Hii sasa Imezidi: Dr. Kitila Mkumbo kupandishwa kizimbani kwa Uchochezi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii sasa Imezidi: Dr. Kitila Mkumbo kupandishwa kizimbani kwa Uchochezi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Jul 19, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Katika kile kinachoonekana ni vita sasa kati ya serikali na CDM jeshi la polisi nchini limeamua kumfungulia mashtaka mhadhiri wa chuo kikuu cha DSM na mjumbe wa Kamati kuu CDM Dr Kitila Mkumbo kwa kile wanachodai ni uchochezi wake aliofanya siku alipohutubia mkutano katika kata ya Ndago jimbo la Iramba Magharibi.

  Wachunguzi wa mambo wanadai mbunge wa jimbo hilo Mwigulu Nchemba ameapa kutumia kila njia kumzuia Dr Kitila Mkumbo asipate nafasi ya kugombea katika jimbo hilo hasa kutokana na kuwa Dr Kitila ni chaguo la wanaIramba wengi na ana heshima kubwa huki kwao hasa kutokana na hekima na busara zake anapozungumza.

  Source: ITV (Dondoo za gazeti la Nipashe la Ijumaa)


  ------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
  Soma habari yenyewe ndani ya NIPASHE:

  Kiongozi mwingine wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amehojiwa na Polisi juu ya vurugu zilizotokea katika mkutano wa chama hicho na kusababisha Mwenyekiti UVCCM Kata Ndago, wilayani Iramba, Mkoani Singida, Yohana Mpinga kupoteza maisha.

  Aliyehojiwa na kuachiwa kwa dhamana ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), Mkumbo Kitila na alitakiwa kurejea Polisi leo asubuhi, kwa ajili ya kupelekwa mahakamani.

  Kamanda wa Polisi Mkoa Singida, Linus Sinzumwa, alisema jana kuwa Kitilah atapandishwa kizimbani kwa kosa la kutoa lugha ya matusi kwenye mkutano wa hadhara, uliofanyika Jumamosi iliyopita.

  "Kitila tumehoji na yupo nje kwa dhamana na tunatarajia kumfikisha kesho (leo) mahakamani…anakabiliwa na tuhuma hizo hizo za kutoa lugha ya matusi," alisema Sinzumwa.

  Juzi jeshi hilo lilimhoji mkurugenzi Habari na Uenezi wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo John Mnyika kwa saa tatu, kuanzia saa 12 jioni, kabla ya kumwachia huru.

  Kuhusu kuhojiwa kwa Mnyika, Kamanda Sinzumwa alisema aliachiwa huru baada ya kuridhika na maelezo yake, lakini wakimhitaji watamwita tena, kwa ajili ya mahojiano zaidi.

  Kiongozi wa kwanza kuhojiwa kuhusiana na vurugu hizo alikuwa Ofisa Sera na Uratibu wa Chadema, Mwita Waitara, ambaye ameshafikishwa mahakamani kwa kosa la kutoa lugha ya matusi dhidi ya Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba.

  Kutokana na hali hiyo, Kitila ataunganishwa katika kesi hiyo, kuhusiana na vurugu zilizotokea Mkutano wa Chadema uliofanyika Ndago, Iramba Mkoani Singida.
   
 2. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ccm imeoza; inanuka!!!!!!!!!!
   
 3. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Msomi mzima hana akili, naye anasimama kwenye jukwaa tena nyumbani kwao anachochea vijana wake wa kazi kuuwa. Kwa nini hao akina Mbowe hatusikii wakiuawa huko kwao?
   
 4. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hizi mbinu chafu zinaashiria kuwa tusitegemee jipya kwenye KATIBA mpya. Kwanini watu wanang'ang'ania madaraka hata kwa damu ya wanaowaongoza?
   
 5. only83

  only83 JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Hivi unaweza fananisha uwezo wa juu wa kujenga hoja na kufikiri wa Dr Mkumbo na huyu chemba? Hata afanyaje jimbo la Iramba ni la CHADEMA mwaka 2015. Wanadhani kumfungulia mashitaka ndio kuafifisha spidi yetu? Hawajui kuwa haya yote ndio yanatupa nguvu kusonga mbele.
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  hawawezi zuia moto, moshi ushaanza kufuka mwigulu wewe ni dada tuu mbele ya CM
   
 7. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  sijawahi kusikia mtu amepatikana na hatia katika kesi ya uchochezi! ni kupotezeana muda na kupeana stess tu!
  polisi ni washenzi sana.
   
 8. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mimi nilikuwepo kwenye mkutano. Dr hakufanya uchochezi wowote.
   
 9. Collins

  Collins Senior Member

  #9
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wanajisumbua tu 2015 CDM mjengoni
   
 10. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  uzuri chadema wana mkanda wa video na watauonyesha mahakamani hata kama mahakama ni ya ccm.
   
 11. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  CCM wanafikiri kutapatapa kwao kutawaepusha na kifo chao 2015.
   
 12. k

  kula kwa tindo JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,330
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  ***** wewee.. Lusinde katoa lugha chafu hukuona.. huyu hujackia unafunga kibwebwe..!!!Bungeni CDM wanaambiwa wanawashwa. Husemi kama ni lugha ya kuudhi Bungeni kwa kua ni CCM.Hata karipio hakupewa..Sasa kwa taarifa yako na yenu.. Raia Milion 35 hawakupiga kura.. Na tambua JKamechaguliwa na Tume na hilo kundi ndilo linaitaka TANGANYIKA YAO!!hata mkamate mamia lakini MTAONDOKA TU NA OKAMPO MTAMJUA!!
   
 13. Electron

  Electron Member

  #13
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acha wazidi kumpaisha...
  Hebu wanasheria nisaidieni, si tayari kuna kesi kuhusiana na hili tifu la Ndago na kuna wengine wameshafikishwa kotini? kwa nini wamfungulie kesi tofauti na mashitaka yake na wasimjumuishe..... au ndio character assassination????
   
 14. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ningekuwa mi ndo hakimu,ningetoa hukumu kitila mkumbo apigwe miaka 300 na viboko ishirini,kumi wakati anaingia,kumi wakati anatoka akamwonyeshe mke wake.
   
 15. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  nikisikia jina la 'Mwigulu' napata kichefuchefu!
   
 16. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Naona nchemba ameamua kupigana na yeyote anayeonekana kujitokeza kushindana naye.Kwa jitihada hz anazofanya atahatarisha maisha ya yoyote anayejitokeza kumpinga na cdm wanatakiwa kujua kudeal naye wakikosa busara za kumdhibiti atawaharibia sana.magamba wanamulinda sana huyu mnyela
   
 17. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  huna adabu wewe
   
 18. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Inaelekea huyu jamaa (Mwigulu) atamwaga damu za watu wengi sana kabla hajaondolewa na uchaguzi wa 2015.
   
 19. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #19
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  ni maoni yako kwa akili yako ikipofikia kufikiri!ni heri kukosa mali kuliko kukosa akili
   
 20. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  chadema ndio mzoga kabisa,bado hata hamjaijua harufu ya magogoni mmeanza kuua?laana ya damu ya yohana itawatafuna,
   
Loading...