Hii Siri ni ya nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii Siri ni ya nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Jun 8, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Wana JF
  Usiri umewaumiza Watanzania kuanzia wakati serikali ilipotia saini kuingiza IPTL huku ikijua athari zake. Baadaye viongozi walewale waliingiza kitapeli na kuipa mkataba kampuni ya Richmond
  Bila aibu viongozi haohao wakaingiza kitapeli Dowans

  na sasa inakubali wananchi wazuiwe kupata habari juu ya Symbion Power kuhusu dili la mitambo ya Dowans na inavyohaha kuhuisha mkataba wa kuzalisha umeme ambao utauzwa kwa Watanzania.

  Lakini wana JF Tukumbuke kuwa Chama cha Wafanyabiashara (TCIA) kilitangaza kununua mitambo hiyo ili wafanye biashara na TANESCO. Mpango huo ukakwama,Baada ya mda mfupi kampuni ya Symbion Power ikajitokeza kusema imenunua mitambo hiyo na haraka, serikali inatangaza kuisaidia iwashe mitambo izalishe umeme.


  Maswali yanakuja na ni lazima tujiulize tukiwe kama watanzania wenye akili timamu na tunaipenda Tanzania yetu

  1.kwanini Symbion Power inaficha habari juu ya gharama walizotumia kununua mitambo hiyo?

  2.Ni kwanini Tanesco imeingia mkataba wa kununua UMEME na hii kampuni bila kuitisha zabuni?

  hivi hii siri ni ya nini? Hivi viongozi wetu wanafanya haya ili kutukomoa kwa kuwa tumewachaguwa ama hawaoni na hawatambui nini kinaendelea?

  Hivi Symbion ikijafanya madudu kama ilivyo tokea kwa kampuni zilizopita,je serikali itakuwa na la kutueleza?

  karibuni wadau

  please Faizafoxy naomba hii thread usichangie kwani wewe kila kitu kwako ni sawa huoni kama kunatatizo ama la,
   
 2. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Mwenyewe Faiza ni tatizo tayari!
   
 3. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ndio Tanzania hiyo! Natumaini wabunge wataona haya live...
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  waone kivipi?wakati hata kamati ya nishati wanasema wapewe ushirikiano wawashe mitambo chap chap! dowans sagga part 2,hawa wakati wa kuwalipa ndo watatu-restisha in peace!

   
 5. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #5
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  kwa hawa wamarekani tumeingia choo cha kike,tukishindwa kuwalipa ni lazima watatulipuwa kwa mambomu,wakidai wanalinda raia

  nadhani ndio maana hata serikali imeamuwa kuingia mkataba haraka kwa kuiogopa marekani

  huu utumwa sijui utaisha lini
   
Loading...