Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,272
Kupata kiwanja cha kujenga nyumba hasa katika prime area ni changamoto kubwa kwa sisi tunao safiri kuelekea uchumi wa kati. Unakuta pango la mwezi unapokaa ni 350, 000, ukipiga hesabu kwa miaka miwili unaona ni kheri ujenge ya kwako.
Umepata kiwanja kwa milioni 20. Bahati nzuri ulikua na akiba ya milioni 5, benki wakakupa milioni 20 mkopo. Rafiki zangu wengi walichofanya ni kujenga nyumba ya kujistiri nyuma ya kiwanja. Ina basic needs tu na kuhamia.
Mbele ya kiwanja anaweka banda la kuku hawa wa kienyeji na matuta manne ya mchicha. Hapo amepiga mahesabu ya kurudisha mkopo. Watoto wakilalamika wamechoka kula mchicha wanapozwa na kuku. Maharage ndiyo kubadilisha menu.