Maajabu ya voicemail kwenye simu

Maajabu ya voicemail kwenye simu

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,288
Reaction score
2,597
Live voicemail ni feature mpya kwenye iOS ya 17 ni kipengele cha ujumbe wa sauti unaotokea kwenye simu yako wakati mtu amekupigia simu.

Ni feature ambayo inaitwa live voicemail itayoweza kukusaidia kuweza kupokea ujumbe baada ya kupigiwa simu ila ukupokea akaamua kuacha ujumbe wa sauti wakati anapiga utaweza kuona ujumbe huo kupitia simu yako.

Itakupa fursa ya kuweza kuchagua either kupokea au lah kwani utaweza kuona jinsi gani iyo simu unayopigiwa ni ya umuhimu gani kwako? Apple walisema hii ni feature itakusaidia kuchagua labda upokee simu au lah.

Utaweza kuona maandishi yanayotokea kwenye simu yako wakati mtu anakupigia alafu ujapokea kuna maandishi yatatokea wakati mpigaji anakupigia utakua na uwezo wewe mpokeaji kuyasoma na kuchagua either kupokea hiyo simu au lah.

Kwaiyo mawasiliano yanayofanyika yatakua ni siri kabisa na wala usijal kuhusu usalama wa taarifa au sauti yako wakati unapiga simu taarifa Zako hazitaweza kuhifadhi mahali popote pale kwaiyo ni salama.

Je jinsi gani inavyofanya kazi [emoji116]
• Ikitokea mtu ameacha ujumbe wa sauti kwenye simu yako , utaweza kuona maandishi ambayo yanakua live yakipita kwenye kioo chako.
• utakua na uwezo wa kuyasoma wakati muhusika anakupigia simu ila ujapokea ivyo utaweza kusoma na kuona Kuna umuhimu wa kupokea simu yake au lah
• utaweza kuamua kumpigia huyo mtu aliyekupigia ukupokea au ukaamua tu kutopokea bali kusikiliza tu ujumbe wa sauti aliyosema wakati amekupigia simu

Utaweza kuamua kumpigia simu au kumtumia ujumbe au Kuendelea na mambo yako ukimaliza utampigia.
voicemail.jpg
 
Back
Top Bottom