Ligogoma
JF-Expert Member
- Aug 27, 2010
- 3,502
- 6,460
Habari wadau wote
Nduguzangu binafsi nilikuwa nina marafiki zangu hivi wawili mmoja anapenda kujiita Jack msafi Kama a.k.a yake na mwingine Ni Musa, Na sisi wote watatu tulikuwa marafiki haswa. Jack msafi alikuwa yeye hajatulia kabisa kwenye suala la mademu jamaa anaweza kuwa na uhusiano na mademu watano kwa wakati mmoja wakati Musa yeye alikuwa kijana mpole na ametulia yupo Kama Mimi tu.
Kuna siku moja Jack msafi na Musa walijikuta wanamtaka demu mmoja but the end of the day Jack msafi ndiye alimpata kwasababu jamaa ana muonekano mzuri pia ana six pack Kama unavyojua Wanawake wengi wanapenda Wanaume wenye mionekano.Baada ya kupita muda kidogo Jack alimpa mimba huyo mdada na huyo mdada alikuwa anasoma form 6 bahati nzuri mimba yake ilikuwa changa na ndio ilikuwa kipindi Cha mitihani na kweli alifanya mtihani baada ya hiyo mimba akibidi amueleze Jack ana mimba yake Jack msafi akaikataa mimba na akavunja uhusiano na huyo dada.
Musa alimuuliza siku moja vipi Jack mbona Sasa hiv sioni upo karibu na demu wako na pia naona Hadi unamkatia simu kulikoni? Akauliza swali hilo Jack akamjibu nimeachana nae alafu ananifuatafuata yaani nikin'gan'ganizi Sana.So baada ya Musa kuona demu kamwagwa na mshikaji wake na ukizingatia bado anapenda yule demu inabidi amtongoze Tena na demu akamkubalia ila akamwambia ila mie nina mtoto hapo ikiwa tayari ameshajifungua Je upo tayali? Musa akajibu me ninakupenda japo una mtoto akamuuliza baba yao vipi Huyo demu akamjibu akamjibu mtoto Ni wa mshikaji wako na amemkataa mtoto pamoja na kunitusi Sana eti anasema kwanini nilibeba mimba mapema,Musa akamwambia Mimi ninamtreat huyo mtoto Kama baba yake usijali.
Huyo demu alikuwa tayari yupo chuo na alikuwa anampango wa kuairisha mwaka kwaajili ya malezi ya mtoto Musa akamwambia we endelea kusoma mimi huyu mtoto nitampeleka kwa Mama yangu na nitamwambia huyu mtoto ni Wangu so atamlea basi wakakubaliana hivyo.kiukwel Musa alikuwa anampenda Sana huyo dada alikuwa anamlipia ada ya chuo hata kipindi ambacho anataka hosteli Musa akamwambia achana na hostel mie nitakupangia chumba kizuri kabisa usome kwa uhuru.Na baadae akamfungulia biashara ya saloni ili imsaidie kujikimu kimaisha huyo demu alikuwa analipiwa na ada shangazi yake ila Musa akampa wazo hiyo hela ya ada anaokupa shangazi yako wewe itumie kwaajili ya matumizi yako ya kawaida ada nitalipa Mimi.Musa aliniambia Mimi kuwa anampango wakumuoa kabisa huyo demu ila ajawahi kukuambia huyo demu.
Baada yakupita muda mrefu Jack akamfuata Musa akamwambia ninataka mtoto wangu Musa alishangaa wewe ulimkataa huyo mtoto Leo nimlea eti unajifanya kuja me sikupi.Jack akaenda ustawi wa jamii na kudai haki yake,Ustawi wa jamii ukawakutanisha Musa, Jack pamoja na huyo demu Kwaajili ya huo mjadala Sasa ikafika muda wa huyo demu athibitishe je Ni kweli Jack alimkataa mtoto? Cha ajabu demu akasema hajamkaa mtoto so akamruka Musa na Musa akaonekana muongo kumbe behind the scenes Jack alimuomba msamaha huyo demu na wakarudiana bila hata Musa kupewa taarifa yoyote.
NB: Huu mkasa uliniumiza utadhani mimi nimefanyiwa, dada zetu sijui wana tatizo gani unapata husband material alafu unachezea fursa alafu mnakuja kulalamika wanaume washezi.
Ni mwiko kumsaidia mwanamke aliye kwenye stress au shida kuu!! Ukimpa relief lazima akukimbie tuu!!