Hii sasa Imezidi: Dr. Kitila Mkumbo kupandishwa kizimbani kwa Uchochezi!

Msomi mzima hana akili, naye anasimama kwenye jukwaa tena nyumbani kwao anachochea vijana wake wa kazi kuuwa. Kwa nini hao akina Mbowe hatusikii wakiuawa huko kwao?

Sio bure utakuwa umetumwa na Mwigulu.
 
Katika kile kinachoonekana ni vita sasa kati ya serikali na CDM jeshi la polisi nchini limeamua kumfungulia mashtaka mhadhiri wa chuo kikuu cha DSM na mjumbe wa Kamati kuu CDM Dr Kitila Mkumbo kwa kile wanachodai ni uchochezi wake aliofanya siku alipohutubia mkutano katika kata ya Ndago jimbo la Iramba Magharibi.

Wachunguzi wa mambo wanadai mbunge wa jimbo hilo Mwigulu Nchemba ameapa kutumia kila njia kumzuia Dr Kitila Mkumbo asipate nafasi ya kugombea katika jimbo hilo hasa kutokana na kuwa Dr Kitila ni chaguo la wanaIramba wengi na ana heshima kubwa huki kwao hasa kutokana na hekima na busara zake anapozungumza.

Source: ITV (Dondoo za gazeti la Nipashe la Ijumaa)


------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Soma habari yenyewe ndani ya NIPASHE:

Kiongozi mwingine wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amehojiwa na Polisi juu ya vurugu zilizotokea katika mkutano wa chama hicho na kusababisha Mwenyekiti UVCCM Kata Ndago, wilayani Iramba, Mkoani Singida, Yohana Mpinga kupoteza maisha.

Aliyehojiwa na kuachiwa kwa dhamana ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), Mkumbo Kitila na alitakiwa kurejea Polisi leo asubuhi, kwa ajili ya kupelekwa mahakamani.

Kamanda wa Polisi Mkoa Singida, Linus Sinzumwa, alisema jana kuwa Kitilah atapandishwa kizimbani kwa kosa la kutoa lugha ya matusi kwenye mkutano wa hadhara, uliofanyika Jumamosi iliyopita.

“Kitila tumehoji na yupo nje kwa dhamana na tunatarajia kumfikisha kesho (leo) mahakamani…anakabiliwa na tuhuma hizo hizo za kutoa lugha ya matusi,” alisema Sinzumwa.

Juzi jeshi hilo lilimhoji mkurugenzi Habari na Uenezi wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo John Mnyika kwa saa tatu, kuanzia saa 12 jioni, kabla ya kumwachia huru.

Kuhusu kuhojiwa kwa Mnyika, Kamanda Sinzumwa alisema aliachiwa huru baada ya kuridhika na maelezo yake, lakini wakimhitaji watamwita tena, kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Kiongozi wa kwanza kuhojiwa kuhusiana na vurugu hizo alikuwa Ofisa Sera na Uratibu wa Chadema, Mwita Waitara, ambaye ameshafikishwa mahakamani kwa kosa la kutoa lugha ya matusi dhidi ya Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba.

Kutokana na hali hiyo, Kitila ataunganishwa katika kesi hiyo, kuhusiana na vurugu zilizotokea Mkutano wa Chadema uliofanyika Ndago, Iramba Mkoani Singida.

Mandela alishasema..." Kwa Tawala zetu hizi, lazima upate makesi au hata kufungwa, ukishatoka ndio unakuwa kiongozi imara"
Hawa CCM wanatafuta kuzuia harakati za kulikomboa taifa na ujima wao lakini kamwe, nchi hii itaongozwa na 'wenye utashi' na sio muflis kama ilivyo sasa. Akina Mkumbo ni hazina, hata wakifungwa, taifa linawatambua kuliko hata walio madarakani! Mtashangaa jinsi kesi hizo zitakavyofurika watu. Watawala watakuwa wanapata tena shida ya kupeleka FFU kila siku esi itakapotajwa! This is a misuse of resources for a shameful output!! We all see!
 
