Hii tabia ya kuwapa no rafiki zenu kuwajaribu wapenzi wenu, mwenzenu imemtokea puani

Simbamteme

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
784
2,063
Kuna kisanga kimoja kimetokea leo kazini kimenifanya nicheke sana..hii tabia ya watu KUTOWAAMINI wapenzi wenu then mkaamua kuwatafuta RAFIKI zenu WATEST uaminifu wa wapenzi wenu plz msije kulaumu pindi kibao kikigeuka...ni bora mtafute mbinu nyngne za kupima uaminifu wa wapenzi wenu tu..

INSHU IPO HIVI

Nipo mkoa ×..na hapa nilipo nna rafiki yangu ana manzi wake ambae anafanya kazi mkoa huu huu lkn ofisi tofauti na yetu

Sasa huyu rafiki yangu yupo vzr tu na manzi wake..na alikuwa na mipango mizuri kbs ya kumweka huyu manzi ndani mazima(manzi alikuwa hajui )..jamaa alikuwa bado anamsoma huyu manzi

Sasa huyu manzi sijui alihisi nn bhana akaamua KUTEST uaminifu wa mpenzi wake kwa kumpa no Shosti wake ambae yupo DSM amsaidie KUMHADAA Mr wake

Kweli manzi alimpigia simu jamaa akajitahidi kumuingiza jamaa KINGI ila jamaa aliamua kumpotezea tu KIAINA..inshu ikapita...Kumbe jamaa ana yake Kichwani

Alipopata likizo kwenda DSM si akamcheki yule manzi kwa no nyngne tofauti kbsa..kwa vile alishawahi kuongea nae Once haikuwa kazi ngumu kujua ABC za huyu manzi..basi wakapanga appointment wakaonana

To make the story short,jamaa alijitafunia manzi mpk likizo ilipoisha akarudi kazini fresh

Sasa kisanga kimeibuka leo baada ya yule manzi wa Dar kupost picha whatsapp Status yupo na jamaa...Bahati mbaya huyu manzi wake wa huku kaiona

Kumbe bhana rafiki yangu alikuwa hajui kama manzi wa DSM anajuana na manzi wake wa huku...na yule Manzi wa DSM alikuwa hajui kuwa jamaa angu anatoka na rafiki yake wa huku(coz rafiki yake wa huku hakumpa picha ya jamaa anafananaje)....kwa hiyo mwisho wa siku jamaa kapita na marafiki wawili hivihvi

Hapa jamaa anajipanga namna ya ku SOLVE huu msala maana kashaharibu kote kote(kwa SIDE CHICK na MAIN CHICK)


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unamnusisha German Shepherd nyama.! Kwa nn asiitafute aitafune haaah haaah.!
 
Back
Top Bottom