Hii tabia ya wavulana ikome

Hii tabia ya wavulana ikome

Nakapanya

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Posts
2,096
Reaction score
709
Mapenzi ni starehe bwana,mapenzi kupeana raha.

Siku hizi imezuka tabia ya mijitu hasa wavulana ( ndio nawaita wavulana kwani akili zao ni za kitoto hata kama ni wanaume),unakuta jitu linaacha kufanya kile kinachotakiwa kufanywa (mapenzi/sex) jitu linakazana kurekodi tendo lile kwenye visimu vyao,mbaya zaidi yeye hajichukui sura ila binti wa watu ndio full kuonekana.

Najiuliza hivi wewe una akili gani mpaka kuacha kufanya yanayofaa kufanywa na kuanza kumrekodi mwenzako ili tu kesho ukamdhalilishe kwa wenzako?hivi unawezaje kwanza kuchukua hiyo video au picha katikati ya tendo ilihali nijuavyo mimi katika tendo lile mtu hutamani hata macho yaangalie kwengine?au ndio unakuwa umeenda pale tu ili ukamdhalilishe mwenzio?

Juzi nilikuwa kijiwe kimoja nikakuta watu wanaonyeshana video za ngono,anayewaonyesha wenzake ndiye aliyepiga hiyo video.yule binti yule wa pale naniii..(sitaji eneo) ndio huyu bwana,jana nimemgonga na video angalieni hii hapa na wenzake wanamshangilia eti we jamaa mkali balaa.

Tabia hii siipendi na inadhalilisha sana dada zetu(sisi wengine tuna dada wengi tu).Hebu fikiria siku moja ndio unakutana na video ya dada yako ndio amefanyiwa hivyo utajisikiaje?au ghafla unakutana na video ya mama yako mzazi alikuwa na michepuko huko wakamchukua video utajisikiaje?
Vile ambavyo utajisikia ndio vile ambavyo mwenzio uliyemfanyia hivyo pamoja na ndugu zake wanavyojisikia.

Achezi tabia hii kwani ni ya kishenzi na ya kidhalilishaji kabisa.kama unaona huwezi kufanya mapenzi bila kurekodi basi acha.

Nyinyi DADA zetu mkiona mpo faragha na jitu linatka likupige picha au video usikubali,vaa nguo zako tembea tena iwe ndio mwisho wa mahusiano yenu,maana huyo hana nia nzuri,anakupiga picha au video ili kesho akakudhalilishe,na mnadhalilika kweli nyie hamjui tu.Video zenu za utupu watu wnaonyeshana vijiweni au hata whatsapp.Wewe ukipita mitaani unaona kama upo sawa tu kumbe watu wankuchora tuu ndio si wameisha kujua kila kitu kuanzia ndani mpaka nje.

Kwa waungwana hii tabia hatuifanyi hata kidogo,naomba na wewe unayependa tabia hii tafadhali badilika maana vinginevyo utakuwa kwenye kundi la washenzi na wapumbavu tu.
 
Na ifikie wakati kina dada/ mama wawe na msimamo ,,,,,,,, ukihisi kurekodiwa katisha utamu vunja simu au futa hiyo video immediately
 
hizi simu za kisasa zimeleta mambo acha kabisa
 
Siyo wanaume tu hata nyie wanawake ndo mnapenda kuturekodi mkawaonyeshe mashoga zenu kuwa yule boy wangu ni nouma hebu muoneni anavyonipandisha juu ya mlima
 
Na ifikie wakati kina dada/ mama wawe na msimamo ,,,,,,,, ukihisi kurekodiwa katisha utamu vunja simu au futa hiyo video immediately

mimi nasema na ndio iwe mwisho wa mahusiano yenyewe maana huu ni udharirishaji.
 
hizi simu za kisasa zimeleta mambo acha kabisa

lakini ni uzuzu tu simu wameleta ili tutumie vema na si kwa uhalifu au kuwakwaza wengine,kama ni hivyo kwanini asijirekodi na yeye aonekane ili tujue kweli simuya kemera imemzuzua?
 
