Hii Samsung Note 4 inapata moto balaa

Randy orton

JF-Expert Member
Apr 29, 2019
1,338
3,539
Nimebadilisha battery mara 2, lakini bado inapata moto hatari, japokuwa siitumii sana ila nikiiwasha tu inapata moto mno. Nimeweka apps kama Wake Lock nk lakini bado tu, tusaidiane wakuu.
 
Nahisi tatizo ni AC. Kwakua unasema umebadili battery mara mbili hapo shida kwa ninavyoona mimi ni AC.

Sikumbuki vizuri kama AC inatengenezeka, baadaye itakua ni bora usiwashe data, usiplay miziki au muvi wala usipige picha au kuchukua shooting.
 
Hizo battery unazobadirisha zina meet requirements za simu yako ?
Charge unayotumia inameet requirements za simu yako ?
Inapata motot wakati gani ?
Ukiwa umewasha data na screen ipo on ?
Ukilock na ikiwa inafanya kazi katika idle state huwa inapata moto ?
Unafikiri ni kwanini ilianza kupata moto
Na kwanini ulibadirisha battery ?
 
Nimebadilisha battery mara 2, lakini bado inapata moto hatari, japokuwa siitumii sana ila nikiiwasha tu inapata moto mno. Nimeweka apps kama Wake Lock nk lakini bado tu, tusaidiane wakuu.
Note 4 Samsung walichemka sana upande wa betri, simu inapata sana moto ukiwasha data. Tena bora ununue hizi betri za kichina wanazouza machinga kuliko kununua battery zao OG zinasumbua kinyama.

Nilinunua mpya 2017 nikatumia nikaona sielewi nikanunua battery mpya ugonjwa ukabaki pale pale, nikaingia mtandaoni nikasoma reviews za watu nikagundua niliingia chaka.

Nilitafuta jamaa mmoja akanipa hela nikamuachia hayo matatizo hata sijui bado anayo au ilishakufa.
 
Back
Top Bottom