Hiki kitendo cha clouds Fm kufanya matangazo karibia dk 20 hadi 25 ki ukweli kinaboa

Nina muda mrefu sijasikiliza Redio na hata kuangalia TV,kama sio miaka 5 basi 7 zaidi ya kusikiliza kibahati mbaya kutoka kwenye Daladala,sokoni na kwa Jirani yangu anayefungulia redio kama wengine hatuna hizo redio.
 
Redio zinajiendesha kwa kutegemea matangazo ndugu hivi vipindi vipo ili kusindikiza hayo matangazo..Efm mikoani hatuwapati nasikia ni nzuri
 
kweli tuna tofautiana sana mimi redio huwa nasikiliza vipindi vya magazeti asubuhi baada ya hapo nazima redio nasubiria saa saba nasikiliza taarifa ya habari ya ujerumani basi, nakuja kusikiliza tena vipindi vya michezo jioni nimemaliza

we jamaa km mimi vile
 
Habari Mkuu

Mimi ni msikilizaji mzuri wa radio lalini:-

Hiki kitendo cha clouds Fm kufanya matangazo karibia dk 20 hadi 25 ki ukweli kinaboa, yaani unasikiliza redio dk 20, unasikia matangazo tu, sidhani kama kuna msikilizaji anapenda kusikia matangazo mda mrefu ivi, hatukatazi matangazo ila matangazo ya mda mrefu yanapoteza Mvuto kabisa, naomba clouds mmbadilishe ratiba zenu, muwe creative, hiyo system yenu ya matangazo inatuboa sana

Unashangaa Clouds Fm, Jaribu kusikiliza Radio free Africa kipindi chao cha magazeti, kipindi dk30, matangazo dk 20 kipindi chenyewe dk10 tena huwa wanaanza na matangazo dk10 baada tu ya BBC kuisha then kawimbo cha utambulisho wakipindi, matangazo dk5, magazeti yanasomwa dk6 matangazo dk5, wanaendela kwa dk 2 haraka haraka. Kimeisha kipindi.

Kifupi ni kwamba hawajali mlaji anakula nini wanataka pesa tu. Uchambuzi wao ni ovyo kabisa.
 
Kuna ile stesheni inataja majina ya bar za kimara karibia masaa mawili... hio nayo ichanganye huko

Sijui kuwa siku hizi ipo hivyo au
 
Unashangaa Clouds Fm, Jaribu kusikiliza Radio free Africa kipindi chao cha magazeti, kipindi dk30, matangazo dk 20 kipindi chenyewe dk10 tena huwa wanaanza na matangazo dk10 baada tu ya BBC kuisha then kawimbo cha utambulisho wakipindi, matangazo dk5, magazeti yanasomwa dk6 matangazo dk5, wanaendela kwa dk 2 haraka haraka. Kimeisha kipindi.

Kifupi ni kwamba hawajali mlaji anakula nini wanataka pesa tu. Uchambuzi wao ni ovyo kabisa.
We acha tu

stop wishing start doing
 
Kama hutaki matangazo tafuta station nyingine kwani wamekubandika hapo kwao
na wao pia hapo ujue ndo wanajipatia hela
 
Back
Top Bottom