Hii Picha Ya Nassari.

Steven Sambali

JF-Expert Member
Jul 31, 2008
352
170
Huyu kijana, kama atawasahau watu wake wa Arumeru Mashariki basi ajiandae kwa laana mbaya sana. Hizi baraka alizopewa za kutoka Moyoni haswa na akizitumia vibaya, zitamuharibu na kumpeleka pabaya zaidi ya watu waliokufa kwa kubugia unga. Anaweza kupata hela nyingi kama Whitney Houston ila akaishia kufia kwa kuzama kwenye bafu (Washing tab).

Kijana, kuwa mwangalifu sana na hizi BARAKA za wazee maana zinaweza kukugeuka.

Kila la kheri na fanaka kwenye kazi yako mpya na Mungu awe nawe.

Mungu Ibariki Tanzania.


Chadema.jpg


 
Last edited by a moderator:
Nimefurahi kusoma kuwa kashaanza kazi ya kuweke visima huko Arumeru Mashariki.

Kijana tunamuombea sana maana kushindwa kwake itakuwa ni pigo sana kwa Wananchi waliomuamini.

Asisahau tu maneno yake mwenyewe kuwa "wamemchagua masikini mwenzao....."
 
hatuna mashaka na kijana ameonyesha nia ya kutekeleza majukumu yake hata kabla hajaapishwa
 
Mbona ndugu yangu umeandika kisharishari? hukumbuki hata maaskofu walisema Kikwete ni chaguo la Mungu na matokeo yake ndio tunayaona? usimtie majaribuni kijana wa watu, hata Nape alisema Nasari atimize ahadi huku aisahau kwamba CCM haijatimiza hata moja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom