Quinton Canosa
JF-Expert Member
- Nov 2, 2012
- 1,228
- 1,264
Wewe unahisi nnkwa hiyo huyo jamaa ako amekuomba uilete hii issue yake huku jf au?
Bahati mbaya jamii zetu na hata waoaji au waolewaji bado wana uelewa finyu kuhusu ndoa.....
Ndoa ni muunganiko wa watu wawili waliopendana na wakaamua kuishi pamoja....kama mwili mmoja....hapo haisemwi kama ni makabila gani na wala ni watu wa asili gani bali kinachoongelewa ni watu wawili waliopendana kwa kuwa mapenzi hayana mipaka.....
Na vile vile suala la mtu kuoa au kuolewa ni suala binafsi...nikiwa na maana linamhusisha mtu mmoja yeye kama yeye....kitendo cha kumuingilia mtu kwenye maamuzi yake yanayohusu ndoa ni sawa na kitendo cha kuyaingilia maisha ya mtu ingawaje kushauriana na mambo ya kawaida hakuna mkamilifu...lakini ushauri wako usiwe kwa shunikizo la yeye achukue maamuzi......
Mchuma janga hula na wa kwao. Ndugu hususan wazazi wana haki ya kuingilia ndoa za watoto wao. Wao walishi, kuna mambo mengi wameyaona sasa unapotaka kufanya jambo ambalo wanaona dhahiri athari yake hawawezi kukaa kimya lazima walisema au kupinga. Wewe una maamuzi ya kukubaliana nao ua kutowasilikiliza.
Si kweli kuwa kila wawili wanapooana basi wameunganishwa na upendo. Ndoa inaweza kuwa ajira, ndoa inaweza kuwa mkakati wa kujipatia mali hata kwa kufanya mauaji au kwa talaka iliyokusudiwa tangu awali kabla ndoa haijafungwa. Ingekuwa kila ndoa ni upendo tusingeshuhudia dhahama kibao kila siku mmoja wa wanandoa akilalamika. michepuko n.k.
Ukiingiza siasa katika suala la ndoa lazima iko siku utajuta hata kimya kimya.
Hiyo ni muhimu mkuu usichukue. Mimi hapa nikivutiwa na demu machoni na kumuita,baada tu ya salam naulizia mkoa wake wa asili ili nitabiri kabila lake, then namuuliza kabila nikisikia "nshomile" au jamii zao napiga chini na kuanza kuulizia ndizi badala ya gemu.Habari za mchana wanajamvi,
Kuna hiki kitu binafsi mimi sikipendi japo bado kimekuwa kigumu kutoka kwenye baadhi ya vichwa vya watu.Wiki moja iliyopita jamaa yangu ambaye ni mwenyeji wa mkoa wa Mbeya alitembelewa na binti nyumbani kwao,jamaa akaona isiwe shida ikabidi amtambulishe kwa wanafamilia kama mchumba wake mtarajiwa,cha ajabu baadhi ya ndugu wa mwanaume wakauliza huyo msichana ni kabila gani, jamaa akawajibu ni mchaga wa machame, basi wote wakakaa kimya.
Yule binti alipoondoka tu maneno yakaanza mara oooh ndugu yetu sisi hatutaki uoe mwanamke kutoka uchagani aidha machame,au mpare na makabila yote ya mkoa wa Kilimanjaro,ukawa mjadala mrefu jamaa akaanza kubishana kwamba anaoa anayejisikia yeye ukawa ugomvi mkubwa sana na ndugu wa mwanaume wakaanza wakamwambia likimpata la kumpata asiwashirikishe kwani wao wanajua tabia za makabila haya.
Jamani hii tabia itaisha lini kwani makabila haya yana nini kibaya mpaka kunakuwa na ubaguzi wa aina hii.
Maoni yenu wakuu
Wewe binafsi unawaelewaje wachagga wa machame? Tuanzie hapo.Habari za mchana wanajamvi,