dexterous
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 2,038
- 3,124
Wasalam
Iko hivi kuna tabia/mazoea kwa wavutaji wa sigara wanaovuta sigara kiholela barabarani na sehemu zenye mikusanyiko ya watu bila kujali afya za watu wengine
Embu fikiria uko njiani unatembea mbele yako kuna mtu anavuta sigara na ule moshi anaoupuliza wote unawarudia mliokuwa nyuma yake mtake msitake mtavuta tu sasa huu sio ustaraabu kwa kweli tambua kuna watoto wadogo wanaathirika pia.
Kama kwenye ma bar na sehemu nyingine za starehe wameweza kuweka smoking zone vipi huku nje tunashindwa nini.
Naiomba serikali kupitia waziri wa afya wekeni utaratibu na pahala kwa hawa ndugu zetu wanaovuta sigara wavute sigara zao bila kuathiri watu wengine, ikiwezekana waweke adhabu kali ili kuthibiti tabia hiyo.
Na kama wewe unajijua ni mvutaji wa sigara ni vyema ukatafuta pahala ukavuta ukishamaliza endelea na safari yako kuliko kuhatarisha afya za wengine.