Siyo wanaume tu hata nyie wanawake ndo mnapenda kuturekodi mkawaonyeshe mashoga zenu kuwa yule boy wangu ni nouma hebu muoneni anavyonipandisha juu ya mlima

kwanza mimi sio mwanamke ni mwanaumetena sio mvulana.Nimeandika haya kupinga udhalilishaji huu kwa dada zetu.sidhani kama hilo ulilosema lina ukweli ndani yake.wanawake hawana ujinga huo na hata kama wapo sidhani kama mwanaume atakubali kuchukuliwa hiyo video.
 
wadada nao wenyewe wanapenda, siku hizi mapenzi ya vijana hayana utamu, utamu wote upo kwenye pesa, kudinyana miaka ile unadinya huku unafumba macho kwa utamu, hutamani hata kushika glass, siku hizi mtu anadinya huku anatuma meseji, anarekodi, anaimba, anacheka.
 
ndio shida kudeal na wavulana wanaobalehe. Deal na watu wenye akili zao timamu tena wamekomaa, wanajua wanachokifanya
 
Ayaaaaa!! Yani ndo nilishaanza kurekodi hapa! Ngoja nifute tu
 
kwani wakati mwanaume ana-shoot hiyo video mwanamke anakua kazimia? ndo wakome kugongwa ovyo! wengi wanaofanyiwa hivyo ni malaya tu kama wale wanaojiuza.
 
lakini ni uzuzu tu simu wameleta ili tutumie vema na si kwa uhalifu au kuwakwaza wengine,kama ni hivyo kwanini asijirekodi na yeye aonekane ili tujue kweli simuya kemera imemzuzua?

ila nadhani wengine wanatoa consent, si unajua mapenzi niondoe ufahamu!!
 
Hata mimi nimetokea kuichukia sana hiyo tabia.

Ila cha muhimu ni wanawake kuwa makini kwani wanaume wengine wanageuza miradi.
 
kuna suala la picha za mnato ambazo wadada wengi hupenda sana kujipiga na kutuma kwa wanaume kwa kuamini ndo anamsisimua hajui kama ikifika huko itazunguka kwa watu wangapi ... mambo ya kujirekodi pia baadhi ya wadada wanaona fahari hata kuamini wanapenda kumbe kudhalilishwa tu ... ifikie mahali wajitambue thaman yao .. na pia wanaume unapomuonyesha mtu ulichorekodi wakati wa tendo ni ulimbukeni
 
wadada nao wenyewe wanapenda, siku hizi mapenzi ya vijana hayana utamu, utamu wote upo kwenye pesa, kudinyana miaka ile unadinya huku unafumba macho kwa utamu, hutamani hata kushika glass, siku hizi mtu anadinya huku anatuma meseji, anarekodi, anaimba, anacheka.

hahaaa hilo neno kudinya umenikumbusha mbali sana.yote ya yote ni ujinga tu
 
ndio shida kudeal na wavulana wanaobalehe. Deal na watu wenye akili zao timamu tena wamekomaa, wanajua wanachokifanya

ndugu yangu hapo nimedeal na wote,hao watu wazima mimi nimewaweka kundi kundi moja na wavula kwani akili zao zinafanana.Anayefanya mambo ya kitoto basi na yeye ni mtoto
 
Asiyejua thamani yake kamwe hawezi kuthaminiwa na wengine. Wenye hekima, busara na wanaojithamini kamwe hawawzi fanya kitu ambacho kitamondolea heshima a thamani mwengine.

Kurekodi na kujionysha ulichojirekodi tena ukiwa mtupu ni kujkosea heshima na kutojijua thamani yako. Ni ujinga na upumbavu uliopitiliza.
 
Back
Top Bottom