Hii ni sala ya dhehebu gani???

Hii ni sala ya dhehebu gani???



Nilishawahi kuuliza ili swali humu humu JF, Ila sikupata jibu
Mkuu; kwa nini upate shida kwa matumizi ya neno washenzi (plural) au Mshenzi(singular)? Kumbuka lugha ya Kiswahili inakua na inaboreshwa kila mara.
Neno "mshenzi" ni asiye "mstaarabu". Mshenzi ni neno linalotumika kumwelezea mtu ambaye kwa matendo yake anamaudhi kwa watu wenzake/Jamii. Kwa mfano mtu anayetumia lugha ya maneno machafu, matusi, anayewasengenya/simanga wenzake na kuwadharau, kiburi, kutendea wenzake kwa ujeuri, kufitinisha na kufarakanisha watu, mdanganyifu, mwongo-mwongo, anayeonesha kwa makusudi mwenendo wa kibabe kwa wenzake n.k
Kwa definition hiyo(if and only if you agree); hiyo sala iliyokuwa inasaliwa na Wakatoliki(mm nikiwa mmojawapo)ililenga kuwaombea kwa Mungu watu wa aina hiyo waweze kutambua na kuona Ubaya huo wanaoutenda kwa wenzao na halafu kwa nia ya dhati wabadilike na waoneshe Upendo kwa wenzao walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Je, hilo halikuwa sahihi?
Hiyo sala Siku hizi haisaliwi tena (ime-xpire; out dated)na matumizi ya neno Washenzi limebaki na linachukuliwa kama ni neno linalomdhalilisha mtu au ni tusi au sifa iliyopitiliza. Kwa hiyo neno hilo hutumika kumtukana mtu au wakati mwingine kumsifia mtu e.g. hebu soma katika sentensi hii "Aisee! Wale jamaa wa Ukraine ni washenzi balaa. yaani wametembeza kichapo na wamemchezesha kwata Mrusi ile mbaya licha ya kuwa mrusi ana masilaha kedekede." Je, hapo Ukraine kasifiwa au katukanwa? Nyingine hii hapa:........... Hapo mlinzi kwa hasira akamkemea Iguro, "Wewe mshenzi nini. Wenzio wanakula hapo halafu wewe unapenga kamasi hapo hapo? Ondoka upesi nsije nkakuwasha vibao"? Je, Iguro kasifiwa au katukanwa?
Ubaya wa Neno au Uzuri wa Neno mara nyingi huwa upo kichwani mwa mtu mhusika.
Samahani kwa nitakayekuwa nimemwudhi. Nakubali kukosolewa ili na mimi nisiwe mshenzi. 🤣
 
Back
Top Bottom