Liquid protector ni protector nzuri sana sina haja ya kuzielezea ubora wake kwa ambao mmeweka hamna hasara yoyote kama wewe uliyeweka hiyo protector umeweka kwa mtu anayetumia mashine ya kiwango,nasema mashine kiwango kwani liquid protector ina mashine za aina tatu
1.Mashine ya kwanza inauzwa 1.5M,
2.Mashine ya pili inauzwa 600k,
3.Mashine ya tatu inauzwa 350,000.
Utendaji kazi wa hizi mashine ni mmoja ila ubora wa liquid ni tofauti sana,mashine no 1 liquid yake ina protect kweli na ndio maana halisi ya protection inapatikana kwenye mashine no.1,ukiweka liquid ya mashine no.1 simu yako haitovunjika milele na milele,haitoingia mkwaruzo hata mmoja,sifa zote zipo hapa. BEI ya kuweka 30,000k (kama umeweka liquid kwa bei chini ya hii tambua haujatumia hii mashine)
mfano wa ubora wa mashine hiii angalia hii video
Mashine namba mbili liquid yake haina nguvu ya kukuta mashine no.1 japo nayo ina protect kioo cha simu yako,bei yakuweka ni 20,000-15000,
Hivii ndivyo inavyoonekana mfano wa picha yake ni hii hapa
View attachment 1328441View attachment 1328442
tukija mashine namba 3 hii ndiyo ambayo imezagaa mitaani na kila kona unaikuta,hii liquid yake inalinda kioo kisipate mkwaruzo TU usije ukamuiga kuifanyia simu yako mtu aliyeweka liquid kwa mashine no.1 na no.2 utalia kilio cha mbwa koko maana simu itavunjiika vizuri tu,liquid ya mashine hiii hukinga simu na kuiweka mbali na mikwaruzo tu,bei ya kuweka hii liquid n 5000 ukienda k.koo utazikuta zimezagaa wape 5000 tu watakuwekea.
USHAURI:
hamna muuzaji atakwambia mashine yake ni ipi,(ni siri yake) kwa hiyo kwasababu hamzijui nawashauri simu zenu mkishaweka liquid,malizieni na zile 3D protector kwa kujiridhisha,namaaanisha muweke protector mbili.
ila kama una uhakika hiyo liquid ni ya mashine no.1 huna haja ya protector nyingine juu,umeshamaliza hata itokee simu imedondoka toka juu ya kabati hadi chini kioo kikatua juuu ya stuli hofu na shaka ondoa.