Hii ni njama madhubuti ya binamu na mumewe au?

Hii ni njama madhubuti ya binamu na mumewe au?

Seneta Wa Mtwiz

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2013
Posts
3,643
Reaction score
4,185
WAKUU

KUNA MWANANGU NILISOMA NA'E A_LEVEL PALE #NDABO (NDANDA HIGH) MIAKA KADHAA ILIYOPITA.

SASA BAADA YA KUHITIMU SHAHADA YAKE TANGU MWAKA JANA
NA SERIKALINI AJIRA NI CHANGAMOTO, MWANA KAONA BORA AENDE DAR KUTAFUTA MISHE ZA KUFANYA JAPO KUPUNGUZA MAKALI YA MAISHA.

KWA KUWA HANA NDUGU WENGINE DAR,
KAFIKIA ALIKOOLEWA BINAMU YAKE (Mtoto wa Shangazi yake)
KULE MITAA YA #YOMBO_DOVYA KANISANI* UKISHAVUKA ILE RELI KAMA UNATOKEA TANDIKA,
KWA MBELE KABISA,
AMBAPO
BINAMU YAKE PAMOJA NA MUMEWE (ambaye anashughulika na ufundi seremala) WAMEJITAHIDI KUPANGA CHUMBA KIMOJA NA SEBULE AMBAYO INA SOFA NA TV.

HIVYO MWANA ANALALA PALE SEBULENI KWENYE SOFA
(Ni sehemu ya maisha Kibongobongo).

****
KWA MUJIBU WA MAELEZO YA MWANA NI KWAMBA,
BINAMU YAKE NA HUYO SHEMEJI YAKE
WAMEMPOKEA VIZURI KABISA,
WANAISHI NA'E VEMA,
KWA AMANI NA UPENDO
BILA TATIZO LOLOTE.

SHEMEJI YAKE AMEMWAMBIA AWE NA AMANI KABISA,
KWA KUWA AMEKUJA KUTAFUTA KAZI,
AKAE PALE NYUMBANI HATA MWAKA MZIMA MPAKA PALE ATAPOPATA KAZI,
PIA ASISITE KUMWOMBA MSAADA WOWOTE (Kama upo ndani ya uwezo atamsaidia tu)
NA
KILA ASUBUHI ANAMUULIZIA RATIBA YAKE YA SIKU,
KISHA ANAMPA NAULI YA KUKIDHI MIZUNGUKO YA KUTWA NA POKETI_MONEY KIDOGO.

KWA MFANO LEO,
ALIPOMWAMBIA KUWA NAENDA KWA RAFIKI YANGU
Seneta WA Mtwiz ANAYEISHI PANDE ZA *MBWENI TETA (Kwa Kisukari)*,

SHEMEJI YAKE KAMPIGIA MAHESABU KUANZIA NAULI YA DALADALA KUTOKA Dovya HADI Tandika,
Tandika HADI SIMU2000,
Mawasiliano HADI Boko_Magengeni,
KISHA NAULI YA BODABODA 1,500/= KUTOKA
Boko_Magengeni HADI Kwa Kisukuri,

KAMPA NAULI YA KWENDA NA KURUDI NA HELA YA AKIBA BILA KUMUOMBA WALA NINI!!!

KWA KIFUPI,
HUYO SHEMEJI YAKE ANAONEKANA KUWA NA ROHO NZURI SANA.
******************

SASA MWANA KANILALAMIKIA KUHUSU TATIZO 1
KWAMBA,

TANGU MWANA AFIKE MJINI HII NI WIKI YA PILI,
ILA KILA SIKU UKIFIKA MUDA WA KULALA MWANA HAPATI USINGIZI KABISA!!!!

YAANI KILA SIKU USIKU
KILA BAADA YA DAKIKA KADHAA MWANA ANASIKIA MLIO WA MTINGISHIKO WA KITANDA UKISIKA KUTOKA CHUMBANI KWA BINAMU YAKE NA SHEMEJI YAKE

" *kwacha! Kwacha! Kwacha! Kwacha! ...*"

KAMA KWA ROBO SAA HIVI,
KISHA MLIO UNATULIA.

BAADA YA DAKIKA KADHAA,
MLIO UNASIKIKA TENA,
" *Kudum! Kudum! Kudum! Kudum! ...*"
****

YAANI MWANA ANATAMANI AAMKE AWASHE TV ILI KU_HARMONIZE SITUATION,
ILA ANAONA JAU TU KUWASHA TV USIKU ULE!

