Hii njia ni sahihi kujua ukubwa wa eneo kwa heka?

Bakulutu

JF-Expert Member
Nov 30, 2011
2,544
1,760
Hivi nikitaka kujua ukubwa wa eneo fulani kwa HEKA ambalo sio mraba au mstatili (eneo halina umbo mahalumu) ninafanyaje? Nilipata hii changamoto kidogo ila niliamua kupima mzunguko wake wote kwa mita (mzingo) labda nikapata mita 120 nikafanya ulinganifu kwa heka1 ina mzunguko wa 280m je 120m ni heka ngapi? Nilikuwa sahihi au kuna njia nyingine?
 
Kwahesabu hiyo inamaana nusu inatakiwa iwe na mzingo wa 140 kwahiyo hiyo 120 ni nusu kasoro miguu 20
 
Sasa mkuu ukisema nusu heka ni 140 sio ukweli mana nusu heka ni 70x35 ambayo ni 70+35+70+ 35 = 210 tatizo hapa
 
Hahaa hili kweli ni tatizo nasijawahi kuling'amua hili kabla hebu watalamu wa mahesabu waje watupe jibu hapa inakuaje mzingo wa ekari moja 70+70+70+70=280 lkn nusu yake ambayo ni 70+35+70+35=210
How.?
 
Huwezi pata ukubwa wa eneo utaenda chaka vibaya mno.

Lets say ekari ni 70 kwa 70 meters mzingo 70+70+70+70=280
A=70×70=4900
Oky tupunguze meters 35 za upande mmoja tuongeze kwenye upande mwingine iwe 105 kwa 35 mzingo 105+105+35+35=280
A=105×35=3675
Unaona sasa maeneo mawili yenye mzingo sawa but ukubwa wa eneo unatofautiana

Chakufanya hilo eneo mlipime kwa kulikata vipande vipande
Kateni eneo kubwa la mraba, kisha vipande vinavyobakia hata kama ni pembe tatu pimeni hivyo hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi nikitaka kujua ukubwa wa eneo fulani kwa HEKA ambalo sio mraba au mstatili (eneo halina umbo mahalumu) ninafanyaje? Nilipata hii changamoto kidogo ila niliamua kupima mzunguko wake wote kwa mita (mzingo) labda nikapata mita 120 nikafanya ulinganifu kwa heka1 ina mzunguko wa 280m je 120m ni heka ngapi? Nilikuwa sahihi au kuna njia nyingine?
Mkuu ngoja nikupe elimu kidogo, hela moja siyo 280m mizunguko, na Wala siyo mita za mraba 4900, na Wala siyo 70m*70m. Mita moja Ni mita za mraba 4046.86 hivyo Ni pungufu ya 70*70, pia Ni pungufu ya 280m kwa mizunguko au mzingo. GPS machine ndiyo upima sahihi, wanatumia Sana wapima ardhi (land surveyors)
 
Hahaa hili kweli ni tatizo nasijawahi kuling'amua hili kabla hebu watalamu wa mahesabu waje watupe jibu hapa inakuaje mzingo wa ekari moja 70+70+70+70=280 lkn nusu yake ambayo ni 70+35+70+35=210
How.?
Hesabu ni ugonjwa wa taifa
 
Kwahesabu hiyo inamaana nusu inatakiwa iwe na mzingo wa 140 kwahiyo hiyo 120 ni nusu kasoro miguu 20
Mwenzio ametumia mita sio miguuu, elewa somo, alafu mita na miguuu ni tofauti naa hatua ya mguu huendana na ulefu wa mtu .
 
Hivi nikitaka kujua ukubwa wa eneo fulani kwa HEKA ambalo sio mraba au mstatili (eneo halina umbo mahalumu) ninafanyaje? Nilipata hii changamoto kidogo ila niliamua kupima mzunguko wake wote kwa mita (mzingo) labda nikapata mita 120 nikafanya ulinganifu kwa heka1 ina mzunguko wa 280m je 120m ni heka ngapi? Nilikuwa sahihi au kuna njia nyingine?
Njia rahisi ni kutumia GPS:-
1) Nenda ofisi ya Halmashauri kitengo cha Ardhi uongee na mpimaji.
2) Mpeleke saiti akupimie/achukue Co-ordinates kwa kufuata maeneo ya mpaka kama utakavyomuonesha.
3) Kwa kukumia vipimo alivyochukua, atakuchorea Site Map na kukupa ukubwa wa eneo husika. Hii itakusaidia kukupa mwangaza kwa ajili
ya mipango uliyonayo na hatua zaidi.

Mfano wa kifaa wanachotumia kuchukua Co-ordinates nia kama hiki hapa 👇👇👇

GPSMAP 64s.jpg
 
Hivi nikitaka kujua ukubwa wa eneo fulani kwa HEKA ambalo sio mraba au mstatili (eneo halina umbo mahalumu) ninafanyaje? Nilipata hii changamoto kidogo ila niliamua kupima mzunguko wake wote kwa mita (mzingo) labda nikapata mita 120 nikafanya ulinganifu kwa heka1 ina mzunguko wa 280m je 120m ni heka ngapi? Nilikuwa sahihi au kuna njia nyingine?
  1. Divide the circumference by π.
  2. Divide the result by 2 to get the circle's radius.
  3. Multiply the radius by itself to get its square.
  4. Multiply the square by π, or 3.14 for an estimation.
  5. You found the plot's area from the circumference and it is an approximation.
 
Manually
 
Back
Top Bottom