Hii ya bot imekaaje du!

Amakando

Senior Member
May 9, 2011
158
27
Wadau nimejiuliza na kukosa majibu, hivi kweli tasisi nyeti namna hii inashindwa kuwa na namna nzuri na ya kisasa ya kuwasilisha maombi ya kazi kwa njia ya E-mail mpaka tutumie posta? je kuna ugumu gani wa meneja mwajiri kuwasiliana na watafutao kazi ambazo zimetangazwa nae (BOT) kwa njia ya kielectronic? Au ni mwendelezo ule ule wa kupeana ajira kwa njia ya kujuana? je wenye sifa na ambao wako mikoani mbali na Dar wafanyeje? du nimebaki na labda!!!!! nisaidieni :sleepy::sleepy:
 
wadau nimejiuliza na kukosa majibu, hivi kweli tasisi nyeti namna hii inashindwa kuwa na namna nzuri na ya kisasa ya kuwasilisha maombi ya kazi kwa njia ya e-mail mpaka tutumie posta? Je kuna ugumu gani wa meneja mwajiri kuwasiliana na watafutao kazi ambazo zimetangazwa nae (bot) kwa njia ya kielectronic? Au ni mwendelezo ule ule wa kupeana ajira kwa njia ya kujuana? Je wenye sifa na ambao wako mikoani mbali na dar wafanyeje? Du nimebaki na labda!!!!! Nisaidieni :sleepy::sleepy:


sio mahali pake.....
 
Si sehemu husika! Lakini wewe si unaomba kazi,hujawahi sikia muomba kazi hajui kusoma wala kuandika? Nadhani mkuu ufuate maelekezo unajua hata hiyo unayosema ni njia nzuri kuna wengine hawajawahi itumia.
 
Si sehemu husika! Lakini wewe si unaomba kazi,hujawahi sikia muomba kazi hajui kusoma wala kuandika? Nadhani mkuu ufuate maelekezo unajua hata hiyo unayosema ni njia nzuri kuna wengine hawajawahi itumia.
Ila mkuu ninachazungumzia ni ile kutokuwepo kwa njia mbadala za kisasa kwa taasisi nyeti kama B.O.T kwa watu tulio mbali kuweza kuwafikia, maana hapo ingelikuwa rahisi kutuma vivuli vya kile kinachotakiwa hebu tafakari huna namna ya kupata gazeti kutokana na mazingira uliyopo halafu ukabahatika kuingia kwenye net nakukuta tangazo la kazi ambalo linakwisha muda wake ndani ya siku mbili, huoni kwamba kwa njia ya posta ni sawa na kwamba itakuwa ngumu kufika kwa wakati?
 
Back
Top Bottom