Hii ni sayansi ya aina gani na nini kinasababisha jambo hili?

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,730
10,033
Naweza kusema labda wengi mmewahi kukutana na hali fulani hivi ambayo inastaajabisha kidogo. Je, kuna yeyote anajua nini kisababishi na inakuwaje? anaweza kuelezea kidogo?

HALI HIYO IKO VIPI?
1- Kwa maelezo mafupi ni hivi. Kuna muda unaweza kuwa upo katika mishe zako za kila siku kupambana na hali yako kimaisha, lakini unajikuta ghafla tu ukiwa unamuwaza mtu fulani ambaye mnajuana vizuri kabisa na kwa upande mwingine huyo mtu unaemuwaza naye anakuwaza kisha kila mmoja anajikuta akifanya juhudi kumtafuta mwenzake wapate kuongea au kuonana kabisa.

2- Kuna wakati unakutana na mtu eneo fulapo mtu huyo ni mgeni kabisa machoni pako lakini cha ajabu zaidi inatokea kila mmoja akimfananisha mwenzake kama wamewahi kuonana mahali lakini *** jibu ni negative*** hakuna aliyewahi kumuona mwenzake!.

View attachment 1469833
 
Itakuwa aina ya sita ya hisia yaani telepathy igoogle ufafanuzi zaida. Pia utakuta watembea mwapishana na mtu alafu wote kwa pamoja mwageuka kutazamana.

Au mpo wawili au watatu mwatembea ukisimama kukujoa basi wote mwajikuta mwakojoa.

Wasema ni njia ya kuwsiliana zaidi ya zile njia kuu 5 za kunusa kugusa kuona kusikia kuonja.

Telepathy is the purported vicarious transmission of information from one person to another without using any known human sensory channels or physical interaction. The term was coined in 1882 by the classical scholar Frederic W. H.
 
Ya kwanza inaitwa kitaalamu telepathy...tafuta maelezo yake kwenye mtandao

Ya pili, inasemekana kila mtu hapa duniani aliwahi kuishi hapo kabla (reincarnation). So yawezekana wawili nyie mshaishi sehemu moja hapo kabla.
 
Hivi na hii ya kuona kama jambo Fulani limejirudia.Yani like kama unafanya jambo,au unawaza jambo unakuta unahisi ni marudio kichwani mwako.Ni hali gani hii?
 
Kuna hili la kumpokea mtu miayo, yani mfano umekaa na mtu halafu akapiga miayo basi akimaliza na wewe unajikuta pia unapiga miayo.
 
Naweza kusema labda wengi mmewahi kukutana na hali fulani hivi ambayo inastaajabisha kidogo. Je, kuna yeyote anajua nini kisababishi na inakuwaje? anaweza kuelezea kidogo?

HALI HIYO IKO VIPI?
1- Kwa maelezo mafupi ni hivi. Kuna muda unaweza kuwa upo katika mishe zako za kila siku kupambana na hali yako kimaisha, lakini unajikuta ghafla tu ukiwa unamuwaza mtu fulani ambaye mnajuana vizuri kabisa na kwa upande mwingine huyo mtu unaemuwaza naye anakuwaza kisha kila mmoja anajikuta akifanya juhudi kumtafuta mwenzake wapate kuongea au kuonana kabisa.

2- Kuna wakati unakutana na mtu eneo fulapo mtu huyo ni mgeni kabisa machoni pako lakini cha ajabu zaidi inatokea kila mmoja akimfananisha mwenzake kama wamewahi kuonana mahali lakini *** jibu ni negative*** hakuna aliyewahi kumuona mwenzake!.

View attachment 1469833
Coincidence!
Illusion..

Wala bangi ndo wanakuwaga na fikra za kindotondoto tu...

Mtu anajikuta yuko na demu mkali kumbe anapiga nyeto.

Illusionists...
Sawa ngoja nifuatilie
Theory's tu hizo hazina uhalisia,,
Simple...Coincidence
Binadamu tunatofautiana uwezo wetu wa kiroho. Kuna watu wana nguvu kubwa zaidi kiroho ya wengine. Nguvu ya kiroho ni suala la wewe mwenyewe kuikuza kuna kanuni zake na gharama zake pia ni kama ukitaka kuwa na misuli ya kutosha kuna kanuni zake na gharama zake.

Kwa hali ya kawaida tu kumwaza mtu mwingine kunaweza kukamuathiri mtu yule au hata kuathiri mawazo yake pia, inategemea nguvu ya kiroho uliyonayo na pia nguvu ya mtu husika. Kwa mfano mimi naweza kuwaathiri baadhi ya watu e.g. rafiki au ndugu wafanye jambo fulani na kweli utasikia wamefanya au wamepiga simu wakisema mambo yale yale "niliyoongea" nao bila wao kujua.

Kuna upeo wa juu zaidi wa kufanya hivyo ila na kanuni zake ni nyingine na "gharama" zake ni kubwa.

Kwa kifupi tu ni kwamba mambo mengi unayowaza yamesababishwa na mawazo ya watu wanaokuzunguka. Familia yako wana nguvu ya asili kubwa zaidi kwako kuliko mtu wa mbali asiyekujua.

Inaweza kuwa ngumu kwa wengi wenu kuelewa mambo haya kwani mnaishi zaidi kimwili kuliko kiroho, au ndio kusema mmekufa kiroho. Niishie hapa kwa sasa.
 
Absolutely correct our mysterious world has got its own codes!
Na naona dini moja imebase sana kwenye hayo mambo,Buddhism.
Kuna master mmoja hivi alikuwa na uwezo wa kufunga na kufunga mlango bila kuugusa!
 
Back
Top Bottom