Hii ya kuimba na kusali Kihaya imekaaje

Congo

JF-Expert Member
Mar 13, 2008
1,686
2,000
KKKT Bukoba wameIndua kitabu cha kwaya na kusali kwa lugha ya kihaya. Je, inakubalika ? Je, waumini wasiojua kihaya watakaokwenda kusali hali itakuwaje? Je, kwa ujumla haoo tunasonga mbele au tunarudi nyuma?
 
swissme

JF-Expert Member
Aug 15, 2013
13,659
2,000
ni vizuri wakajitenga na ni bora wawe na nchi yao maana serikali ya Tanzania haiwathamini hadi kudhurumiwa pesa za wahanga bukoba kwangu ni bora wawe na nchi yao tu.

swissme
 
Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
15,127
2,000
Hayo mambo ya kawaida sana huko kaskazini. Biblia inatafsiriwa kwa lugha zote na watu wanasali kwa lugha zao. Nimeshaona Biblia za Kichaga na nyumbani ninayo ya Kinyakyusa.

Sisi Mungu wetu sio kabila fulani kwamba asielewe lugha ije kutulazimu kujifunza lugha gani sijui.
 
chongchung

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
4,136
2,000
Mambo ya kawaida sana hayo Arusha pia KKKT wanaendesha misa kwa kimaasai na Bible ya kimaasai ipo halikadhalika kwa wachagga Roman Catholic.
 
balibabambonahi

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
10,033
2,000
KKKT Bukoba wameIndua kitabu cha kwaya na kusali kwa lugha ya kihaya. Je, inakubalika ? Je, waumini wasiojua kihaya watakaokwenda kusali hali itakuwaje? Je, kwa ujumla haoo tunasonga mbele au tunarudi nyuma?
Mbona sisi huko Biirabo toka tukiwa wadogo tunasali kihaya na hata kitabu cha nyimbo na liturjia cha kihaya kipo!
Kaimbe na kusali kikwenu
 
Eyce

JF-Expert Member
Mar 16, 2016
3,403
2,000
Hahahaaaaaa unanikumbusha nilipokuwa nasoma high school kagera...

Sasa kuna padre alikuwa mzee yaani siku hiyo akiongoza misa ..waswahili tumekwisha maana Mnaingia kanisani lakini misa inaendeshwa kwa kihaya kwa kila kitu labda kwaya tu waimbe kwa kiswahili

Lakini ilitupelekea tuanze kujifunza kihaya na si lugha ngumu kunifunza maana hata wenyeji hujisikia fahari pale mgeni anapoonesha nia ya kujifunza tamaduni zao
 
mdetichia

JF-Expert Member
Feb 13, 2015
5,293
2,000
KKKT Bukoba wameIndua kitabu cha kwaya na kusali kwa lugha ya kihaya. Je, inakubalika ? Je, waumini wasiojua kihaya watakaokwenda kusali hali itakuwaje? Je, kwa ujumla haoo tunasonga mbele au tunarudi nyuma?
Hata kule kwetu Kilimanjaro ibada zinaenda kichaga kwenye litrugia na huko vijijini kuna watu hawajui kiswahili vizuri unachoshangaaa ni kitu ghani.
 
mdetichia

JF-Expert Member
Feb 13, 2015
5,293
2,000
Hayo mambo ya kawaida sana huko kaskazini. Biblia inatafsiriwa kwa lugha zote na watu wanasali kwa lugha zao. Nimeshaona Biblia za Kichaga na nyumbani ninayo ya Kinyakyusa.

Sisi Mungu wetu sio kabila fulani kwamba asielewe lugha ije kutulazimu kujifunza lugha gani sijui.
Huyu mshamba tu mbona kingereza anakiona cha maana chake hicho umasikini wa fikra mbaya sana
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
18,370
2,000
ni vizuri wakajitenga na ni bora wawe na nchi yao maana serikali ya Tanzania haiwathamini hadi kudhurumiwa pesa za wahanga bukoba kwangu ni bora wawe na nchi yao tu.

swissme
Siasa zimeharibu ubongo wako
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom