Hii taarifa nimeikuta katika media 2 solution. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii taarifa nimeikuta katika media 2 solution.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kingfish, Apr 19, 2012.

 1. kingfish

  kingfish JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [h=1]KWELI CHADEMA WANAPENDWA HIVI AU MACHO YANGU!?[/h] [​IMG]KWELI CHADEMA WANAPENDWA HIVI AU MACHO YANGU!?

  Imetokea 04/18/2012 kwenye Dala dala la Kutoka Airport kwenda Buhongwa (MWANZA), Kama kawaida ya konda ndani ya dala dala anadai nauli, kabla hajamaliza kudai nauli gari likakata mafuata (likawa linazimika zimika), ikabidi dereva aingie sheli kuongeza mafuta. Hatujajua kinachoendelea akainuka mama mmoja kwa hasira na kumfokea konda na dereva, akisema “Mambo ya kutembea na Mafuta ya vidumu mnatuchelewesha kwenye vikao na ntaenda kupigwa faini kwa kuchelewa Tsh. 5,000/=” Mara jirani yake akahoji, Kikao cha nini? Mama akajibu Kikao cha chama, kwa mshangao wa wengi, kila mmoja alidhani labda kikao cha wakinamama au SACCOS: Mama akaendelea kulalama ” Tena kwenye kikao cha chama cha CHADEMA!” Nkiwa bado nashangaa abiria wakasema nisicho kitarajia, “Kama ni kikao cha CHADEMA, tutakuchangia iyo faini”, nilidhani kama utani! Kwanza yule konda akamwambia yule mama: wewe ni mjanja, akamrudishia nauli yake, Konda akajipa kazi ya kuanza kukusanya michango kwa ajili ya yule mama. Amini usiamini mchango uliyo kusanya ulifikia Tsh. 32,500/=. Chakushangaza zaidi hata watoto wa shule walimchangia yule mama. hadi nashuka ndani ya Dala dala hilo bado nilikuwa na maswali mengi ya kujiuliza? Lakini kubwa ni je CCM wanajuwa hii inamaana gani? Naanza kuhisi mabadiliko, tena kabla ya 2015 ….
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  imetoka jf
   
 3. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 326
  Trophy Points: 180
  Tulishaipata hapa toka jana.
   
 4. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  CHA MSING taarifa
  imetoka wap si issue saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana
   
 5. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kwani humu ni wap? CHADEMA INAPENDWA KWELI.
   
 6. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mimi ndio naipata leo, si mbaya!
   
 7. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #7
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hiin ame-copy na ku-paste toka JF. Ni vizuri akasambaza taarifa, ila Inabidi a-dedicate source alipoitoa.
   
 8. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #8
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  unataka taarifa au dedication?
  Kama uliipata jana wengine wanaisubiri kesho.
   
 9. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nina shaka na ukweli wa habari hii.
  Watu kwenye daladala wachange 32,000?
  Jaribu tena baadae
  OTIS
   
 10. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #10
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ni utaratibu tu wa kusambaza taarifa, hata BBC wali indicate source za picha walizotoa JF. Na sisi members huwa tuna indicate taarifa tunazozitoa kwenye magazeti kabla ya kuzijadili. Hii inasaidia pia kusambaza vyanzo vya habari (kuna watu bado hawaijui JF), na pia inaonyesha authentification of the news.
   
Loading...