Ninashangaa! Ninashangaa! Waliotukanwa hawajalalamika, sasa hawa wanapata wapi ujasiri wa kuwafungulia mashtaka hawa kina Kitila? Au wanataka kufanya changa kama lile la Lema.
 
sijawahi kusikia mtu amepatikana na hatia katika kesi ya uchochezi! ni kupotezeana muda na kupeana stess tu!
Acha! Hapa WANAMPANDISHA CHATI Dkt Mkumbo. Hapo penye RED, Kitila huwezi kumpa STRESS. Yeye ni Mwanasaikolojia ANAYEWASAIDIA wengine KUONDOA stress. Ni kama kumpeleka Chura majini!
 
Inaelekea ,watawala na vibaraka wao wamepania kuratibu vitendo vinavyolenga kutusononesha na kutufedhehesha sisi wana mabadiliko.
Kwa kuwa tangu kitambo tumechagua kuwa mwitikio wetu,daima ni kukataa kusononeshwa na kufedheheshwa ,kwa hiyo,ingefaa waelewe wazi kuwa mpango wao huo hautafanikiwa..Sisi tupo imara.Tunaamini kabisa, baada ya tukio hili tutaibuka tukiwa imara zaidi.
Yawezekana Mungu ameruhusu haya yatokee ili kumuimarisha zaidi Dkt.Kitila tayari kuwatumikia wananchi wa Iramba Magharibi mwaka 2015.
Fikra huru hazijui wala hazitambui wingi wala aina ya mashtaka na matokeo yake.
Hata Mandela alipata kufunguliwa kesi ya uchochezi.
Hatuna haja ya kuogopa wala kutetereka.Kama alivyopata kutuasa Dkt Kitila tunapaswa "kuogopa kuogopa".
Wana mabadiliko,popote pale tulipo tuwaombee makamanda wetu wakati huu wanapokabiliana na mahakama ili Mungu awape moyo wa ustahimilivu.
 
Huyu Kitila si ndio juzi tu amehongwa cheo na CCM kwa kuwa mkuu wa kitivo ? au Kitila yupi usemae ww ?


Mkuu Dumela la Mbegu,yaelekea hujui vigezo vinavyotumika kuwapa wanataaluma nafasi za uongozi katika Taasisi nyeti kama UDSM.Moja ya vigezo ni uwezo wa kitaaluma, uchapa kazi na ushirikiano na wana taaluma wenzako katika Idara husika.Hakuna kujuana kama huko CCM!!
Mingependa uelewe kuwa Dokta pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiaya ya Wanataaluma wa UDSM.Kwa mtazamo wako utadai kahongwa!!
 
Jamani watanganyika na CDM wenzangu 2015 tusitegemee tena kushinda kwa kutumia ballot box kwani CCM haijajiandaa kuwa wapinzani na kutoka madarakani bali tunatakiwa tuwe na commited mind then tujiandae tu kufanya maandamano makubwa yasiyo na kikomo kama misri na liwalo na liwe kwani dalili zinajionesha kuwa kamwe CCM haiwezi kuachia madaraka hivi hivi.

"Peacefuly if we may, Forcely if we must"
 
Bado nafikiria sana (na siyo kuwaza) kwamba ivi Mnyika Angeuawa pale ingekuaje??? CCM wanakubali viongozi wao wengine wa iharibu nchi hivihivi mchana kweupe.
 
Wadau,
waache hawa ma chcm waendelee kuwanyanyasa majembe/makamanda na hii itaongeza chuki dhidi yao kwa wananchi na wapiga kura kwa ujumla.
Cha kufanya kwa sasa ikitoke tume ina ina uhusha/update daftari la mpiga kura kila mmoja ajiandikishe na atunze kadi yake najuwa mwajua cha kufanya 2015.
 
Pro-Chadema JF wengi ni watupu kwenye mambo ya kisheria kwa kweli mtu makini na msomi kama Dr Kitila Mkumbo kauli aliyetoa imenisikitisha sana...Julai 14 mwaka huu saa 10.00 jioni, mshatakiwa Dr Mkumbo alitoa lugha ya matusi dhidi ya mbunge wa Iramba Magharibi.

Dr Mkumbo alitamka kuwa mbunge huyo ni malaya, mzinzi, na ni 'the comedy' alitoa lugha hiyo kwenye mkutano wa hadhara wa Chadema...

Acheni ushabiki na kufuata mkumbo hata kama mnampenda Dr Kitila Mkumbo kubalini kuwa ameteleza.
 
Back
Top Bottom