Hii teknolojia ya “ceremic liquid” ya screen protector kwenye simu kitalaamu ni salama kweli?

PhD Palla

Member
Dec 27, 2019
7
45
Uliwaza mbali Sana ,kuuliza Hilo swali,big up
Habari za hapa,
Jana nilikuwa Mororogo Mjini nikapita mahali nikaona kijana moja akielezea teknolojia mpya ya kulinda kioo cha simu ya Ceremic Liquid na nyingine ya protector fulan hivi ngumu.

Hii teknolojia ya ceremic anatumia vimiminika fulani hivi vya aina kama 4 alafu anaweka simu kwenye ki mashine kama picha inavyo onyesha na baada ya dakika 10 inakuwa tayari hapo anajaribu ikitoboa na hiyo drili mashina na simu haitoboki wala kuchubuka pia hata misumari na vitu vyenye ncha havichubui.

Ya pili baada ya Ceremic anaweka hiyo Protector ngumu (extreme lamination)na kioo kinakuwa strong kiasi kwamba anapigilia msumari kwenye hicho kibao na simu kabisa kwa upande wa kioo.

Sasa niliangalia nikiwa na maswali hii ni salama kwa simu kweli ? Baadae haitaleta madhara kama kuondoa sensitivity ya kioo ? Na nilimuuliza inaweza toka akasema hapana labda utoe kioo chote!

Naamini hapa kuna wataalamu walisha iona hata kuijua vyema wanaweza elezea zaidi CHIEF MKWAWA pia natumai ulisha sikia hii
View attachment 1312781
View attachment 1312782

Sent using Keo
 

Eng. Zezudu

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
4,852
2,000
Sasa kama ikapasuka inapasuka na kioo si bora nibaki na kioo tu pekee

Napenda zile protector za kawaida zenyewe huwa hazijakaza sana hata simu ikipata shock yenyewe ina act as shock absorber ina crack haraka kioo kinabaki safe

In short protect huwa ni kwa ajili ya kukinga scratches kwenye kioo na sio kuzuia kioo kupasuka!

Kinachokilinda zaidi kioo kisipasuke ni zile kava za juu hata simu ikidondoka toka height flani!.

Sent using Jamii Forums mobile app
Simu yangu inakava ilidondoka protector ikapasuka na kuscratch

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Napoleone

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
8,950
2,000
“Much know “ ndio tatizo la bahadhi ya member wengi hapa mada iko wazi we unaleta mada juu ya mada. Punguza kiherehere cha kujua sana na mihemko na changia hoja kama inavyo taka . Poor
Kakuuliza swal la msing lakin
 

Eminentia

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
2,480
2,000
Kuna review niliona YouTube wakawa wanafanya same test kwa simu tatu zinazofanana moja haina protector ya pil inayo ya glass ya tatu inayo hiyo ya liquid ....sasa kuna saa ya glass ilipasuka pia ile ya liquid kuna test iliweka ufa tatizo likaja ile ya liquid haifai kutoa lkn jamaa aliweza toa ile ia glass na kuweka ingne simu ikawa mpya kwa hiyo wakapendekeza bora glass maana ikiharibika unatoa
 

Wick

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
8,323
2,000
Screenshot_20200117-051438.jpg
Screenshot_20200117-053429.jpg
 

trey007

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
731
1,000
Naona mmevimisi vile vioo vya simu za bird disko na oking the home of mikwaruzo the sense of kucha😂😂😂
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom