Hii vita iraisha lini?

Hii vita iraisha lini?

VanDon

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2013
Posts
418
Reaction score
699
HII VITA ITAISHA LINI.

#HABARI Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema ameviamuru vikosi vyake kusimamisha shughuli zote za kijeshi nchini Ukraine, huku akitangaza "usitishaji vita kipindi cha Pasaka" hadi Jumapili.

Kwa upande wake, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema Kyiv imezingatia makubaliano hayo, lakini akaishutumu Moscow kwa kuyavunja.

"Ikiwa Urusi sasa iko tayari kuingia katika mazungumzo ya kumaliza vita kabisa na yasio na masharti, Ukraine itachukua hatua ipasavyo kwa kuakisi vitendo vya Urusi,"

"Vitendo vyetu viko na vitakuwa vya ulinganifu. Pendekezo la kusitisha vita kabisa bila masharti kwa siku 30 bado liko mezani jibu lake linapaswa kutoka Urusi," aliandika Zelensky kwenye X.

Zelensky amesema Ukraine itakuwa tayari kuongeza muda wa makubaliano ya kusitisha mapigano zaidi ya tarehe 20 Aprili, akionekana kurejelea pendekezo la awali kutoka kwa Marekani la kusitisha mapigano kwa siku 30 ambalo tayari Ukraine ilikuwa imekubali.

Akijibu kuhusu tangazo la Putin, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andriy Sybiha aliandika kwenye X: "Putin sasa amezungumza kuhusu utayari wake wa kusitisha mapigano. Saa 30 badala ya siku 30."

"Kwa bahati mbaya, tumekuwa na historia ndefu ya kauli zake kutoendana na matendo yake. Tunajua maneno yake hayawezi kuaminiwa na tutaangalia vitendo, sio maneno," aliongeza.

Putin alitangaza usitishaji vita wa muda katika mkutano na mkuu wake wa majeshi Valery Gerasimov. #EastAfricaTV
 

Attachments

  • FB_IMG_1745141938317.jpg
    FB_IMG_1745141938317.jpg
    125.9 KB · Views: 17

Similar Discussions

Back
Top Bottom