Hii ni kwa Wanawake tu! Chukua hii

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,643
33,432
Wasalam mama na dada zangu,

Leo naomba niseme na nyie mawaridi ya ulimwengu huu. Huu ulimwengu ni bure bila nyie, Mungu baada ya kumuumba Adam baadae aliona Adam hakukamilika na alihitaji MSAIDIZI! Hivyo kwa ufupi sana wewe mwanamke ni MSAIDIZI! Najua unajua hilo.

Sasa sikia, tena tega sikio uzuri kabisa! Kuwa msaidizi maana yake ni nini! Maana siku hizi wengi mmeenda shule kama wanaume, mna kazi nzuri kama wanaume, mnafanya hadi kazi za kichungaji kama wanaume! Hivyo kupitia usawa huu kuna mipaka mnavuka bila kujua na ulimwengu unavurugika!

Msaidizi ni yule anayefanya kazi ambayo mwenzake hawezi kufanya! Ni mtu anayekamilisha jambo, anayeleta utimilifu. Inawezekana huyo anayesaidiwa hawezi kufanya au kukamilisha jambo fulani sababu ya asili yake ( mapungufu ya kibinadamu), maumbile, au kutokana na majukumu aliyonayo n.k

Hivyo tunapohubiriwa tutafute wenza wa kufafana nao maana yake si mtu mnayeendana kwa namna ya kibinadamu tu! Mwenza mnaofanana ni yule ambaye Mungu atakupa ili ukawe MSAIDIZI (kwa mwanamke). Kufanana ni wewe kwenda kumtimiliza mwenza wako ktk mapungufu yake.

Hivyo kama mtajua nafasi yenu hapo ulipo kwenye ndoa yako, tutaokoa ndoa nyingi na hazitovunjika kwa petty issues kama ilivyosasa na mtatimiza nafasi yenu ya malezi ya familia. Siku hizi mna walimu wengi na mbaya zaidi wengi ndoa zilishawashinda na hutumia matukio machache mabaya ya ndoa kueneza sumu kuhubiri ubaya wa ndoa na hasa mkiambiwa msiwe wavumilivu ule mliokiri madhabahuni.

Usikiuke kile kiapo na kuvunja ndoa bila baraka za Kanisa ulipokula kiapo.Sisemi mvumilie hadi mambo yanayo hatarisha uhai wenu lakini pia msidanganywe muache asili na nguvu yenu ya uvumilivu. Kama ni mtu wa ibada na unaishi kama MSAIDIZI, Familia yako itapona na mwisho mtajenga jamii na taifa bora.

Mama na dada zangu, nyie ndio chanzo cha dhambi kuingia duniani kwa kumtii shetani kupitia Eva lakini Mungu akawatumia nyie pia kurekebisha hiyo laana kupitia Eva mpya (Bikira Maria) kwa kutii ujumbe wa malaika Gabriel na pale pale kupitia Roho Mtakatifu dunia ikapata mkombozi Yesu Kristo, Maria angeweza kukataa maana ni nafsi huru lakini alitii kwa unyenyekevu! Hivyo hata sasa ukengemfu mwingi unaweza kurekebishwa na nyie kupitia utii na kuitambua nafasi yako.

Itambue nafasi yako kama mwanamke na usimame bila kuyumba ingawa mawimbi ni mengi maana nyie ndio mnaojenga jamii. Fanyeni kazi ya USAIDIZI na si kujaribu kuwa sawa na wanaume! Ndio wanaume wana mapungufu na matatizo mengi lakini hao wanaume wametoka kwenye mikono yenu! Ndio mfahamu madhara ya kutotambua nafasi yenu mnaandaa wanaume wabovu ambao ndio akina baba wa kesho.


Chukueni nafasi yenu mponye ulimwengu!


N.B
Leo ni akina mama tu wapumzisheni akina baba. Pia nimetumia mifano kupitia imani ya Kikristo ninayoifahamu lakini dini zingine wanaweza kuelewa maana mantiki ya ujumbe wa Msaidizi ni kwa binadamu wote.
 
