Hii ni tabia mbaya sana khaa!

Hii ni tabia mbaya sana khaa!

LUBEDE

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
4,322
Reaction score
6,700
Leo kuna sehemu nimeamkia,yaani kuna jirani nyumba ya pili anasafisha kinywa kama anataka kufa,hayo makohozi anavyoyavuta na kujikoholesha,utadhani alikula kinyesi,yaani mtu mmoja anasafisha kinywa ila makelele yake ni kero hadi huku kwa jirani,namuuliza mwenyeji wangu anasema washamzoea,ningekuwa naishi hapa wallah ningemfuata huyu jamaa,yaani amenichefua sana asubuhi hii,huko pande zenu vipi,hamkutani na kadhia hizi?
Huu ni uswahili uliopitiliza,utadhani amejifunzia ukubwani kusafisha kinywa daah!
 
Kawaida sana kwa uswazi ukitaka uishi utakavyo wewe jenga nyumba yako uishi peke yako
 
Hawa itakuwa ni wale watu wenye tabia ya kusafisha ulimi wakati wanapiga mswaki,sasa inapotokea mswaki umeelekea kooni hali ya kutapika inamjia kwahiyo lazima utamsikia anafanya kitu kama kuvuta makohozi,hata mimi hii tabia huwa siipendi sana...
 
Tikiwaambia mje mashambani huku muishi nyie mnang'ang'ania Mbagala Kuu. Huku kwetu sauti pekee unayoisikia asubuhi ni jogoo kuwika.

Poleni sana kwa makohozi
Hata huko mashambani ni balaa, asikwambie mtu.

Siku moja nilitembelea mkoa, babu yangu amepanda miembe shambani kwake na mimi ninapenda sana hayo matunda.

Kipindi hicho ndiyo ulikuwa msimu wake na mchana nikawa nimepanda mwembeni bila kelele nikila matunda kimyakinya kwa utulivu mkubwa, bila kelele wala sauti.

Baadaye kidogo nikasikia sauti ya baiskeli, kisha mtu akapaki akaja moja kwa moja kujibanza na kuchuchumaa kwenye shina la mti niliopanda bila ya kuangalia juu, kisha akafungua mkanda na kuanza kujisaidia haja kubwa!

Kitendo hicho kilinikera na kuniharibia 'mood' kwa sababu alikuwa akinyea sehemu niliyopandia.
Lakini pia alinivuta hisia za cheko zangu kwa jinsi madoido yake aliyokuwa akiyafanya wakati wa tendo hilo.
Alianza kwa kukenua meno na kutoa sauti yenye kujirudiarudia...' Enhnhenhenhenhenheneeeee' huku katoa jicho mkoma, katepesha midomo na kushindwa kujikontroo.
Tendo hilo likanifanya nicheke kwa kujibana!
Lahaula! Huyo mzee akashituka, kama mtu anayekatishwa usingizini ghafla!
Akavuta suruali juu bila ya kuchamba na kuanza kuangalia juu huku akijifunga mkanda na aliponiona akanitambua na kuanza kuniporomishea matusi.
Aliendeleaa kulalamika na kutoa lawama nzito kwamba kwanini nilimwacha ajisaidie bila hata kumshitua kwa kujikohoza?
Mashitaka hayo aliyapeleka hadi kwa babu kunikandamiza kuwa mimi ni mtovu wa nidhamu niliyekubuhu.
Wakati yeye kosa lake la uchafuzi wa mazingira kwenye shamba la mtu kaliweka pembeni!

Kesi ile babu yangu aliimaliza kiutu uzima.
Uone kwamba hakuna mahali panapoishi binadamu pakakosa vituko. Iwe mjini ama vijijini, pote ni vurugu tupu.
 
Kuna kale ka wimbo ka...... Uswahilini kuna vituko
 
Tikiwaambia mje mashambani huku muishi nyie mnang'ang'ania Mbagala Kuu. Huku kwetu sauti pekee unayoisikia asubuhi ni jogoo kuwika.

Poleni sana kwa makohozi
Tatizo sio kuja Asprin, tatizo kianzio cha maisha huko shamba ndio tatizo.
 
Kuna dada alikua anafanya hivyo Kwenye dirisha la chumban
Kama muijuavyo tandale...
Siku nikaamua tu kuweka porn nikamaximize volume nikaweka simu dirishani
Toka hapo sijawahi kumsikia tena
 
Hata huko mashambani ni balaa, asikwambie mtu.

Siku moja nilitembelea mkoa, babu yangu amepanda miembe shambani kwake na mimi ninapenda sana hayo matunda.

Kipindi hicho ndiyo ulikuwa msimu wake na mchana nikawa nimepanda mwembeni bila kelele nikila matunda kimyakinya kwa utulivu mkubwa, bila kelele wala sauti.

Baadaye kidogo nikasikia sauti ya baiskeli, kisha mtu akapaki akaja moja kwa moja kujibanza na kuchuchumaa kwenye shina la mti niliopanda bila ya kuangalia juu, kisha akafungua mkanda na kuanza kujisaidia haja kubwa!

Kitendo hicho kilinikera na kuniharibia 'mood' kwa sababu alikuwa akinyea sehemu niliyopandia.
Lakini pia alinivuta hisia za cheko zangu kwa jinsi madoido yake aliyokuwa akiyafanya wakati wa tendo hilo.
Alianza kwa kukenua meno na kutoa sauti yenye kujirudiarudia...' Enhnhenhenhenhenheneeeee' huku katoa jicho mkoma, katepesha midomo na kushindwa kujikontroo.
Tendo hilo likanifanya nicheke kwa kujibana!
Lahaula! Huyo mzee akashituka, kama mtu anayekatishwa usingizini ghafla!
Akavuta suruali juu bila ya kuchamba na kuanza kuangalia juu huku akijifunga mkanda na aliponiona akanitambua na kuanza kuniporomishea matusi.
Aliendeleaa kulalamika na kutoa lawama nzito kwamba kwanini nilimwacha ajisaidie bila hata kumshitua kwa kujikohoza?
Mashitaka hayo aliyapeleka hadi kwa babu kunikandamiza kuwa mimi ni mtovu wa nidhamu niliyekubuhu.
Wakati yeye kosa lake la uchafuzi wa mazingira kwenye shamba la mtu kaliweka pembeni!

Kesi ile babu yangu aliimaliza kiutu uzima.
Uone kwamba hakuna mahali panapoishi binadamu pakakosa vituko. Iwe mjini ama vijijini, pote ni vurugu tupu.
Huko lazima kutakuwa usukumani mkuu. Mashambani kwetu tumezungusha ukuta, mtu akijifanya kuruka atasemezana na madogi LOL
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom