpaka chumbani kwa boyfriend wangu. Nikabadili nguo na kwenda jikoni kufanya nilichoelekezwa. Kufika nikamkuta bidada kajaa tele jikoni anapika, nikamuuliza unaitwa nani na umetokea wapi na ni mgeni wa nani? Akanijibu ni mgeni wa "Jay" ambaye ndiyo shemeji yangu. Basi nikamtaarifu Boyfriend wangu uwepo wa mgeni huyo. Naye kaonekana kushangaa make yule shemeji yangu naye ana mchumba tofauti ya yule bidada aliyeko jikoni. Na kwa wakati huo mchumba wa shemeji yangu alikuwa kasafiri.
Basi baada ya muda Shemeji karudi na pia boyfriend wangu akarudi ila sikuona kama boyfriend wangu kachukizwa na kile kitendo cha kaka yake kuleta msichana mwingine pale kwake tofauti na anayefahamika. Mbali na hilo kuna siku tulikuwa tumetoka out ile kurudi shemeji akatoka chumbani kwake akiwa ameongozana na msichana mwingine tofauti na mchumba wake na pia tofauti na yuleeee bidada niliye mkuta jikoni.
Kiukweli nilichukizwa kile kitendo cha shemeji kubadilia wasichana watatu ndani ya mwezi mmoja, nilimhoji mchumba wangu, kwanini kaka yake nafanya vitendo vile mbele yake na yeye mdogo mtu hachukui hatua hata ya kumkanya? Pale sio ghetto bali ni nyumba ya familia, heshima inatakiwa kuwepo, yaan nilionekana mwiba make kidogo nichakazwe reception.
Kitendo kile ninanitatiza sana, kama kaka mtu anaweza kufanya vile mbele ya mchumba wangu na mchumba wangu haonekani kuchukua hatua wala kuchukia si hata mchumba wangu pia anafanya hayo????? Yaan nimekosa imani naye tena nahisi hata mimi nisipokuwepo naye huwa ananifanyia hayo hayo!! As "Birds of the same feather flock together."
Naomba ushauri wenu....
Ndimi Dada Hawa C/O charminglady
Kwa nini ukapike na kusafisha nyumba wakati haujaolewa? Source lara 1
Yaani hata ukiachana na huyo aneyefata nae atakukimbia tu akijua wewe hauna akili ya kufikiria.
Sio tu waoaji hakuna hata waolewaji pia hakuna kama wadada wenyewe sio tu kusoma hawajui bali hata kuangalia picha hawawezi.
Tulia kwenu subiri uolewe ndio ukapike na kupakua..
Wanaume tunajuana, na nina uhakika 100 parcent Mchumba wako nae anafanya hivyo hivo,, ndege wafananao wanaruka pamoja
sisi waislamu tuna ambiwa hivi,mfikirie mwenzio vizuri...hata kama umemuoana mwanaume na mwanamke wanatoka kichakani jiambie ya kuwa walikwenda kila mmoja kivyake pale kichakani kutafuta mbuzi wao aliyepotelea kichakani na wakakutana kwa bahati mbaya..hata kama wanatokea guest na ukawaona,jiambie ile ni nyumba ya wageni na wametoka pale kutazama mgeni wao aliyefikia pale...ryt? Maadamu hujamfumania mchumba wako,uache hisia mbaya,ndoa na mahusiano mengi duniani yamekufa kwa sababu ya hisia mbaya,sio kwa sababu za ukweli...take it from me!
boss umenikumbusha zamani watu tulikuwa tunawah kwenye nyumba za ma bf kupanda maua, na kufagia eti ili uolewe uonekane material wife.na hili la eti mwakani tumepanga kufunga ndoa si ajabu lipo kichwani mwako
kidume hakina hata taarifa kuwa kinakuoa mwakani,mnapishana kumfulia na kumpikia tu hapo
The boss kachora rula ya chuma. Ukweli ni huu, kuna asilimia kubwa sana ya boyfriend wako kutokuwa mwaminifu na ndiyo maana anashindwa kumkemea kaka yake uovu wake. Halafu kwa nini aishi na kaka yake?? Kama hana kazi si amtafutie hata kamtaji akaanze maisha yake taratibu ili kama ufuska akaufanyie kwake??
Hebu hoji jambo hilo kwa undani na kama utaendelea kutishiwa kupigwa uamuzi ni wako uendelee au usieendelee.