Kwahiyi wanawake ndio wakuwe wakuvumimilia madhambi ya wanaume
Unajua wakati wakuvumilia anapitia uchungu gani!?
They go through hell na hakuna wkausaidia kila mtu anakwmabia vumilia
Acheni hayo mambo buana
 
Kwahiyi wanawake ndio wakuwe wakuvumimilia madhambi ya wanaume
Unajua wakati wakuvumilia anapitia uchungu gani!?
They go through hell na hakuna wkausaidia kila mtu anakwmabia vumilia
Acheni hayo mambo buana
Hizo hell zinaweza kuwa ndio kiwango cha moto kinachohitajika kuwafanya bora maisha yenu yote. Sio kila couple kila kitu kitakuwa smooth tu, sometimes going through hell si mauti bali purification! Kama dhahabu vile
 
Wanawake waolewe na vilema ili wawasaidie kufua, kupika n.k


Skuizi gengeni naona wababa wanajazana sana hii inamaana hawajui maana ya mke usaidizi.
 
Wanawake waolewe na vilema ili wawasaidie kufua, kupika n.k


Skuizi gengeni naona wababa wanajazana sana hii inamaana hawajui maana ya mke usaidizi.
Lazima mwanamke abakie kwenye usaidizi, amtimilize mwenza wake kwenye mapungufu yake. Hata kama baba ni mvivu ktk utafutaji au uvivu wowote, kama ana MSAIDIZI atabadilika tu! Hakuna kitu ambacho mwanamke akiamua kukibadili inashindikana.

Hivi mnafikiri wazazi na mababu zetu walikuwa watakatifu sana? Kwanini ndoa zao zilidumu? Tunatafuta justifications nyingi kuhalalisha ndoa kuvunjika! Huko mitandaoni wanaambiana hata ukimkamata mumeo akichit achana nae! Purely evil teachings ingawa kuzini pia ni dhambi lakini kuvunja ndoa unazidi kuongeza matokeo mabaya zaidi ya ile dhambi ya mwanzo!

Leo sitaki kugusia upande wetu akina baba nataka tujikite namna gani akina mama wanachukua nafasi zao?
 
Kila siku shetani anatengeneza vitu vipya kuwakamata wanawake na anajua akiharibu huko wanaume tumekwisha. Hivi vikundi, vikoba siku hizi vinakuja na mengi sana! Mabata, party zisizo na uelekeo na mwisho ni michongo ya mabwana!

Sio vikundi vyote ila kuna trend mbovu sana inaambukiza vikundi kwa vikundi na hata kama mkeo alikuwa mtiifu utashangaa ameijua kidimbwi, amejua mabwana wa wenzie wake za watu! Kidogo kidogo wanageuza fikra zake na kupandikizwa negativity kibao juu ya wanaume (akiwemo mumewe). Utashangaa anaanza kupenda bata kinyume za siku za nyuma!

Jitahidi akina mama na dada zetu, malimwengu yanayowajia yachujeni kwa umakini sana maana nyie ni rahisi mno kuwa brainwashed. Hakikisha kuna mstari huvuki, ukiona uelekeo wa wenzako si mzuri usisite kuachana nao kabla hujaambukizwa fikra zao.

Bado leo nasisitiza wanawake wakisimamia misingi na nafasi zao jamii nzima itapona.
 
Kwahiyi wanawake ndio wakuwe wakuvumimilia madhambi ya wanaume
Unajua wakati wakuvumilia anapitia uchungu gani!?
They go through hell na hakuna wkausaidia kila mtu anakwmabia vumilia
Acheni hayo mambo buana
Wanawake waolewe na vilema ili wawasaidie kufua, kupika n.k


Skuizi gengeni naona wababa wanajazana sana hii inamaana hawajui maana ya mke usaidizi.
Yani umepewa somo badala ujifunze na wewe umekuja na somo lako tena.
 
Kuna uwezekano msaidizi wa baba yenu hakufanya kazi yake vizuri mwisho mmeishia kuwa wavivu mpaka kusoma!!
Hii mkuu mbona ipo had shuleni😁 wengine wakat wanasoma sisi backbenchers tunakuwaga tunasimiliana stori za pisi kali au machungoni😆😆😆 usishangae
 
Hizo hell zinaweza kuwa ndio kiwango cha moto kinachohitajika kuwafanya bora maisha yenu yote. Sio kila couple kila kitu kitakuwa smooth tu, sometimes going through hell si mauti bali purification! Kama dhahabu vile
Na nyie mvumilie hell mkuwe dhahabu kuna mawili kuamua kuvumilia na kuamua kuondoka jmn sisemi muachike ila ukiona miaka mitatu unalia kila siku ondoka kabla hujafa na pressure.
 
Back
Top Bottom