SASA IFIKAPO USIKU WA MANANE ND'O MLIO WA KITANDA UNAZIDI,
" *NGUNDAN! NGUNDAN! NGUNDAN! ...*"

YAANI INAFIKIA HATUA MWANA
ANAONA ASUBUHI INACHELEWA KABISA ILI ULE MLIO USIWEPO!

SASA IKIFIKA ALFAJIRI MLIO ND'O UNABADILIKA TENA,
" *Kwiyo! Kwiyo! Kwiyo! Kwiyo! ...*"

----------
SASA MWANA
ANASHANGAA,

1.
KWA NINI YULE SHEMEJI YAKE ASITENGENEZE KITANDA IKIZINGATIWA YE' NI FUNDI SEREMALA???

2.
KWA NINI TANGU YE' AFIKE HUU MLIO HAUNA MAPUMZIKO
(Yaani ni kila Siku ifikapo mida ya kulala mlio unaanza kudufua)???

3.
AU KUNA AJENDA YA MADHUBUTI YA KUMTAKA MWANA AJIONGEZE ARUDI #BUNDA???

HIVYO
KAJA KUNIOMBA USHAURI,
AFANYAJE?!
************

NIKAMUULIZA MWANA,
TARATIBU ZA NDOA YA HUYO SHEMEJI YAKE KUMUOA BINAMU YAKE ZILIKUWAJE??

MWANA AKANIAMBIA,
KIUKWELI KWA KUWA BINAMU YAKE NI MWEUPE NA KAJAZIA,
WAZEE WALIMTOZA JAMAA MAHARI YA NG'OMBE 19 NA MBUZI 21,
NA WALIMKAZIA,
HAKUPUNGUZIWA HATA MBUZI MMOJA
PAMOJA NA KUOMBA SANA APUNGUZIWE!
HIVYO JAMAA ALI_HUSTLE SANA KUIKAMILISHA ILE MAHARI.

NIKAMWAMBIA,

KUMTOZA JAMAA MAHARI KUBWA TENA BILA PUNGUZO KAMA VILE MNAMKOMOA,
ND'O KOSA KUBWA AMBALO MMELIFANYA HUKO KWENU.

KATIKA MAZINGIRA HAYO
NI NGUMU SANA KUMLAUMU JAMAA KUTOUDHIBITI MLIO WA KITANDA VYOVYOTE IWAVYO!

HIVYO AENDELEE KUVUMILIA MPAKA ATAPOPATA KAZI.

Wakuu,
Au Kuna ushauri wowote wa nyongeza tumpe huyu ndugu?
 
[emoji102] [emoji187] [emoji125]
 
Sipendi kumkaribisha mgeni aanze kuhadithia ya ndani, mimi nimesamehe privacy yangu ili nikukarimu, unayoyaona nyamaza, sasa huyo dume zima linakwenda kuota siri za watu katika nyumba yao.😡😡
 
Atizame lilomleta mjini ndio alifatilie,kama kafata kusikiliza milio ya vitanda na sauti azidi kusogea karibu na mlango,la kaja kutafuta maisha afanye upesi ahame wasije wakamchoka,kwanza maisha sikuizi magumu kupita kiyasi..
 
sasa alitaka binamu yake asipigwe mambo ili uje kumsemea hapa mwambie ajiongeze kama shemej yake ana uwezo wa kumpa hizo elfu tano kila siku bora ampangie chumba na kingine ni bora aende kwa huyo shemej yake akajishkze kwa ufund seremala na yeye apate cha kwake sio kila siku kuomba omba
 
Huyo rafiki yako alikujaje mjini bila kujipanga, mbona huko yombo unapata hata chumba cha 20 kwa mwezi. Ipo siku iyo milio itasikika kwenye kochi analolala afu kashindwa hata kuongozana na huyo shemejio kwenye useremala wakati anasubiri hayo mambo yake yatiki????
 
mwambie aache umbeya afunge bakuli lake lasivyo ntamfukuza kwangu
 
Uncle Maghu kazi tu kweli unayo kwa vijana wa namna hii
 
Hahahhh uyo mshkaji wako ajiongeze hawamtaki apo kwahyo yeye ndo mshangiliaji magoli yao
 
Back
Top Bottom