Hii tabia siipendi, sijui wewe vipi

Hii tabia siipendi, sijui wewe vipi

Emc2

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
16,808
Reaction score
16,968
Nawasalimia wana JF, Mambo.

Aise kunatabia moja kweli huwa siipendi.
Unakuta labda mko sehemu fulani mmekaa eidha kwa maongezi au mmetoka out.
Unakuta, mmetoka na mtu yaani yeye yuko busy na simu, anachati tuuuuu haoneshi ushirikiano kama mko pamoja.

Wakati mwingine anacheka peke yake na simu. Yaani hii tabia inanikera sana.
Unakuta sometime mmetoka out malipo unafanya mwenyewe na mko na mazungumzo ya muhimu.

Kwa kweli binafsi hii tabia siipendi kabisa, wakati mwingine mtu unamuheshimu kabisa halafu yuko busy na simu, hivi haya ni maendeleo, usasa, dijitali au kitu gani sasa.

Kuna mtu niliwahi kumuambia "Sio vizuri mkiwa na mtu wewe uko busy na simu" Dah jibu nililo pewa acha tu.

Wana JF hivi mnaionaje hii iko poa au mimi tu.

Nawasilisha hoja.

karibuni

Sio tabia nzuri kabisa,ila wengi unakuta hawako interested na hayo mazungumzo au unam-bore sema anashindwa kusema...
 
Sio tabia nzuri kabisa,ila wengi unakuta hawako interested na hayo mazungumzo au unam-bore sema anashindwa kusema...
Lakini unakuta sometimes mko watu kama watano hivi, kila mtu anaongea, but yeye pekee yake unaonaje mzee wa calculus?
 
kama vipi unamchana live. "ebana eee, kama uko busy, au kama unachofanya ni muhimu zaid its better ukaondoka!".. simple like that.
 
Nilishawahi kuwa na boyfriend siku za nyuma hiyo ndo iliuwa tabia yake, hataka km yuko juu mnaniniliu simu yake ikiita anapokea kiukweli niachana nae kwa tabia km hiyo hapo
 
Kweli aisee... Kuna jamaa alikuwa ananisisitiza nikamtembelee gheto, nimeacha shughuli zangu nimeenda kwake, mtu anakuwa bize na simu. Hakuna stori hakuna nini... Ukimuukiza kitu anakujibu baada ya dak 2... Kisa simu...
 
Ukiona hali hiyo aga kama unaingia toi then sepa.
Akija shtuka akikupigia mwambie "nilikuacha uendelee na simu yako nitarudi siku nyingine ukimaliza hiyo mambo"

But ukiona hivyo ujue wewe amekudharau na uzito amepewa mtu mwingine.
Na if hata ni wako mnaweza mkawa mko kwa mambo yenu while anatumia hisia za mwingine.

Piga chini mara moja.
 
Kwanini usiinuke, huyo hajakuheshimu hata kidogo au you're too boring. Mimi siwezi, naondokaga hata kama namuheshimu labda ni mkubwa, ni kheri kumwambia nitarudi baada when you're free
 
hakika wengi ni urimbukeni uliopitiza kwani ndo matokeo ya sms 250-300 au zaidi za BURE BURE kwani ingekuwa kila text unayotuma unalipia kama tulivyokuwa tunafanya kipindi cha nyuma , hakika heshima ingekuwepo, coz hii tabia ya kujifanya uko busy na simu ina kera tena sana, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kutoa machungu yangu dhidi ya tabia hii hasa kwa maduu an mabraza men.
 
Mkuu kwani unadhani free texts tu ndo zinafanya watu wawe busy?
Mbona wengine ni addict wa JF, FB, Whatsapp, Twitter na mablog kibao. Saa zote wako full on air. Wana betri tatu tatu na mobile charger juu.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mkuu ukiwa na mtu kama huyo kwanza mkifika mkubaliane tu no phone until the mtoko is over. La sivyo akikataa mkiingia tu ukaona mambo yanaendelea basi nyanyuka sepa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Nawasalimia wana JF, Mambo.

Aise kunatabia moja kweli huwa siipendi.
Unakuta labda mko sehemu fulani mmekaa eidha kwa maongezi au mmetoka out.
Unakuta, mmetoka na mtu yaani yeye yuko busy na simu, anachati tuuuuu haoneshi ushirikiano kama mko pamoja.

Wakati mwingine anacheka peke yake na simu. Yaani hii tabia inanikera sana.
Unakuta sometime mmetoka out malipo unafanya mwenyewe na mko na mazungumzo ya muhimu.

Kwa kweli binafsi hii tabia siipendi kabisa, wakati mwingine mtu unamuheshimu kabisa halafu yuko busy na simu, hivi haya ni maendeleo, usasa, dijitali au kitu gani sasa.

Kuna mtu niliwahi kumuambia "Sio vizuri mkiwa na mtu wewe uko busy na simu" Dah jibu nililo pewa acha tu.

Wana JF hivi mnaionaje hii iko poa au mimi tu.

Nawasilisha hoja.

karibuni

Huwa anaweza kuwa na dhararua ya kuongea na simu mara chache, lakini mtu anayechat full time wakati mmeitana kwa mazungumzo huwa natafsiri ni kama kitendo cha kudharau wito au mazungumzo mliyoitiana na hivyo ni bora kuvunja kikao/mazungumzo na kuondoka maana maana halisi ya kikao/mazungumzo inakuwa haipo na mhusika unaishia kuboreka tu ...!
 
Ni kumweleza tu mkuu unajua binadamu kila siku huwa tunajifunza kanuni ambazo si rasmi kutokana na exposure, kama vile watu mnaweza mkawa mnakula meza moja lets say hotel, kama hujui sijui wenyewe wanaita table manner ukimaliza kula unasepa unawaacha wenzako lakini wenyewe wenye exposure zao huwa wanasubiri mnainuka wote. Kuna ambao hawajui watendalo wanahitaji kuambiwa ila kuna ambao wanafanya makusudi. Waelewa huwa wanaomba samahani alafu ana reply sms
 
Hahaha au kama vipi na wewe watoa ya kwako...

Kwanini usiinuke, huyo hajakuheshimu hata kidogo au you're too boring. Mimi siwezi, naondokaga hata kama namuheshimu labda ni mkubwa, ni kheri kumwambia nitarudi baada when you're free
 
Hii tabia kweli inakera! mi natafsiri jama ni dharau maana kungelikuwepo na heshima wasingelifanya wanachofanya
 
Ukiona hivyo mazee piga chini usirudi tena huyo mtoto hana good manners msije mkafika mbali atakuja kufanya hayo matendo mbele ya wakwe zake halafu utaingia aibu wewe.
 
Bora umelisema hili, but mtu kama huyu me huwa napotezea on the sports kwa sababu huwezi kuwa bize wakati mimi niliye wa muhimu kwako hujanijali, kwangu ni tafsiri ya dharau..............
 
Back
Top Bottom